TANESCO board split on MD Rashidi's fate


Yaani unataka aachiwe tu afanye tu atakacho bila challenge, Uwezo wake utapimwa pia kwa kuwadhibiti hao wanaomwingilia. Kama hawezi kuwadhibiti basi awe na uwezo wa utawala wa kuwafanya wamuunge mkono ktk maamuzi yake mpaka TANESCO isonge mbele.
Mengine yote sema lakini kimsingi si CEO mzuri kama TANESCO inasuasua, labda ni mzuri ktk mazingara ya nchi fulani fulani, lakini hajafikia viwango vya uzuri wa kufanikisha mambo ndani ya TANESCO ya TZ. Unajua kabisa kungekua na bodi huru, labda waliomtangulia Rashidi wangekua tayari wamefanikisha TANESCO kua imara.
Lazima tuwapime watu kwa uwezo wao kupambana na mazingara halisi ya Tanzania pamoja na siasa zake. Sio bodi huru, then anaweza.
Kama Rashidi atatoa pesa kwenye kampeni ya CCM kwa kua na uhakika kua kufanya hivyo TANESCO itaimarika sioni tatizo.
 
Tanesco was about to die, it was rashid's ideas and influence mpaka tanesco iko hivyo leo. Aliweza ku lobby ktk mabenki na wakamkopesha karibu 300b ambazo serikali haikuwa imezifikiria kuzipata ili tanesco ipate unafuu japo kidogo, kwa hiyo kwa sasa anaiendesha tanesco kwa maono yake huku akijipa nguvu ya kurejesha mapesa ya mabenki yetu, sasa kama magazeti ya mengi yanashangaa kurejeshwa kwake basi waende kwenye mabenki wakawaulize namna walivyoshiriki kuinusuru tanesco kwa dhamana ya kichwa cha rashid.

Problem hapo ni hao vijana wanaoiongoza wizara, ni so jr kwa rashid wakiwa bot na vodacom, nadhani jk aliangalie hilo pespectively.

Siku njema na kila la heri mzamivuidriss
 


- Mkuu ahsante sana kwa hizi hoja nzito sana za masilahi ya taifa ambazo zinasaidia kuweka wazi kwa nini hatuelewani, lakini kama nilivyosema jana ninapumzika kidogo nitarudi soon na mijadala mingine!

- Punguza dharau na majivuno mkuu, yatakushinda haya kama bado hayajakushinda tayari ni uhsauri wa bure tu!

Respect.


FMEs!
 
HATUDANGANYIKI!!!... Tanesco can never die. Hamna serikali yoyote inayoweza kuachia shirika pekee la umeme nchini life. This is total nonsense. Ukweli ni kuwa Dk. Rashidi kweli alitumia uzoefu wake wa mabenki kutengeneza proposal ili Tanesco ipewe syndicate loan na mabenki kadhaa. Swali ni je, hizo 300bn/- kazitumiaje? Ripoti ya CAG imeonyesha kafanya renovation ya hundreds of millions of shillings kwa nyumba za viongozi wa Tanesco ili wajiuzie bei poa (Mbunge Ndassa alitoboa siri hii Bungeni), pia amenunua magari ya kifahari kwa viongozi wa Tanesco. Halafu tena akatumia zaidi ya 4bn/- kununua magari kutoka kampuni ya Yusuf Manji ya Quality Motors kwa bei ya juu. Huo ndio uongozi bora? Au ni one of the best CEOs of our parastatals kwa kwa matumizi mabaya ya pesa?
 
Bwana Zitto, tunahitaji na wngine ambao watafanya kwa kuyakwepa makosa yaliyopita. Hivi kwnda kmpa mtu mitambo yetu ya Ubungo aendeshe halafu anatucharge kiasi kikubwa kuliko kwao ni busara kweli? Matatizo ya umeme yalianzia enzi za Kidatu kungine kooote tunajidaganya danganya tu.
Waje watu wenye kufikiri tofauti kwa masilahi ya Wananchi maana naona hawa wa maslahi ya Taifa wametueleka pabaya.
 
