TANESCO board split on MD Rashidi's fate

Other members of the TANESCO board of directors are Victor Mwambalaswa, Agnes Bukuku, Juma Bakari, Vintan Mbiro, Semindu Pawa, Beatus Segeja, and Ngosi Mwihava.

Hivi hawa wote kuna hata mmoja mwenye ABC za mambo ya umeme?


na hili ndio tatizo kubwa..tokea mwanzo wakati IR anateuliwa watu wengi walilalamikia uzoefu wake katika masuala ya umeme....walikuwepo watu wenye uwezo hata ndani ya Tanesco ambao walikuwa na uwezo wa kuendesha kampuni....wafanye kama basi TTCL,management ni wafanyakazi wanaojua kampuni nje/ndani....
 
mkataba kati ya tanesco na richmond ulikuwa June 23, 2006.
ambao tanesco walikuwa wanalipa 152m/- per day
mwaka wa fedha wa 2006 umeisha april 2007 ni miezi kumi kasoro tuseme tisa ya malipo kwa richmond.
na kutoka april 2007 mpaka oct ni miezi saba malipo kwa richmond na mwaka wa fedha umeisha april 2008.
na pia bado kulikuwa na mkataba wa IPTL ambao ulisitishwa pia
annual cost ya IPTL ni $55.2m na RICHMOND $54M

ndio maana nikaita zile ni headline figures kwa ajili if u take these into the account utaona nini kimetokea. kupungua kwa hasara kunatokana na kusitisha mkataba kwa ajili wanasiasa wameingilia kati.

sawa rashid hausiki lakini keep in mind kwamba ametoka vodacom akaenda tanesco
sababu za kusitisha mkataba ni political na sio rashid + rex attorneys.

kutokana na maneno yako(zitto) mtu ambaye amepewa mkopo wa bil 400 anataka kununua mitambo ambayo wewe mwenyewe ulisema itaifishwe kwa ajili ni mali yetu. na wewe unamuita huyu mtu the best ceo. the best ceo anataka kununua mali yake mwenyewe. unadhani watu wangekataa kama angeenda kununua GE mipya.

mjadala unakuwa mtamu kama tutajikita kwenye facts badala ya maneno ya mtaani na kisha kuyaweka kama facts.
mwanzoni mwa mwaka jana tanesco imepandisha bei kwa 23% na ilikuwa inataka 40%. connection charges zimepanda kwa 100%.


zitto
kuwa audited na PwC hakumaanishi tanesco ni nzuri bali tanesco imekaguliwa na kampuni nzuri.
na kama hamna matatizo yeyote kwa nini wasiweke hiyo ripoti online au wewe uweke ripoti hapa JF. tanesco ni shirika la umma, na umma unatakiwa kujua nini hali ya kifedha ya tanesco, na wewe ukiwa kwenye tume ya mahesabu ni wajibu wako kuhakikisha tunapata info za mahesabu.
 

Ni nani aliyesema kama si wewe mwenyewe?

Aliyeandika hayo ni huyu hapo "JF Great thinker" Acha kukurupuka usiwe kama sio mjinga!
 

This is classic! watu wanataka uwe kama wao, wanasoma michango ya mwanzo wakiona trend ni kukandika na wao wana bandwagon, ndio JF style ukifanya tofauti wewe fisadi, umetumwa, CCM nk
 

ceo mzuri sio lazima awe anajua mambo ya umeme. hata dr wa sindano anaweza akawa ceo mzuri. na hata mkurugenzi wa benk anaweza akawa ceo mzuri wa hospitali.

je hao wafanyakazi wa TTCl wamefanya nini/mafanikio gani???
 
Other members of the TANESCO board of directors are Victor Mwambalaswa, Agnes Bukuku, Juma Bakari, Vintan Mbiro, Semindu Pawa, Beatus Segeja, and Ngosi Mwihava.

Hivi hawa wote kuna hata mmoja mwenye ABC za mambo ya umeme?

Its not important for them to know ABC za umeme, what matters is theyem., know who appoints them. umesahau tupo Tanzania?
 
