TANESCO board split on MD Rashidi's fate


- Mkuu Zitto amesema maneno yake yamekuwa quoted kwa nia mbaya, hivi Zitto kama kiongozi alitegemea nini hasa kwa kuja hapa JF na kuandika as he was kwa jina lake kamili wakati sheria za JF ziko very clear kuhusu kuingia hapa kwa majina kamili?

- Unafikiri waanzilishi wa JF hawakuyajua hayo walipoamua kuingia hapa iwe kwa majina ya bandia? Vipi wakuu mbona mnashusha standards zetu hapa mkijaribu ku-defend the indefensible? Zitto anatakiwa kuwa a big boy na kusimamia maneno yake, kama kuna sheria za uandishi zimevunjwa sio tatizo letu members wa JF, ni tatizo la Zitto na hao waandishi, lakini it is none of our business!

- Nyinyi hamuwezi kutulaumu members hapa JF kwaniaba ya Zitto, kwa sababu yeye alipaswa kujua form day one alipoingia hapa kwa jina lake kamili kwamba he was opening himself for anything na haya ndio matokeo yake, I mean tunapenda Zitto aendelee kuwepo hapa, lakini no conditions attached, anaweza kuendelea kama alivyo yaani Zitto au abadili ID na yeye sasa aje na fake ID, halafu atuambie jinsi anavyoweza kutukomboa taifa letu na matatizo yake akitumia fake ID!

Respect.

FMEs!
 

Naona kwa wengine somo dogo sana linakuwa zito kweli kweli.

Huwezi kuthibitisha huyu aliyesema haya hapa JF ni Zitto, kuna sehemu nyingine Zitto alipozungumzia haya offline, on record?

Kama hakuna hizi zinakuwa speculations, innuendo na propaganda tu, in a court of law ushahidi huu unatupwa kama circumstantial at best. Huwezi kutumia maandishi yasiyo verifiable ya online forum kama basis ya habari serious.
 
- Mkuu Zitto amesema maneno yake yamekuwa quoted kwa nia mbaya, hivi Zitto kama kiongozi alitegemea nini hasa kwa kuja hapa JF na kuandika as he was kwa jina lake kamili wakati sheria za JF ziko very clear kuhusu kuingia hapa kwa majina kamili?



Hakuna issue ya jina hapa, wala tatozo sio JF, tatizo ni the manner of JF use as a source na the motive behind


Vipi wakuu mbona mnashusha standards zetu hapa mkijaribu ku-defend the indefensible?


Hukuna anataka kumtetea mtu, tuna moral obligation kutaka vitu vifanywe the right way.


kama kuna sheria za uandishi zimevunjwa sio tatizo letu members wa JF, ni tatizo la Zitto na hao waandishi, lakini it is none of our business!
Its very true sio tatizo letu as JF as a whole, inapotokea waborongaji hao ndio hao hao members wetu tena wa heshima hapa JF, nadhani tunaobligation ya kuwareprimand na naamini ujumbe umewafikia


-
Respect.

FMEs!

Mimi ni miongoni mwa wale ambao wanaamini in being yourself bila mwamvuli wa pen name kusema kwa uwazi mawazo yako at the same time ukubali to pay the price ambayo Zitto ameilipa.

Siungani na msimamo wake wa withdrawer, naamini hizo ni hasira tuu, as times go by, zitapungua na Zitto atarudi tena on bord but this time, more carefully more coutious na michango yake humu ili situmiwe vibaya against him.

Zitto ni zito, hahitaji fake ID kama mwamvuli kuja kuleta utumbo humu kwa vile hakuna atakayemjua, namshauri aendelea kusimama kama Zitto, no matter what come out may na hiki ni kipimo cha endurance yake na pia ni njia ya kupitia tanuru la moto kumthibitisha jee kweli ni jemedari wa kweli sio anataka ukamanda halafu anafika uwanja wa mapa,bano kusikia mlio tuu wa risasi huyoo anataka kukimbia.
 

FMES,

Unfortunately una ji contradict.