Na nafasi ya CEO wa DAWASCO nayo imetangazwa kwenye magazeti ya jana. Kamjamaa kalikokuwa pale kaliletwa na EL wakati akiwa waziri wa maji na mifugo. Hakakuwa kamepitia udahili wowote. Kamewavuruga kwelikweli wafanyakazi kaliowakuta pale.
 
Wakuu nitauliza tena swalki langu..
Ni lini na wapi Zitto aliyasema ama kuyaandika haya ya kusifia uongozi wa Rashid..
Maanake nashindwa kufuatilia mada hii

Mkandara,

Tokea uanze kuchangia humu naona hujatulia,
Soma hii hii thread Zitto ameanza kuchangia pg 4 topic #35 ndo alikoanzia kulikologa. Baadaye kuna thread ya Tina na - gazeti kulikoni, Mods ndo wameiunganisha na hii ya tanesco.
Ni kweli kama hujatulia unaweza kuchanganikiwa kwani wengi tumetoka kwenye weekend. Pole.
 
We Zitto njoo ujibu haya maswali, mkutano wa madola umeisha, CEO mzuri wa kuiendesha TANESCO ni yupi?? huyu huyu Dr. Rashid ambaye tunayemjua!!! kumbukumbu zangu humu leo ndo anatakiwa kukabidhi ofisi.

Nenda baba zao la ufisadi, unasubiliwa segerea, hapa wanakuchelewesha tu.
 
Mkuu unaweza kutuambia ni Benki zipi alizoweza ku lobby Rashid wakati serikali ilishindwa..Na hivi kweli serikali iliwapa tanesco kaisi gani vile?.. maanake tusichanganye vitu hapa.
Kisha nambie kuna tofauti ipi kati ya Tanesco hii ya Rashid na ile iliyotangulia... Naomba somo klidogo nipate kuelewa zaidi.
 

Mkuu FMES waache watu kama hao.
Kwa kawaida watu kama hawa huwa wamejipiga" Tangayika Jack" na ku assume kuwa wanafahamu kila kitu.
Lakini mtu aliyejipiga "Tangayika Jack" utamjua kwa kutembelea ncha za vidole na kongea mambo ya kufikirika.
He has no firm contact with the ground ,what ever he/she propounds is what he has read not experienced.
Hakuna jingine ila kuwakaribisha into the mad real world.
 
Mbona watu mnabaki kusema Dr. Idris ameshindwa bila kutoa data? ameshindwa vipi? mnasema TANESCO inasua sua hamsemi inasua sua vipi kama ni umeme ilitakiwa izalishe kiasi gani na kiasi gani kinazalishwa kuna hasara kiasi gani? Naona hata FEM naye anongelea hisia tu mpaka anaenda kulala hajasema vitu kwa figures??? TINA yeye amekazania ukarabati wa nyumba jambo ambalo lazima lilikuwa kwenye plan na liliidhinishwa na bodi bila shaka. Mnataka kusema Zitto amekuwa anaongea kwa ushabiki lakini amesema kwa figure mwenye kubisha urgument za Zitto basi naye aje na figure kujustify anachotaka kusema.


 

Mbogela , the pros and cons za thread hii na argument nzima zimekwisha jibiwa katika several presentations hapo nyuma.
Whatever will be said now will just be a repetition of the obvious stated facts and later opinions.
So long as Zitto JF ameamua kukaa kimya nafikiri hii thread ife kifo cha kawaida.
Mwenye akili ataconclude apendavyo
 
kuna maswali kwa bwana Zitto, yeye kwa mtazamo wake alishauri hiyo MITAMBO YA DOWANS ITAIFISHWE NA IWE MALI YA SERIKALI kutokana na hasara na mikataba ya ujinga ya hapo Tanesco, Lakini CEO bora kabisa Tanzania aliomba AINUNUE HIYO MITAMBO, SASA SWALI INAMAANA HUYO CEO BORA HANA UPEO KAMA WA ZITTO WA KUJUA KWAMBA HIYO MITAMBO SIO YA KUNUNUA BALI YA KUITAIFISHA TU