This is classic! watu wanataka uwe kama wao, wanasoma michango ya mwanzo wakiona trend ni kukandika na wao wana bandwagon, ndio JF style ukifanya tofauti wewe fisadi, umetumwa, CCM nk

Ni vizuri ukachangia, thread zote wewe ni kulalamika kuwa CCM mnaonewa humu!!! ukichunguza members wengi hawana vyama.

Kwa Mh. Zitto, kama kweli unajibu kwa hizo facts bado hujajibu Mchango No. #94 & #97 tuelezee CEO mzuri kwa utetezi wako huo kwanza, tuachane na mambo ya richmond hata haya ya kawaida??
 
Aliyeandika hayo ni huyu hapo "JF Great thinker" Acha kukurupuka usiwe kama sio mjinga!
Sawa Mkubwa, sasa Huyo Dr kapewa hesabu za darasa la pili 1 =1 kashindwa, sembuse za secondary nk. in the context kwamba kapewa mkopo wa kuongeza tija kwa shirika yeye kaenda kukarabati majengo , sasa huyo utamwita CEO anayefaa.
 
Dr Rashid ninayemfahamu

Kwa bahati nzuri nimeshiriki katika kazi maalum ya pale TANESCO wakati wa kipindi cha NET Group na baada kuingia kwa Dr Rashid pia. Watanzania tuache uchafuzi wa CVs za watu pasipo kuwa na uhakika. Kuna mabadiliko makubwa sana ambayo Rashid ameyafanya ndani ya TANESCO, ambayo ni mazuri na makubwa. Rashid alikabidhiwa mkoba wa lile shirika ukiwa na pumzi inayokaribia kufa. Jambo la kwanza la kuangalia, tazama hati za ukaguzi wa mahesabu za sasa zinazofanywa na kampuni moja ya kimataifa, (Audited financial statements) ambayo imekuwa ikikagua kampuni hiyo tangu wakati wa NETI Group. Utaona kuna mabadiliko makubwa sana. Kutoka Adverse opinions/Disclaimer opinions hadi sasa utaona atleast Qualified opinions. Ukweli ni kwamba Dr Rashid ni kati ya ma CEO makini na wazuri katika nchi hii. Ndiyo, upende usipende, pamoja na kelele nyingi na mapungufu yanayoweza kujitokeza, bado Dr Rashid ni CEO makini. Kwa wanao ongea kwa kutazama maandishi ya kwenye magazeti tu, hawawezi kuelewa!.

Siasa zinapokuwa zimeingia katika professionalism ndipo tunaona kupakwa kwa kinyesi kwa Dr Rashid. Tatizo letu wa TZ mambo ambayo yanahitaji wataalamu tunayawekea kimbelembele cha siasa, hata pasipohitajika!. Tangu tuhuma za Rashid zianze siyo leo, lakini kila siku ni tuhuma tuhuma tuhuma tu!. Hata wasiokuwa na data, ni tuhuma tu.

Jambo la pili, tazama hata maendeleo ya baadhi ya makampuni ambayo Dr Rashid anayasimamia kama Mwenyekiti wa Bodi, kwa mfano benki ya Akiba, tazama miaka miwili ambayo huyu mzee wetu Rashid ameingia kwenye board na kupewa uenyekeiti wa bodi, amefanya mabadiliko makubwa na tunaona benki hii ni kati ya benki ambazo zinakua na kufanya mabadiliko makubwa katika technolojia na utendaji pia, hapa nchini.