Huwezi kusema "Mkuu Pasco, maneno yako ni mazito sana, lakini mnasahau kwamba sisi JF tunachojali ni hoja muhimu kwa taifa" halafu hapo hapo useme "mambo ya sheria za uandishi hazituhusu hapa"

Sheria za uandishi hazituhusu wakati issue nzima imetoka kwenye article ya gazeti? Kama baba yako angeandikwa kasema maneno ambayo hakusema bado ungesema sheria za uandishi hazituhusu? Huwezi kusema unaangalia maslahi ya taifa na hujali sheria za uandishi, maslahi ya taifa ni pamoja na sheria za uandishi. You cannot have one without the other, sheria za uandishi ni subset ya hoja muhimu za taifa, ukiondoa umuhimu wa sheria za uandishi umeondoa kitu kimoja muhimu sana katika mambo muhimu ya taifa, therefore umepunguza "hoja muhimu za taifa.Kama uko makini kuhusu mamabo muhimu ya taifa utajali sheria za uandishi, hata kama ni kubadilisha sheria mbovu, lakini huwezi kusema hujali sheria za uandishi na ukasema unajali mambo muhimu ya taifa, huu utakuwa ni utovu wa ukweli au upotofu wa fikra tu.

Ni sawa sawa na kusema "hapa JF tunachojali ni kukamata mwizi kulinda maslahi ya taifa" na kuendelea kusema "mambo ya sheria na jinsi gani mwizi anakamatwa na kuhukumiwa hayatuhusu". Basically una endorse mob justice, watu kupigana mawe ovyo bila due process, una set bad precedent.Siku moja hata wewe watu wanaweza kukuita mwizi ukachomwa moto, hapo ndipo utaona umuhimu wa kufuata due process. Unaset precedent mbaya kuruhusu viandishi uchwara kuokoteza habari hapa na kuzichapisha bila further verification.

Mtu pekee anayeweza ku-ignore hii principle ya fairness iliyo wazi kabisa ni a Machiavellian partisan courtesant.Ni mtu anayetaka kutumia mjadala huu ili kufikia ends zake za kisiasa tu - au labda na yule ambaye shule imempita kushoto kiasi cha kutoelewa concept nzima ya journalistic integrity- anayeweza kudiscuss utumbo huu ulioandikwa na waandishi uchwara kama serious news.

Kwa taarifa yako tu, journalistic integrity ina play a big part katika transparency, freedom and responsibility of press, rule of law, na vitu vyote hivi vina umuhimu mkubwa kabisa practical - sio theoretical na academic tu- katika mambo yaliyo muhimu kwa taifa.

Mkuu unavyoongea unataka kunishawishi kwamba wewe ni mtu ambaye hajawahi kukanyaga shule, na haelewi umuhimu wa journalistic integrity katika kujenga jamii responsible.

Ukishasema "sikatai kwamba huenda kuna ethics za uandishi zimekiukwa" na hususan kama ethics zenyewe zinahusu verifiability ya the fact kwamba Zitto ni kweli amesema au hakusema, wapi unapata audacity ya ku comment further kuhusu hii issue? Kama kuna utata on whether Zitto amesema au hakusema, utaendaje kuhukumu, kutoa positions and all that?

Mbona logic ndogo tu ya if A then B inatushinda?

Mbona logic ndogo tu ya "If we are not sure that Zitto said this" then "there is no news to discuss" inatushinda?
 
Naona kwa wengine somo dogo sana linakuwa zito kweli kweli.

Blue Ray lazima tufike mahali tukubaliane watu hatulingani katika suala zima la uelewa baadhi ya issue zinazohitaji deep thinking, ni kweli humu JF tuna ma deep thinkers wachache na rundo la mamediocre, huwezi mbadili mediocre into deep thinkers, haya ni mambo ya I.Q, tutaendelea kubishana hapa mpaka asubuhi. Tufike mahali tukubaliane kutokukubaliana ili tusonge mbele.
 
- Mkuu Pasco, maneno yako ni mazito sana, lakini mnasahau kwamba sisi JF tunachojali ni hoja muhimu kwa taifa, ..........FMEs!

Kweli kabisa Mkuu.......