SWALI LINGINE HIVI KWA NINI ZITTO NA HUYO BWANA RASHIDI WOTE WALIKUWA NA ALTERNATIVE YA KUTUMIA MITAMBO YA DOWANZ KAMA KINGA DHIDI YA TATIZO LA UMEMEME

SASA HAYO MAWAZO YAO YANAYOFANANA TUYAUNGANISHE VIPI NA HILI LA ZITTO KUMSIFIA Dr KUWA NI CEO BORA AMBAYE ANAFAA KUOPNGOZA TENA TANESCO

ZITTO UR TOO OBVIOUS
 
 
Moja tu - Amechukua u CEO pakiwa na hasara ya 162bn kwa mujibu wa audited accounts za 2006. 2007 hasara ilishuka mpaka 67bn. 2008 imeshuka mpaka 30bn na

mpaka june 2009 tayari TANESCO ilikuwa imebreak even. Kama sio mgawo wa Septemba, Oktoba na Novemba wangepata faida mwaka huu.

Mbili - kwa mara ya kwanza Taasisi za fedha zimekopesha TANESCO 400bn na wana service mkopo huo bila tatizo lolote na hivyo kuweka mazingira ya kukopa zaidi.

Tatu - Shirika lina mpango wa muda mfupi, wa kati na mrefu wa kuzalisha na kusambaza umeme. Miradi yote ya kuanzia mwaka jana imekwamishwa na Serikali kama Mhisa mkuu.

HTML:
Nne - Sasa Shirika lina rejesta ya mali zake zote (zenye thamani ya 1bn usd) na wakati Rashidi anaingia CAG alitoa disclaimer audit opinion kwa kuwa pamoja na mambo mengine Shirika halikuwa na orodha na thamani halisi ya mali zake. NHC wana tatizo hilo na Kamati ya Bunge ya Mashirika ya Umma iliwatimua na mpaka leo hawajaweza kufanya kama TANESCO.

Tano - Yupo very clear anataka Shirika lifike wapi kwa muda gani. Kwa mfano kama Mhisa pekee (serikali) angetekeleza commitment zake na faida iliyotarajiwa mwaka huu ikawa realised, lengo lilikuwa ni kustain faida kwa miaka mitatu ili TANESCO iuze hisa zake DSE na hivyo public listed company - kuongeza uwazi kwa mujibu wa masharti ya PLCs.

Niendelee?
___________________________________________________________

Endelea....lakini this is the very minimum this guy was supposed to be doing. Tatizo moja ambalo tunalo katika nchi zetu hizi zisioendelea ni kwamba ni watu wa kuridhika mno, na mara nyingi tunaridhika na mafanikio ambayo hayashikiki. Mimi nakataa kupima ufanisi wa huyu bwana kwa vigezo hivi vya kukopesheka,kupunguza deni, kupata clean audit certificate,etc maana huo ndio wimbo ambao Mkapa aliouimba kwa miaka kumi, lakini hiyo haikumaanisha kwamba baada ya miaka kumi wananchi wetu walikuwa na hali bora zaidi.

Zitto, naomba uendeleze hoja, na safari hii naomba uteremka na takwimu zinazoonyeesha kwamba hali ya upatikanaji wa umeme-kiwango na ubora-umeboreka katika kipindi cha Dr Rashid. Hayo uliyoyataja yote ni in-house matters ambazo ni za kiutawala, ambazo mpaka sasa hazijaji-translate katika kutupatia umeme. Serikali hii ilituahidi ilipoingia tu madarakani, naamini kwa kuhakikishiwa na akina Dr Rashidi, kwamba mgao wa umeme ni mwisho, utakuwa historia. Lakini ni kipindi cha serikali hii na uongozi huu wa TANESCO ambapo tumekumbana na matatizo ya umeme kwa kiwango cha kutisha. Ndio maana mimi naendelea kukataa kumpa sifa hiyu bwana kwa vigezo vya index vya akina Mo Ibrahim.
 
