TANESCO board split on MD Rashidi's fate





- Sasa naenda kulala kesho nitaendelea ila for now naachia wananchi waamue mchele na pumba zilipo, pole pole huwa sina haraka mpaka nitakufikisha panapotakiwa!

Usiku mwema mkuu!


FMES!
 
- Sasa naenda kulala kesho nitaendelea ila for now naachia wananchi waamue mchele na pumba zilipo, pole pole huwa sina haraka mpaka nitakufikisha panapotakiwa!

Usiku mwema mkuu!


FMES!

Ushasema unaenda kulala mara ngapi wewe.

Sema midongo imekuzidi uzito tu.

Hapa tunakupiga mawe hata ukilala utayasikia kwenye ndoto urudi kupata dozi zaidi na zaidi.
 
Wale watu wenye doubts na uwezo wa Dr Idris , ningeomba kuwauliza maswali.
Kwanza Idris amekuwa CEO wa Tannesco kwa muda gani? Alirithi Tanesco ikiwa katika hali gani? Alikuwa na resources zipi? Kwa sasa Tanesco iko katika hali gani ikilinganishwa na wakati akiingia? Serikali/wanasiasa wame mpa ushirikiano kiasi gani?
Lazima tuwe wa kweli, hata kama mtu yeyote angepewa resources 200% over the required amount na bila kuingiliwa na wanasiasa, hiyo turn about mnayotaka isingeweza kupatikana kwa huo muda Dr Idris amekaa.
Hata mtu ukilima mazao ya biashara hutegimei kupata faida overnight ndiyo itakuwa Tanesco.
 
- Kabla sijaendelea na ku-present kesi yangu, naomba uweke wazi huyu uliyekua unamjadili hapo juu ni Zito yupi? Mbunge au siye?

- Nikirudi nitakuja kuendelea na kesi, lakini please jibu kwanza hili swali?

Later saa ya mzigoni sasa!
Bwa! ha! ha! ha!

FMEs!
 

- Haya huyu ni Zitto yupi mkuu? Mbunge au?

- Later!


FMEs!
 
Obviously huna the slightest idea ya tofauti kati ya scrutiny level inayotakiwa na kukubalika baina ya discussions za members online na newspaper report.

I know that without help you cannot even comprehend the above statement, najua ulivyo mtupu!

You have absolutely no idea, una ramble tu kama caveman.

Endelea tu kuji expose, the more you do this the more credibility you lose because serious people see you for who you are. A joker who cannot fin his bearings in an issue as simple as this.

Then unataka "kukata issue"!

Unachekesha kwelikweli.

Mimi naendelea kukubalasa wewe na waandishi wako uchwara.

Naona wanaendelezaa upuuzi wao hapa

Mtu na akili zake anawezaje kutetea upuuzi kama huu?
 
 
 
 
 
I m actually amused.Mtu ambaye hana mke amepiga mke.MMtu ambaye hana record hata ya complain za nosy neighbor ana rekodi polisi.Mtu ambaye hakusoma hata kwa kutumia mkopo wa mnyamwezi aliokuwa na access nao kasomeshwa na serikali ya tanzania.Tena kaonekana DC.

Mara nimepata degree kwa miaka saba kwa kutumia hela za serikali ninayoikandya (unanijua vizuri sana kwa minajili hii)

Mara hunijui.

The king of incoherency. Najitahidi kutafuta mtu aliye more incoherent humu ndani sijampata bado.
 

Mkuu, wewe usiye na doubts naomba nikukumbushe tu kwa hii hotuba ya huyo aliyemteua Dr. Idris.

Mwezi wa tano mwaka 2006, Raisi Jakaya Mrisho alikuwa na haya ya kusema kwa wadau wa Shirikisho la Wenye Viwanda Tanzania (CTI).

.
Miezi sita baadaye
Dr. Idris Rashidi akateuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Tanesco. Miaka miwili ikapita na sasa mwaka wa nne unakatika na ad hoc measures bado ziko pale pale na reliable power supply nchini bado ni ndoto. Ajabu ni kwamba Dr. Idris naye bado yuko pale pale na kuna mbinu zinafinyangwa aendelee pamoja na kushfa lukuki alizozivaa utafikiri shati. Si hayo tu amewahi hata kudiriki kutishia nchi kuingia gizani kama mitambo ya wizi haikununuliwa.
Hiki kiburi kinatoka wapi na kinatokana na nini - miaka minne ya kuongoza shirika linalohodhi nishati muhimu kama umeme, leo anathubutu kutamka huu uchuro ! God dammit, halafu kuna mtu anajitokeza kumtetea eti best CEO, come on, give me a break ! Halafu ndani ya JF home of great thinkers wanatokeza watu kumuunga mkono, I give up.
 