Tunawakubali sana viongozi wa Siasa wanapokuja kujiunga nasi hapa JF.......na tunawaheshimu sana kwa hilo............however ikumbukwe kuwa muhimu hapa ni Taifa..........kama hoja iliyoko mbele ni kwa manufaa ya wananchi........hapa JF tunamkoma Nyani giladi.........hatuangalii makunyanzi....sasa kama Kiongozi amekuja hapa ili "ajifiche fiche" eti kwa kuwa kuna ethics za uandishi wa habari........nafikiri mtu unahitaji kufikiri kwa mara ya pili...........

kuna mazuri yaliyoandikwa magazetini (na mengine kufanyiwa kazi) kutokana na mawazo ya watu hapa JF pamoja na ID zao feki.........

Kuna mambo yaliandikwa hapa na Zitto kuhusu Buzwagi na.....hoja hiyo ilikuwa mali magazetini hadi bungeni.......VIPI kuhus hilo Wakuu.......

Whether ni Zitto feki au ni Zitto halisi....kama anaona hakutendewa haki...still ana nafasi ya kuutarifu umma visivyo..........then awachukulie hatua wahusika...........


Again........Taifa Kwanza!..........hapendwi mtu hapa
 
Mbona logic ndogo tu ya if A then B inatushinda?

Mbona logic ndogo tu ya "If we are not sure that Zitto said this" then "there is no news to discuss" inatushinda?
Blue Ray, mambo ya Logic ndio hayo hayo ya I.Q!
 

Ogah ni kweli hapendwi mtu hapa ni kumkoma tuu giladi, issue hapa sio hiyo, kuna issues ambazo JF hazituhusu, hii JF sasa ni chombo cha habari tena chenye heshima kubwa, JF inatumika kama bonge la source, hivyo kwachangiaji tuu JF ni kutoa habari in a way. Tunawataka hawa wana JF
ambao pia ni waandishi wa magazetini, to play in by the rules wakati wakihamisha habari hapa JF na kupeleka kwenye magazeti yao ili kuuza, wafuate maadili yao. Sisi JF tunaendelea na kanyaga twende.
 
Pasco na Bluray,
Mmeelezea vizuri sana ethics za journalism.
Me kwa mara ya kwanza nilivyoiona hii threas, jambo la kwanza nikajiuliza, Ni sahihi kwa gazeti kuchukua habari katika internet forum?
Na kwanini Iwe Zitto?, wangapi na habari ngapi huchangiwa hapa haziandikwi??ndo baadae nikapata picha kuwa hii imeangikwa kwa nia Mbaya.
Tuachne na hayo, jinsi mlivyoelezea Journalist ethics, mmemaliza kila kitu nashauri members hapa wapitie hii thread waone jinsi mlivyoelezea.
 

Ogah,

Zitto amesema popote on record offline ku validate hii article?
 
Semenya,
Asante kuliona hilo, Spika Sitta aliwahi kusema bungeni, Mafisadi wanamuwinda, wao wanaposti articles kwenye mtandao, halafu wanaquote hizi articles toka mitandaoni kwenye magazeti yao.

Sina tatizo na Thisday/Kulikoni kuitumia JF, wana team nzuri zenye vichwa vya investigative journalism, walikuwa na kila sababu ya kifanya story halali, ila walifanya walichokifanya delibarately. Tatizo lao ni moja tuu, wanakuwa too pesonal mpaka wanageuka kuwa na chukibinafsi dhidi ya watu fulani fulani. Wamejenga chuki binafsi dhidi ya Rashid kwenye issue ya rada, sasa wanamlink na Zitto aonekane part and parcel. This is bad journalism.
 
Pia ukija kugundua kwanini Thisday/kulikoni yaliundwa, yaliundwa kwaajili ya Kuwabomoa watu flani kisiasa, nadiriki kusema Manji alikua wakwanza kukumbwa na mkasa wao.
sasa habari za kuwabomoa kisiasa watu zimeanza kwisha, na habari za akina EL na RA zimechakaa naona wamehamia kwa Kabwe. Maana mpaka kuandika habari ile sijaona mantiki yoyote, na ukiangalia theme ya habari ile yote ni nini?,Ndo maana sishtuki nikiskia kuwa magazeti hao na mengine mengi tu Tanzania yameanza kujiendesha kihasara,sasa wanajaribu kutafta masoko kwa wengine ili wapate faida.
 