Mashirika Mengi aliyo pitia Dr Idrissa iwe BOT, NMB, TANESCo ni makambuni yakupata faida at a probability rate ya 99.9% kwa hali ya soko lilivyo Tanzania, BOT haina mshindani, kwa NMB soko la fedha lina Obvious market na mtu akitaka kuona kama huyu jamaa alifanya kazi nzuri zaidi ya wengine walinganishe hiyo NMB, NBC, pili walinganishe hiyo NMB wakati wake na baada ya yeye kuondoka , na Hata Huko Akiba Commercial Wanaweza kufanya hivyo hivyo kipindi chake na baada ya kuondoka, TANESCO kwanza halina ushindani, pili mahitaji ya Umeme ni makubwa kuliko uzalishaji, sasa Kiongozi yoyote atakaye liongoza shirika hili au mashirika haya akapata hasara tutamshanga, na akitengeneza faida hilo ni wajibu wake na sio kwamba ana uwezo uliotukuka ndio akaweza kuliwesha shirika hilo kupata faida.
Sasa kwa kuwa Viongozi wengi au watawala wetu wanaelewa hivyo ndio maana wanacheza na shirika hilo kwani wanajua pale ni sawa sawa na Gold mines, ndio maana wana kuja na vijimradi vidogo vidogo ambavyo wao wanaweza kuwekeza ili waweze kuimiliki taifa hili kiuchumi na kiutawala na kuwahakikishia familia zao kipato bila kufanya kazi, kwana bill wanazo tuwekea ni za ajabu maana hakuna competition, pili soko lisilo na ushindani lipo.
Hivyo ili mtu au watu tuweze kumpongeza mtu kwamba ni CEO mzuri unatakiwa uangali mambo mengi, eg mtaji uliokuwepo, matumizi ya maendeleo, matumizi ya kawaida, mikataba ya uzalishaji iliyo kuwepo, maana wengine wali endesha wakati mikataba mizuri ilikuwepo wengine wakati mikataba mibaya ipo, wengine wakati mtaji upo, wengine mtaji hakuna nk nk.
unaweza kukuta kuna CEO mzuri tu kwenye sekta nyingine, lakini kwa sababu hatugusi kwa mambo yetu ya kila siku tukamruka au tusimuone, au kwa kuwa shirika lake ni la huduma, hatuoni financial profit, hivyo ulinganishaji wetu wa Tanzania unaangali zaidi viashiria vya utawala bora. Kwa mfano siku hizi baada ya serikali kuelewa au kujitoa , wafanyakazi hulipwa vizuri zaidi kuliko ilivyo kuwa miaka 20 iliyopita, composition ya Bodi umebadilika kidogo toka enzi Zile za Akina Mzee Songambele , kuna usimamizi zaidi wa Donors (IMF, World bank na tasisi zingine zinazokopesha hayo mashirika) kuongezeka kwa kelele toka kwa watu ikiwemo JF, wabunge, magazeti nk nk.
 
Swali rahisi. Mtumiaji wa umeme na yule ambae angependa kutumia umeme amefaidika vipi na uongozi wa Dr. Rashid. Tanesco? Hayo ya ku-break even kwa sababu hamuwalipi Dowans na IPTL tuweke pembeni. Mimi, Fundi Mchundo kama mtumiaji wa kawaida wa umeme amenifanyia nini toka ashike usukani?

Amandla..........
 
Hatimae Field Marshall ame surrender na kuweka silaha chini. Miaka kenda ya majivuno na vitisho eti yeye ni sauti ya umeme mara hii kakutana na mionzi mikali ya kibluu kwishey.

Mie nilidhani ni Field Marshall kweli kumbe wa udongo!
 
Nadhani msingi wa mtizamo wa Zitto kwa Dr Rashid ni kuwa ameweza kuitoa Tanesco from CHAOS to state of NORMALCY na angependa kuona anapata muda zaidi ili kutumia hiyo state of NORMALCY to ensure EFFICIENCY or even EXCELLENCY on services kama wengi mngelipenda kuona inakuwa.


Is it wrong or Is it abnormal to have such kind of stand?

Sometimes lets avoid political expediency in every things…..

It looks like being pragmatic and optimistic is sinful in our society?



omarilyas
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…