Kuna factors nyingi zinazochangia kwa organisation isifikie malengo and part of them ni foreseeable and unforeseable factors. Rais alipozungumza alikuwa anaelezea vision ya yake na expectation zake kwa Tanesco.

Unapozungumzia competence ya mtu zungumzia facts na usiwe subjective kwa kuelezea hisia zako eti una give up!! Give up baada ya kutoa facts na sio kuwa bias pasina kuwa na vigezo vinavyomtuhumu Dr.Idris JF wengi wetu tunajitia wataalam but naona mara nyingi tunapiga siasa tu. Competence ya mtu inapimwa na results na sio blah blah!!! tupeni facts zinazoonyesha kuwa hafai idrissa. Na tutoe relative performance metrics za idriss against other prior management. Venginevyo mnatuelezea hisia zenu which mwisho wa siku tunaweza kusummarize as majungus.

Hatuna critical analysis ya kwanini Tanesco kwa Dr. Idris haifai zaidi ya majungu majungu. Hatuna facts zinazomtoa Dr. Idriss katika UCEO badala yake mnatoa arbitrary arguments ambazo to me ni rubish and does not make any sense nadhani mjadala tusummarize kuwa hakuna hoja inayomzuia Dr. Idriss asiwe tena CEO zaidi vimajungu majungu vya watu.

Nakaribisha hoja!!!
 
Mag3. My sentiments exactly. Huyu bwana hajawahi hata kuweka wazi ( isipokuwa pengine kwenye hizo ripoti kwa waheshimiwa wakina Zitto) ni namna gani tutatoka kwenye haya matatizo tuliyo nayo. Anapojitokeza ni kutishia nyau; nitajiuzulu, nisilaumiwe kwa yatakayotokea n.k.
Hatufai, period.

Amandla.......
 

Basi wewe weka facts za kuonyesha kuwa huyu bwana anastahili hiyo sobriquet ya kuwa ni one of the best CEOs in this country of ours.

Huko kulinganisha na predecessors wake unataka tuanzie wapi? Kwa wakina Kasambala? Au unadhani Tanesco ilianza na Net-Group?

Amandla.......
 
According to Zitto,

"Moja tu - Amechukua u CEO pakiwa na hasara ya 162bn kwa mujibu wa audited accounts za 2006. 2007 hasara ilishuka mpaka 67bn. 2008 imeshuka mpaka 30bn na mpaka june 2009 tayari TANESCO ilikuwa imebreak even. Kama sio mgawo wa Septemba, Oktoba na Novemba wangepata faida mwaka huu.

Mbili - kwa mara ya kwanza Taasisi za fedha zimekopesha TANESCO 400bn na wana service mkopo huo bila tatizo lolote na hivyo kuweka mazingira ya kukopa zaidi.

Tatu - Shirika lina mpango wa muda mfupi, wa kati na mrefu wa kuzalisha na kusambaza umeme. Miradi yote ya kuanzia mwaka jana imekwamishwa na Serikali kama Mhisa mkuu.

Nne - Sasa Shirika lina rejesta ya mali zake zote (zenye thamani ya 1bn usd) na wakati Rashidi anaingia CAG alitoa disclaimer audit opinion kwa kuwa pamoja na mambo mengine Shirika halikuwa na orodha na thamani halisi ya mali zake. NHC wana tatizo hilo na Kamati ya Bunge ya Mashirika ya Umma iliwatimua na mpaka leo hawajaweza kufanya kama TANESCO.

Tano - Yupo very clear anataka Shirika lifike wapi kwa muda gani. Kwa mfano kama Mhisa pekee (serikali) angetekeleza commitment zake na faida iliyotarajiwa mwaka huu ikawa realised, lengo lilikuwa ni kustain faida kwa miaka mitatu ili TANESCO iuze hisa zake DSE na hivyo public listed company - kuongeza uwazi kwa mujibu wa masharti ya PLCs."

Hizi figures zinaonyesha kwanza kiongozi wa pale juu anavision na shirika analoliongoza na sio kukosa mwelekeo. Na pili anaazma ya kulinasua shirika katika ukata. Kuhusiana na benchmark kwanza jiulize ni wakati gani shirika lilianza kuwa na madeni na matatizo ya kifedha ndio utapata jibu la benchmark ya kumeasure relative performance. Pili no one had the audacity of facing ministers ask for the repayment of the outstanding debt ya shirika. Jamaa amewaface walipe hayo madeni je hao mabest CEO wenu akina Kasambala walikuwa wapi??? Unaijua sababu ya NetGroup wakatimka walikuwa wakiwadai madeni makampuni ya vigogo ambao walikuwa hawalipi wakipitisha vimemo wasamehewe madeni wazungu wakaona huo ni ujinga na upumbavu.

