TANESCO achana na Solar Energy, ni wizi na hasara kwa Taifa

Wewe ndio hujui kitu. Unasema wenye nyumba wanazalisha umeme? Umeme wa nyumbani wa kuwashia bulb tano na TV energy saving ndio unataka utumike kuendeshea vinu vya kuchana mbao?

Nitajie kiwanda kinachoendeshwa na umeme wa jua hapa duniani. Kisha nani kakwambia makampuni ya mafuta yanahujumu.

Tatizo ni moja: Gharama za kuendeshea umeme wa jua ni ghali. Unajua kwa nini mtu atakayegundua njia mbadala na more convenient kutunzia charge zaidi ya Lithium ion batteries atakuwa the next billionaire?

Investors hawatumii kelele na siasa nyingi. Hawana porojo hata siku moja, hakuna mfanyabiashara kichaa atanunua batteries za kuhifadhi umeme kwa gharama kubwa kisha baada ya miaka miwili zipoteze nusu ya uwezo wake, baada ya miaka minne azitupe anunue nyingine. Wakati huo panels zilimuweka gharama kubwa, wataaalam wana kazi nyingi ni wengi na wana elimu kubwa hivo kuchangia staff kuwa kubwa na gharama sana. Staff wa HEP station ni mgambo kuzuia wewe usijitupe uko na stress zako. Mitambo inakaa mihongo hata minne haijaguswa kabisa.

Unajua zile pikipiki za umeme za LINKAL zinauzwaje na zikiisha battery yake ile ambayo hupungua uwezo baada ya miezi hata 20 inauzwaje? Sasa battery heavy za viwanda ziuzwe bei gani hapo kwa comparison.

Nitajie bwawa lolote la kufua umeme hapa Tanzania ambalo lishawahi fanyiwa ukarabati tangu yajengwe. Kule DRC wanatumia umeme wa HEP ambayo haikuwahi kamilika hata. Uganda, Owen Falls iliporekebishwa watu tulitangaziwa wakati imetumiwa miongo kadhaa. Nchi yako inashindwa DART sembuse miradi ya kuharibu kabisa uchumi kama umeme. Umeme na mafuta havina majaribio ya kubahatisha, inflation ya hapo hutoiweza.
 
Mkuu kwanza jipange upstairs.
 
Thanks Mkuu ngoja kesho nimtafute fundi nimpe hayo maelezo yako ayafanyie kazi.
 
Nakazia TANESCO kuwekeza kwenye Njia hizi za Umeme hasa wa Solar ni gape la upigaji...

Kwa wauza vifaa vya umeme wa solar Tafadhali msiwadanganye wananchi wakawaida wasiofahamu kuhusu mambo basic ya kiufundi wakawekeza pesa nyingi kwenye umeme huu huku mkiwapotosha kwa sababu mwanga wa jua ni bure na umeme wa maji unakatika katika ovyo hasa vipindi vya kiangazi na jua kali...

Nawaachia wachangiaji wa mada hii andiko zuri kuhusu HVDC (high-voltage, direct current (HVDC)) na kwa nini kuamua kuitumia at high scale kwa Nchi nyingi Africa ni sifa za kijinga na wizi usiojali kesho ya wengine HVDC Transmission Systems
 
Kama kawaida ya waTanzania, unazungukazunguka tu huelezi kitu kikaeleweka vizuri na wasomaji. Sababu kuu ni kwamba hujui chochote juu ya teknolojia hiyo.

Unachanganya mambo ambayo yote huyajui. Unaufahamu wowote kuhusu umeme unaotokana na nuklia? Unachanganya makubaliano ya kimikataba kati ya Tanesco na makampuni na kuviweka fungu moja na teknolojia za kufua umeme..., jambo linaloonyesha wazi hakuna unachojua kuhusu mada uliyowasilisha hapa.

Duniani kote hakuna nchi inayotegemea njia moja pekee ya kufua umeme. Solar, upepo, nuklia, maji, makaa ya mawe, n.k., zote ni njia zinazotumika kufua umeme, na mara nyingi hutumiwa kwa mchanganyo ili kutotegemea njia moja tu.