Tatizo letu wa TZ tunachonga sana hata pasipokuwa na data za kutosha kuendeleza mchongo!! Utakuta mwandishi wa habari au M- TZ mwenzangu, yeye pekee ni prosecutor, yeye huyo ni Forensic expert, yeye ni Auditor, yeye ni Engineer, yeye Mhasibu nk, huu ni mtazamo hasi. Lazima tufike mahali tuwe tunachonga kwa data, pale panapohitajika, si kuchonga tu!. Tunawasaidia wafanyabiashara kuuza magazeti bure!!. hali wengine wakisubiri pesa za wananchi zitumike kuwanyamazisha kuendeleza uandishi wa habari usiokuwa na tija na uliojaa udaku udaku tu!. Magazeti mengi yanajifanya yanaandika habari za uchunguzi, lakini ukisoma utaona ni UDAKU TU!. Soma hata habari hii ya Thisday, hapo juu; kwa umakini, utaona hakuna investigative journalism inayoonekana katika makala hiyo, zaidi ya kujaa udaku udaku tu!; See this "According to these sources, the TANESCO board of directors chaired by Peter Ngumbulu has already formally recommended the re-appointment of Rashidi - but under controversial circumstances............Ngumbulu was yesterday not available for comment on the implication of a split amongst TANESCO board members (directors) over the Rashidi issue, while acting board chairman Adolar Mapunda flatly declined to comment". Sasa kama hawa Thisday walikuwa wamemkosa Ngumbulu, walikuwa na haraka gani ya kuileta hii habari gazetini, kabla ya kupata uhakika wa taarifa hizi. Hata habari yenyewe haielezi, what are the contravential circumncistances.... Huu ni ubabaishaji katika uandishi wa habari. Hebu angalia, Sources za habari hawajatueleza, hata hizo contravential circumncistances hawajaeleza. Maana yake ni kwamba, sources na taarifa zenyewe wanazotaka kutuhabarisha hawazijui. Isipokuwa wanataka kuuza gazeti tu!

Ninachokiona na ambacho waandishi wengi wa habari wanakosa, ni "Report Writing Skills". Pia ninadhani, wahariri wengi, hawana uwezo mzuri wa kukaachini na kuhariri habari vyema. Pia waandishi wa habari waelewe kwamba kuwa mwandishi mzuri wa habari kunahitaji kuwa na skills zaidi ya taaluma ya uandishi wa habari. Wajitahidi waongeze taaluma, mbalimbali ambazo zitawafanya wawe wanaelewa namna shughuli zinavyofanywa katika makampuni na mashirika. Si ajabu kumkuta mwandishi wa habari aliye andika habari hii katika Thisday, hajui hata Corporate Governance, hajui hata namna masuala mbalimbali yanavyosimamiwa na kutekelezwa katika mashirika na makampuni. Yeye alivyoambiwa Ngumbulu hayupo, basi, akaona ndiyo mwisho wa fikira! Akakimbia kwenda kwenye mtambo kupeleka habari eti Habari hizi nilizoziandika ngumbulu hakupatikana kuthibitisha!!. Hata asijue kwamba suala kama hili ni sensitive, linalohitaji umakini katika kulitolea taarifa kwa maslahi ya taifa. Tatizo wanatoa taarifa kama WANAVYOPEANA TAARIFA ZA MISIBA!!.


Nadhani Thisday nao wamepoteza mwelekeo!! They are more of Majungu, kuliko investigative journalism wanayoiimba kila kukicha!


"For actions speaks louder than words, let us embrace actions more than words!!!!!"
 
.......... ninasafiri kwenda Trinidad kwenye Commonwealth. So najua kutakuwa na maswali kibao nitajibu nikifika huko....

Kila la kheri Mkuu...........mkutano mwema
 

Kaka analysis nzuri sana.

However, is it of the national interest to let the dictatorship of the demagogues to win the day?


Unawajua wanasiasa wetu, unajua sekta yetu ya habari na pia unawajua "wazee wa data" wetu iwe hapa JF ama kwengineko. Unadhani wana uwezo(capacity), haiba (caliber) ama mamlaka ya kimaadili (moral authority) kuachwa kuwa waamuzi wa mawazo ya wananchi na hata kutaka kutuamulia hatma ya nchi yetu?



omarilyas
 
Very good and constructive discussion going on here on the topic.

But here's my one fundamental question before I can jump to any conclusion.

What makes an individual the best CEO/Leader?

Here are the few key areas that may qualify someone to meet that criteria:

Customer service: How well does the company serve its customers

Revenue and Profit: Company financial performance quarterly, semi-annual, yearly and so forth. Any profits/loss and what contributed to the bottom line.