Tatu hivi jamani mnaosema eti Dr.Idriss alitumia uzoefu wake kusecure almost 400bn from Financial Institution mna akili kweli. Unadhani kuna benki particularly private banks zikakubali kutoa pesa tu kwasababu ya kumfahamu mtu pasina kuwa na facts figures and vision inayomake sense. Mie kwa experience yangu ya benki sidhani hilo linawezekana ndio uzoefu matters but audited financial statements, liquidity, collateral are among other factors zinazoangaliwa kwasababu mteja akidefault MD au GM unakuwa katika kiti moto katika board. Je utaka kutwambia wale wenye mabenki walikuwa wendawazimu kuwakopesha pesa zote.

Sasa hivi hadi mashirika ya nje ya kipesa yanafikiria kuikopesha Tanesco maana watanzania tuna mentality ya mzungu yuko right je nao wendawazimu acheni majungu na uzushi usio na maana. Takataka kama hii ndio imesababisha ATC ikafa hivi hivi shirika lina madeni kibao, haliendeshwi kifaida wadaiwa hawalipwi mwisho wa siku shirika linakufa. Serikali wameibail out but kama kuna poor management do not expect miracles.
 
Sasa unaleta hearsay na kudai kuwa ni facts? Ingekuwa facts basi angebandika angalau sehemu ya hizo audited accounts. Na hizo round figures hazimo kwenye facts.

Kufanikiwa kukopeshwa si dalili ya utendaji bora hasa katika mazingira ya kwetu. Swali ni kuwa huo mkopo wameufanyia nini?

Tuambie hiyo mipango ni ipi? Target zao ni zipi? Na ni miradi ipi iliyomo kwenye hiyo mipango iliyokwamishwa na serikali?

Kuwa na rejesta ya mali yeyote ni kitu ambacho any CEO woth his or her salt atakiwa kufanya. Kwamba waliomtangulia walikuwa incompetent hakumfanyi yeye kuwa the best!

Huo u-clear amemweleza nani? Wewe haujui umategemea maneno ya Zitto. Badala ya kunong'onezana basi aweke wazi hiyo vision yote ili wote tuione. Unfortunately, muda umeishapita na sasa hivi ni too late.

Hao wakina Kasambala kwani walikuwa wakiidai serikali? Huyu unayemtetea wote tunajua kuwa yuko karibu na mheshiwa rais na inawezekana hicho ndicho kilichomwezesha kudai hayo madeni. Swali ni kuwa baada ya kulipwa, amefanyia nini?

Hamna ulichosema ambacho kimenibadili mawazo. Aondoke. Hatufai.

Amandla....
 

Tupe wewe facts basi badala kutoa subjective arguments sema kwanini aondoke na kwasababu zipi?

Unadai katika thread iliyopita kuhusu nyumba je swali langu hujajibu board ilikuwa wapi wakati huo?

Kuhusu ukaribu wa Dr Idriss na Rais again majungu unahakika gani alitamka wazi? au umesoma katika GlobalPublishers?

Acheni uzushi wa kijinga na majungu nipe facts kwanini Dr Idriss aondoke mniconvince but out of 44 pages of this thread hakuna hoja wala argument inayobadilisha mawazo.

Mie naona Dr.Idriss anafaa na probably kama Zitto alivyosema he is one of the best CEO katika Parastatals zetu
 

Mangapi bodi zetu wamepitisha ambayo ni bomu? Kama utetezi wako kuhusu matumizi mabovu ni kuwa bodi imepitisha basi inaonyesha jinsi usivyoijua nchi yako.

Don't flatter yourself. Hakuna anayetaka kuku-convince. Wewe umeshindwa kuleta facts. Mtu ambaye tungetegemea angeweza kutuletea hizo facts ndiye huyo ameleta za ovyo ovyo tu.

Hatujawahi hata siku moja kudai kuwa tuko Tanesco, serikalini, au bungeni kwa hiyo tuna access na hizo facts. Uamuzi wetu ni kutokana na yale yaliyopo kwenye public domain. Na yaliyopo kwenye public domain ndiyo hayo yanayoonyesha udhaifu wa huyu unayemtetea.

Kwani nani kasema kuwa karibu na Rais ni dhambi? Si kila kitu kilichomo kwenye public domain, including wakina Global Publishers, ni majungu.

Mtu wako hatufai.

Amandla.......
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…