Mkuu, sijui upo tayari kujibu maswali yangu haya?
Mkuu, unatumia system ya Watts ngapi( PV module), taa nne za watt ngapi ?
Je. Taa nne zote umezifunga kwenye chumba kimoja ama kila taa ipo kwenye chumba chake? Naweza kujua ukubwa wa chumba zilimo/ ilipo taa yaani upana, urefu na kimo!? Je. Mtambo/ system yako hiyo ipo maeneo gani/ mkoa gani Tanzania!? Je. Panel hiyo/ hizo umezifunga katika uelekeo upi/ orientation ( pembe ya kuinama na uso wa panel umeangalia upande upi yaani upande wa kaskazini, kusini , magharibi, ama mashariki)
Kwa ufafanuzi zaidi, ninaomba maelezo ya vifaa vyote vinavyounda mfumo/ mtambo/ system yako hiyo ya solar.
Nina uhakika ukinipa majibu ya maswali haya kwa ufasaha, wataalamu wetu wa mifumo hii watatupa sababu kwa nini mfumo wako huo haukidhi kiu ya mahitaji yako ya mwanga hapo nyumbani/ofisini.