Siasa...........! tungeacha mashirika yakawa na bodi huru na kuziwekea malengo na kuzipima kutokana na malengo mashirika haya yangeenda vizuri sana. Siasa zinaingia sana na huyu Rashidi ni mmoja wa CEOs anayewakatalia wanasiasa waziwazi. Wanamchukia sana. Mfano kawaambia Wizara walipe pango la jengo la TANESCO, wizara eti hawataki..... CCM nao wameng'ang'ania Rest House ya TANESCO dodoma, amewatimua. Wamekasirika. Basi ni matatizo tu..... Sasa kwenye kampeni wanataka waweke CEO goigoi awape pesa maana Rashidi hatakubali na wao wameshazoea.....
Yaani unataka aachiwe tu afanye tu atakacho bila challenge, Uwezo wake utapimwa pia kwa kuwadhibiti hao wanaomwingilia. Kama hawezi kuwadhibiti basi awe na uwezo wa utawala wa kuwafanya wamuunge mkono ktk maamuzi yake mpaka TANESCO isonge mbele.
Mengine yote sema lakini kimsingi si CEO mzuri kama TANESCO inasuasua, labda ni mzuri ktk mazingara ya nchi fulani fulani, lakini hajafikia viwango vya uzuri wa kufanikisha mambo ndani ya TANESCO ya TZ. Unajua kabisa kungekua na bodi huru, labda waliomtangulia Rashidi wangekua tayari wamefanikisha TANESCO kua imara.
Lazima tuwapime watu kwa uwezo wao kupambana na mazingara halisi ya Tanzania pamoja na siasa zake. Sio bodi huru, then anaweza.
Kama Rashidi atatoa pesa kwenye kampeni ya CCM kwa kua na uhakika kua kufanya hivyo TANESCO itaimarika sioni tatizo.