Ogah,

Zitto amesema popote on record offline ku validate hii article?

Bluray,

Najua swali lako linahitaji jibu fupi....however

Ukisoma post yangu ya kwanza kuhusu huumjadala utaelewa msimamo wangu kuhusu kauli ya Zitto hapa JF na jinsi ilivyotolewa huko kulikoni........

Zitto alitumia neno "Devils advocate"...........mwandishi alitakuwa kumuelewa Zitto kwa hilo na alitakiwa aliweke wazi pia......si ku-quote on one side of Zitto discussion.........na hence nilimulewa Mh Zitto aliposema ujumbe ulivyowakilishwa.....ulikuwa na nia mbaya........still hiyo ni tafsiri ya Zitto...i.e NIA MBAYA......kwani inatupasa kumuuliza Mhariri/Mwandishi nia yake hasa ni nini...........pengine naye alikuwa anachokoza mada uraiani........huko uraiani kuna ma-"Devils Advocate" pia....au sio?........

Notwithstatnding the above.........si wananchi wengi walio na uwezo wa kuingia ktk internet na kuchangia hoja hapa JF..........wengi wao watasoma kulikoni......very unfortunate watasoma a biased story....(i.e. "Nia Mbaya")........huko uraiani wananchi watamuuliza Mh wao kama kweli alisema/aliandika maneno hayo........

....anyway pamoja na ethics na standards za uandishi pia muelewe kuwa kuuza habari kuna technicalities zake........
 
Lakini wauze c kwa ku destroy image ya mtu au watu, ndo tunarudi tena katika ethics za journalism. kwanini hamtaki kulikubali hilo wakati lipo clear ndugu zangu. Ifike wakati mambo ya ajabuajabu tuyakatae watanzania, ndio itakua njia pekee kuliokoa Tanzania.

kaka hapo juu wewe mwenyewe umekubali ni Bias story, afu imetolewa katika forum ya internet, hiyo pekee inatosha kuupinga na kukemea upupu wa Kulikoni, kuliko kuutetea.
 

Mimi beef yangu ni deeper than that, hata huyo anayesemwa kwamba ni Zitto aliyesema hawezi kuthibitishwa kwamba ni Zitto.

It's not like alirekodiwa kwenye tape na watu wakimuona, au alirekodiwa kwenye video, au alisema kitu publicly kuna mashahidi mwandishi akaandika.

Hakuna ushahidi kama huu, zip zero.

Kwa hiyo hii si news, ni innuendo, propaganda.
'
Na mimi siwezi ku lower bar that low, kwa sababu haijafikia standard ya news.

Ni utumbo fulani ambao mtu ambaye haelewi umuhimu wa proper sourcing tu anayeweza kuu entertain.

Ukisema kuuza magazeti kuna technicalities zake una sound kama unatetea utumbo huu, unless nina ku misread ujieleze una maana gani.
 
Upo sawa kabisa
Ni kama leo aje mtu hapa ajiweke JK, then aandike kitu vyombo vya habari vim quote.

Me sijui sana mambo ya journalism, ile je JF inaweza ikawa proper sourcing kweli?
 
Zito wa JF (haijalishi hata kama si yule Mh.Mbunge) alisema.


"Kinachonipa tatizo ni jinsi watu walivyoline up (jipanga) kuchukua nafasi pale Tanesco ili kufurahisha wanasiasa. Nitawapinga hao kwa nguvu zangu zote......,"
Kauli hiyo inaleta maswali kibao mfano:-

Ni akina nani hao wanaojipanga na wanajipanga kivipi kufurahisha Wanasiasa-akina nani?

Ebu Zito wa JF jaribu kuwa wazi vinginevyo hizi ni tuhuma zisizo na uthibitisho.

Sikiliza, haijalishi kama uliyekuwa unamtetea ni mtendaji mwenye ufanisi au la; hakuna aliyeandikiwa kuwa katika nafasi ya ukurugenzi wa Asasi yeyote ya Serikali kwa milele.