Kama Tanesco wanaingia mikataba mibovu na makampuni yanayozalisha umeme kwa kutumia jua, hiyo haina maana kwamba njia hiyo ya solar haiwezi kutegemewa kuzalisha umeme nafuu kuliko njia zingine.

Mada yako haielezi chochote mbali ya kuchanganya mambo na kukufanya uonekane huna ufahamu wowote juu ya mambo uliyoandika juu yake.
 
Umeme wa jua hauwezi kuwa nafuu kuliko Umeme wa maji, Mafuta na Gesi per unit price.

China ni nchi ya pili duniani kuwa na Solar plant kubwa lakini Waliamua Kutengeneza artificial sun (“artificial sun,” a nuclear fusion reactor ). Kwa sababu itawapa alot of Energy kuliko mwanga wa jua..
 
Wakati mwingine ni uungwana kukubali kuwa wewe ni mjinga na pengine mpumbavu inapotokea kitu unachofahamu kuhusu jambo fulani ni matokeo ya ujinga ulio nao.
Sielewi kwa nini uliona kuna umuhimu wa kuanza mchango wako na haya maneno uliyoweka kwenye mstari huo!

Nimesoma ulichochangia katika mistari iliyofuata na kuona angalau mchango wako ni bora kidogo kuliko wake; lakini sikuona "upumbavu" wowote katika mada yake. Lakini pamoja na unafuu kidogo katika mchango wako, sioni maelezo yaliyo muhimu zaidi kukufanya wewe usiwe na "ujinga" wa kiasi kikubwa katika mambo uliyochangia.
 
Eeeeh? Hebu sema tena?

Kwamba: "Umeme wa jua hauwezi kuwa nafuu kuliko umeme wa Mafuta per unit price"? Hebu weka tarakimu zako hapo tuanzie mjadala kwenye hilo!

Kuhusu hao waChina "kutengeneza 'artificial sun'" hili hujaeleza chochote mbali ya kutaka kutukoga tu kuonyesha kwamba umeisoma mahali. Sijui kama unaufahamu wa kutosha kutokana na hiyo "artificial sun."

Sijui kwa nini huoni 'contradiction' katika hayo uliyoandika kuhusu "China kuwa nchi ya pili duniani kuwa na solar plant kubwa...," na hayo mengine uliyoendelea kuyaandika. Wasingeona umuhimu wa 'solar plant' isingewalazimu kuwa na "solar plant kubwa".

Hukusoma niliyoandika hapo juu kuhusu ulazima wa nchi kuwa na "energy mix"?
 
Kwa mtazamo wangu njia rahisi ya kumaliza tatizo la umeme hapa nchini ni kuruhusu makampuni mengine yaje kuleta ushindani kwa tanesco,
Eenheee. Utatufanya tulie sana tena mkuu. Mara hii unatufanya tusahau waliyotufanyia IPTL?

Ninakubaliana nawe kuhusu ubovu ulipo Tanesco. Hebu tujaribu kuwarekebisha na wengine tuwaweke ndani wanapokengeuka.
Lakini pia sikatai pendekezo lako la kuwapa ulaji hao makampuni, mradi tu pawe na mbano wa mikataba tunayoingia nao. Hii ya kuja kuvuna hapa na kutuachia majonzi kama tulivyokwishashuhudia na majaribio yaliyofanyika haikubaliki.
 
Mkuu ingawa binafsi nina bifu na Tanesco ila bado hujatoa maelezo ya kitaalam kutushawishi sisi raia ambao ndio wamiliki wa hilo shirika kuona ubovu wa huo mradi wa Solar Energy.

Nilichokiona hapa ni title tu na content ambayo iko very weak iliyojaa malalamiko tu lakini hakuna lolote la kitaalam humo ndani lenye faida.

Jaribu kuleta sababu za kitaalam tukuelewe kuwa huo mradi ni mbovu.

Labda nikusaidie kidogo tu tueleze kitaalam;

1. Hasara za Solar energy vis a vis hydro electric power, gas , oil.

2. Gharama zake.

3. Unit moja itauzwaje compared na ya sasa.

Mpaka hapo baadae,
Utakapokuja na uchambuzi wa kina hii ni ngonjera kama zingine tu.
 
