- Mkuu Pasco, maneno yako ni mazito sana, lakini mnasahau kwamba sisi JF tunachojali ni hoja muhimu kwa taifa, mambo ya sheria za uandishi hzituhusu hapa, kutumiwa kwa habari hii kwa nia mbaya kama alivyosema mwenyewe Zitto hakuna uhusiano wowote na context za maneno ambacho ndio hasa interest yetu hapa JF,
- Nijuavyo ni kwamba viongozi wetu kuanzia ngazi za ubunge kama wa Zitto, wanakuwa on duty 24/7 chochote wanachosema to the public kama hapa JF tulivyo ni fair deal kuwa quoted, sikatai kwamba huenda kuna ethics za uandishi zimekiukwa, sasa hayo tuwaachie mahakama ndio iamue kwamba maneno ya Zitto hapa JF ni off the record, lakini sio members wa JF hapo na sisi sasa tunaingilia uhuru wa mawazo wa Zitto, ndio maana tuna mahakama sisi tunaweza kuichambua hukumu iliyotolewa na mahakama, lakini sasa tunaanza hata kuwa mawakili wa Zitto bila ya yeye kutuomba, pleasee!
- Ya sheria za uandishi wa habari hazituhusu wakuu!
Respect.
FMEs!
FMES,
Unfortunately una ji contradict.
Huwezi kusema
"Mkuu Pasco, maneno yako ni mazito sana, lakini mnasahau kwamba sisi JF tunachojali ni hoja muhimu kwa taifa" halafu hapo hapo useme
"mambo ya sheria za uandishi hazituhusu hapa"
Sheria za uandishi hazituhusu wakati issue nzima imetoka kwenye article ya gazeti? Kama baba yako angeandikwa kasema maneno ambayo hakusema bado ungesema sheria za uandishi hazituhusu? Huwezi kusema unaangalia maslahi ya taifa na hujali sheria za uandishi, maslahi ya taifa ni pamoja na sheria za uandishi. You cannot have one without the other, sheria za uandishi ni subset ya hoja muhimu za taifa, ukiondoa umuhimu wa sheria za uandishi umeondoa kitu kimoja muhimu sana katika mambo muhimu ya taifa, therefore umepunguza "hoja muhimu za taifa.Kama uko makini kuhusu mamabo muhimu ya taifa utajali sheria za uandishi, hata kama ni kubadilisha sheria mbovu, lakini huwezi kusema hujali sheria za uandishi na ukasema unajali mambo muhimu ya taifa, huu utakuwa ni utovu wa ukweli au upotofu wa fikra tu.
Ni sawa sawa na kusema
"hapa JF tunachojali ni kukamata mwizi kulinda maslahi ya taifa" na kuendelea kusema
"mambo ya sheria na jinsi gani mwizi anakamatwa na kuhukumiwa hayatuhusu". Basically una endorse mob justice, watu kupigana mawe ovyo bila due process, una set bad precedent.Siku moja hata wewe watu wanaweza kukuita mwizi ukachomwa moto, hapo ndipo utaona umuhimu wa kufuata due process. Unaset precedent mbaya kuruhusu viandishi uchwara kuokoteza habari hapa na kuzichapisha bila further verification.
Mtu pekee anayeweza ku-ignore hii principle ya fairness iliyo wazi kabisa ni a Machiavellian partisan courtesant.Ni mtu anayetaka kutumia mjadala huu ili kufikia ends zake za kisiasa tu - au labda na yule ambaye shule imempita kushoto kiasi cha kutoelewa concept nzima ya journalistic integrity- anayeweza kudiscuss utumbo huu ulioandikwa na waandishi uchwara kama serious news.
Kwa taarifa yako tu, journalistic integrity ina play a big part katika transparency, freedom and responsibility of press, rule of law, na vitu vyote hivi vina umuhimu mkubwa kabisa practical - sio theoretical na academic tu- katika mambo yaliyo muhimu kwa taifa.
Mkuu unavyoongea unataka kunishawishi kwamba wewe ni mtu ambaye hajawahi kukanyaga shule, na haelewi umuhimu wa journalistic integrity katika kujenga jamii responsible.
Ukishasema
"sikatai kwamba huenda kuna ethics za uandishi zimekiukwa" na hususan kama ethics zenyewe zinahusu verifiability ya the fact kwamba Zitto ni kweli amesema au hakusema, wapi unapata audacity ya ku comment further kuhusu hii issue? Kama kuna utata on whether Zitto amesema au hakusema, utaendaje kuhukumu, kutoa positions and all that?
Mbona logic ndogo tu ya if A then B inatushinda?
Mbona logic ndogo tu ya
"If we are not sure that Zitto said this" then
"there is no news to discuss" inatushinda?