Na ku-line up (suitable candidates) kwa ajili ya nafasi wazi (au inayotarajiwa) kuwa wazi si kosa maana huo ndio ushindaji tunaoutangaza duniani kote katika nafasi za kuteuliwa au za kuchaguliwa ili kuhakikisha kuwa anapatikana mtu anayefaa zaidi kuboresha huduma katika Serikali zetu.

Yawezekana wako watu kibao wana sifa za kazi na uzoefu pengine kuliko yule tu unayemfahamu au mwaminia; cha msingi ni kuwa ‘open minded' na kuwapima wote waliojitokeza au wanaodhaniwa kufaa katika nafasi fulani na kumtetea mwenyesifa zaidi ya wengine wote!

Zito wa humu, tunaendelea kukushauri humu kuwa uachane na sweeping statements na pia zile zinazoibua maswali kibao vinginevyo uwe tayari kuyajibu kama nilivyokuuliza hapo juu.
 
jamani Dr Rashidi alishasema yeye anastahafu, sasa mbona wakina ZItto wanataka kumrudisha tena
 
It is complicated to be a CEO in a government owned institution in Tanzania kwa sababu unapambana na players kibao, ikiwemo CCM. Inawezekana Dr Rashidi amekuwa hodari sana wa kuwawekea ngumu CCM, katika mahela na kupindisha mipango ya shirika. Nafikiri pia Dr Rashidi amekuwa hodari sana wa kuboresha maslahi ya wafanyakazi kwa sababu siku hizi hatuskii tena migogoro ya wafanyakazi katika shirika la TANESCO. Ni wazi pia kwamba, miongoni mwa ma CEO wa mashirika ya umma, Dr Rashidi ana uwezo sana wa kujenga hoja, tena kisomi, na hapa ndipo alipoukoga moyo wa Zitto. Najua Zitto ni mwepesi wa kushawishika kulingana na uzito wa hoja, kitu ambacho ilikuwa rahisi sana alipokutana na Dr Rashidi. Na kwa hili Dr Rashidi atakuwa aliwaacha mbali sana Ma-CEO wengine waliokutana na kamati ya akina Zitto. Lakini ubora wa Dr Rashidi unaishia hapa, hauendi zaidi.

Kwa kigezo cha perforamce, kwa maana ya kufikisha umeme kwa wananchi, majumbani, viwandani, n.k., nafikiri Dr Rashidi anaingia kwenye kundi la ma CEO walioshindwa sana. Katika utu uzima wangu na tangu niingie katika mzunguko wa watumiaji wa umeme hapa nchini, kumbukumbu zangu zinaonyesha kwamba ni kipindi cha Dr Rashid ambapo nchi imeshindwa kutoa huduma ya umeme hata kwa kiwango cha chini kabisa. Huyu ni mtu ambaye ameongoza TANESCO katika kipindi ambacho upatikanaji wa umeme nchini umekuwa ni wa kubahatisha na ubabaishaji kuliko hata kipindi cha NETGROUP ambao tuliwachukia sana.

Sasa ushauri wangu ni kwamba tusipime mafanikio ya Dr Rashid kwa kigezo cha kuelewa mambo, au kupendwa na wafanyakazi, au kupata hati safi ya ukaguzi wa mahesabu; tumpime kwa kufanikisha upatikanaji wa umeme hapa nchini-kwa maana ya uhakika wa upatikanaji na kiwango alichopanua huduma hii kwa wananchi wengi iwezekanavyo. Tukitumia kigezo hiki tutagundua kwamba Dr Rashid alipaswa kuwa ameachia au kuachishwa ukurugenzi, sio jana, bali tangu juzi!
 

Asante sana Kitila Mkumbo kwa hili, kitendo cha kumuweka Rashidi kwenye mzani na kumpima pro na cons zake, kumetufungua macho wengi wetu kuhusu hawa vigogo wa mashirika ya umma.

Its high time now, mzani kama huu wa JF ukaelekezwa kwa ma CEO wengine wa mashirika yanayomater na maisha ya Watanzania, hivyo JF kuact kama 'whistle blower' na 'pressure group' kusaidia kuwaengua viongozi bomu, tusisubiri mpaka mashirika yetu yako ICU ndipo tuanze kupiga kelele.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…