Short term/Long term goals and product development: What are company short and long term goals as well as product development or service improvement to current and future customers. This also includes it labor force development.

Day to day operation: How is the company conducts its business daily? Is there a lot of problems customers face everyday? Employees face any hardship while doing their job?
Why do I have to bribe a customer rep before I get any service?
 
Sisimizi kwanza nashukuru kwa mchango wako, na kama utaweza kurejea kwenye moja ya post zangu kuhusu huyu Dr, ni kwamba on the Face value ni mzuri, ninasema hivyo kutokana na kwanza na elimu yake, na pia hatua alizochukua huko nyuma alipoingia NBC, za kuwauliza wazee wazamani kuhusu wepesi wa file zao, kutokana na hilo namfagilia, lakini tukija kwenye matokeo ya kazi zake, EG Bot U-governor zaidi ya kusisitiza watu wawe na qualification naomba utupe nyama kuonyesha aliweza kufanya hiki , na kile alizui wizi, aliinvest vizuri mali zetu nk nk., lakini navyo kumbuka BOT kulikuwa na ile Kashfa ya DCP na mambo ya akina Chavda/Jetu Patel etc, zaidi ya Hapo kulikuwa na Mkataba wa IPTL, sasa hapa namuingiza Governor wa BOT kwa sababu Mikataba mikubwa ambayo inahusisha utoaji wa Pesa nje lazima iruhusiwe na Governor, na hata hii fedha ya Jersey , uwezekano mkubwa imetokana na IPTL na sio ya Radar, sasa alivyo toka BOT bila kuongezewa tuache hivyo hivyo, ndipo akaenda AKIBA commercial Bank, kama MD , lakini hakuka muda mrefu ndipo akaenda VODAcom, sasa mafanikio ya AKIBA Commercial Bank inawezekana yametokana na mambo mengi kwanza effectiveness ya board, pili ya management, na tatu kuwa ni mali ya watu binafsi sio cha Umma ukimaanisha kumilikiwa na serikali.
Sasa control environment iliyo kuwepo AKIBA ndio inawezekana iliyo leta Tija.
Sasa akaenda VODA, lakini kuna mchangaji moja kasema baadae alishushwa mpaka akawa Mkurugenzi wa Masoko, from CEO, sasa sijui hili utatueleza Nini?
Ok ukija kuhusu Audit Reports, unatakiwa uelewe kuwa na hati safi hakumaanishi ufanisi wa investment bali mahesabu yamekuwa supported na documents na kutumika kwa Accounting Standards, ikiwemo kuwa na asset register, ambayo hapo zamani haikuwepo hivyo kuleteleza kuwa na hati chafu nk, na hapa nisingependa kumuhukumu Dr, kwa sababu hili zoezi lilikuwa in pipeline kutokana na audit report zilizo pita, kwa hiyo kilikuwa kitu kipo in process au kilicho tarajiwa, kitu ambacho hakikutarajiwa na watu wengi ni huku kuwekeza kwenye investment zisizo na tija, na ile hali ya kukosa umeme inayo ikabili taifa kwa sasa wakati umeme ndio roho ya uchumi na maendeleo yetu, na hiyo investment ina ready market na return is alomost assured, hata ukichukulia mkopo, na hii ni wazi world bank na other international financial organisation watakuwa tayari kutoa mkopo kwa hili , ilimradi tuwe na strategy inayo eleweka na sio ya umeme wa dharura. na kingine kuipigia kelele mitambo ya Dowans, sasa ukiweza kunielezea kwenye hayo mambo, ninaweza kusema YES kwa DR.
Mwisho umesema ulikuwa na Kazi hapo, je kutokana na uliyo yaona hapo lini tutaachana na na Hii supply ya vijikampuni vya megawat 100 mia kila mtu analeta kijikampuni kake, jingine lini angalau 50% ya nchi itakuwa na Umeme wa uhakika? na wa bei nafuu? sio huu wa ghali.
 
Other members of the TANESCO board of directors are Victor Mwambalaswa, Agnes Bukuku, Juma Bakari, Vintan Mbiro, Semindu Pawa, Beatus Segeja, and Ngosi Mwihava.

