T14 Armata
JF-Expert Member
- Mar 7, 2017
- 12,362
- 41,886
Wewe ndio hujui kitu. Unasema wenye nyumba wanazalisha umeme? Umeme wa nyumbani wa kuwashia bulb tano na TV energy saving ndio unataka utumike kuendeshea vinu vya kuchana mbao?Wewe your outdated,tekinologia ya solar imeishapiga hodi katika mataifa mengi, na zimefanyika breakthrough ya solar panel hata battery.
Hata ujenzi wa nyumba kwenye watu makini wanaezeka kwa solar panels.
Kama hiyo haitoshi wenye nyumba wanazalisha umeme wa ziada kuliko matumizi yake na kuuzia makampuni makubwa ya ugavi wa umeme.
Lakini solar tekinologia imehujumia na makampuni yanayozalisha mafuta.
Nitajie kiwanda kinachoendeshwa na umeme wa jua hapa duniani. Kisha nani kakwambia makampuni ya mafuta yanahujumu.
Tatizo ni moja: Gharama za kuendeshea umeme wa jua ni ghali. Unajua kwa nini mtu atakayegundua njia mbadala na more convenient kutunzia charge zaidi ya Lithium ion batteries atakuwa the next billionaire?
Investors hawatumii kelele na siasa nyingi. Hawana porojo hata siku moja, hakuna mfanyabiashara kichaa atanunua batteries za kuhifadhi umeme kwa gharama kubwa kisha baada ya miaka miwili zipoteze nusu ya uwezo wake, baada ya miaka minne azitupe anunue nyingine. Wakati huo panels zilimuweka gharama kubwa, wataaalam wana kazi nyingi ni wengi na wana elimu kubwa hivo kuchangia staff kuwa kubwa na gharama sana. Staff wa HEP station ni mgambo kuzuia wewe usijitupe uko na stress zako. Mitambo inakaa mihongo hata minne haijaguswa kabisa.
Unajua zile pikipiki za umeme za LINKAL zinauzwaje na zikiisha battery yake ile ambayo hupungua uwezo baada ya miezi hata 20 inauzwaje? Sasa battery heavy za viwanda ziuzwe bei gani hapo kwa comparison.
Nitajie bwawa lolote la kufua umeme hapa Tanzania ambalo lishawahi fanyiwa ukarabati tangu yajengwe. Kule DRC wanatumia umeme wa HEP ambayo haikuwahi kamilika hata. Uganda, Owen Falls iliporekebishwa watu tulitangaziwa wakati imetumiwa miongo kadhaa. Nchi yako inashindwa DART sembuse miradi ya kuharibu kabisa uchumi kama umeme. Umeme na mafuta havina majaribio ya kubahatisha, inflation ya hapo hutoiweza.