Labda kama unaulewa wa Masuala ya umeme...

Otherwise naweza nikaongea na wewe kilayman...

Charger ya Simu na battery which one is costly than the other one?


Solar is DC in nature, production ya volt 1 ya DC ni ghali kuliko production ya 1V AC, so technically we gharama haziwezi kuwa sawa kamwe
 
Mleta mada yuko sahihi...

Umeme wa solar ni wizi najibu maswali yako
1. Solar Energy vs Hydro electrict

Solar Energy works on principle of Electrons emission by photos... Hii ni process ambayo photons(Light particle zikigonga metallic surface zinasababisha electrons to move)

Sasa zile solar pannels unaziona 98% kama sio zote zimeundwa kwa Silion katika (Layer 3) ya juu ni N-TYPE na ya chini ni P-TYPE ili uweze kuzifanya electrons zitoke kwenye N-Type kwenda P-Type unahitaji only (Visible Spectrum of specific wavelength 300nm hadi 11Knm) na hii ndio challenge ya kwanza kwenye solar energy inaanzia inaitwa Effeciency... Solar cells zote zina effeciency(Uwezo wa solar cells kubadili mwanga wa jua kuwa umeme) currently maximum ni aroung 20% efficiency (in other words 80% ya mwanga wa jua hupotea bure kabisa)

Kuhusu efficiency inategemea na aina ya material iliyotengeza most efficient material ni Mono Crystalline na gharama zake kuziunda ni ghali nakuhakikishia utapita kariakoo nzima usikute solar panel ya hivi, aina ya pili na common ni poly crystalline hii efficiency yake ni around 10% na ya mwisho ni less effecient ni thin-film hizi mtu wa kawaida kabisa anaweza kuuziwa.

Kwa upande wa Hydro electric yenyewe ni AC nina hakika humu ndani ukiomba mtu akusukie generator ya mafuta inayoweza kuzalisha volt 250 hadi 400 from scratch utapata hata watu 10

2. Moja inakaza gharama
 
Namsikitiaga sana mbogo anayeongelea mazingira wakati hana uhakika wa kula yake ya siku/wiki.
Mazingira yanafaida gani kama watu wetu wanakufa na njaa au hawana uhakika wa kula. Serikali ituhakikishie kula kwanza kwa kuwekeza kwenye vyanzo rahisi zaidi ili excess itumike kuendeleza miundombinu mingine ya nchi na kusaidia wananchi wake
 

Very stupid arguments!
 
Haihitaji kuwa mtaalam wa umeme kujua haya unayojigamba nayo hapa mkuu.

Tatizo la watu wa Tanzania ni kwamba, ukiwa na ujuaji kiduchu juu ya jambo fulani, hapo unajiona wewe umemaliza kila kitu katika eneo hilo, huku hata kueleza unachojua watu wakielewe huwezi. Sasa huko ni kujua kweli?

Unaponiwekea mfano wa "charger ya simu na battery" kuonyesha kuwa unajua tofauti ya umeme unaozalishwa kwa jua na 'thermal' inaonyesha kwamba hujui kitu chochote katika maswala haya.
Tena wewe unadhani kuwa tu DC au AC ndio inayotofautisha sana njia hizi mbili za kufua umeme na gharama yake, hapo inakufanya kuwa na elimu ya kuungaunga katika eneo hilo.

Mimi sina utaalamu katika mambo ya umeme, lakini elimu ya sekondary katika physics iliniwezesha kabisa kujua tofauti ya DC na AC na kwamba kugeuza DC kuwa AC sio swala la gharama kubwa kiasi cha kutaka watu waamini kuwa umeme unaozalishwa kutokana na mafuta ni bei nafuu kuliko ule wa Solar.

Kama kweli unayo elimu katika eneo hili, basi utakuwa na tatizo kubwa la kueleza unachokijua watu wakuelewe. Utaalam wa aina hii ndio unaoliangamiza taifa hili.
 
Bora solar energy tu,Tanesco wenyewe na leo krismas lakini umeme hakuna
 
Unaangalia mbele ya pua yako, unadhani umeona dunia nzima?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…