Hivi hawa wote kuna hata mmoja mwenye ABC za mambo ya umeme?

Ngosi Mwihava ni mhandisi na ni kamishina msaidizi wa mojawapo ya vitengo pale wizara ya nishati na madini, hope ana ABC za mambo ya umeme.
 
Pre-emptive strategy...........!

Umpende usimpende Rashidi, ni one of the best CEOs of our Parastatals.

Zitto, huwezi kumkana swahiba wako dr.rashid, tumekuona tangu sakata la mitambo ya dowans. Alipoona ushawishi wake kwa kamati ya Mzee Shelukindo umekwama akakimbilia kwako na bila hata aibu ukapiga parapanda na kucheza ngoma ya dr.rashid kwa mdundo alotaka yeye.

hata akina lowasa & co wanatajwa kufanya mambo mengi. Chadema mlikuja na list of shame pale mwembeyanga wananchi hawakusubri muwapeleke mahakamani lakini walijumuika nanyi kuwanyooshea vidole vya tuhuma za ufisadi nanyi mkashangilia. Leo hii unageuka kipofu kwa kuwa anayetuhumiwa sijui una mapenzi nae, au una deal unataka kufanya nae(labda ulishafanya nae) ndipo unaikumbuka mahakama? Lakini kwa jinsi ulivyotetea ununuzi wa mtambo wa dowans wala hatukushangai kuja hapa kumtetea dr. rashid kwamba is one of the best CEOs!!! hapa si suala la kufuata upepo ila ni suala la kuelewa kwamba huwezi kutuhumiwa tu hivi hivi, kama tatizo ni thisday na kulikoni wanamzushia, si aende mahakamani? Nadhani ushirika ulionao na dr. rashid itabidi watanzania waujue, si bure. Alichofanikiwa kukifanya dr.rashid akiwa tanesco ambacho tutaendelea kukikumbuka ni kutokuwa na mipango mbadala, yaani bila mitambo ya dowans watanzania tukatishiwa kuingia gizani na kweli tukakumbana na mgao.
Jambo lingine tutamkumbuka kwa kuifanya tanesco iongeze kiwango cha ukiritimba. ukitaka kuunganishiwa umeme inabidi ununue nguzo halafu uwape chochote kitu ndo waingize umeme ndani ya nyumba, yaani tanesco imekuwa ni kero kubwa sana nchi hii.
 

Mheshiwa ZItto,
Kwa sifa hizi ulizomwekea Rashid basi labda angefaa kuendelea kuwa Gavana wa Benki kuu na si kuwa Mkurungezi mkuu wa TANESCO japo hata huko Benki kuu nako ana skendo kama hiyo ya wizi wa pesa kupitia ununuzi wa rada. Misimamo yake uliyoitaja hapa haina uhusiano kabisa na ukuaji wa sekta ya umeme nchini kwetu. Sioni badiliko lolote ambalo Rashid anaweza kujivunia ameleta katika ufumbuzi wa matatizo ya umeme nchini mbali ya kutetea ununuzi wa mitambo chakavu ya Dowans ambayo nayo inazusha maswali mengi juu ya integrity yake. Tungefurahi kuona kuwa amepanua wigo wa uzalishaji wa umeme nchini na kupunguza kama si kuondoa kabisa tatizo la mgawo wa umeme. Hapa tungemwona mtu anayefaa kuendelea kuingoza TANESCO. Tuna makaa ya mawe ya kutosha kuzalisha umeme wa uhakika usiotegemea mvua. Na sasa hivi kuna teknolojia za kuyatumia makaa ya mawe kuzalisha umeme bila kuchafua mazingira kwa kiwango kikubwa.
 
Other members of the TANESCO board of directors are Victor Mwambalaswa, Agnes Bukuku, Juma Bakari, Vintan Mbiro, Semindu Pawa, Beatus Segeja, and Ngosi Mwihava.

Hivi hawa wote kuna hata mmoja mwenye ABC za mambo ya umeme?

Yes!
Huyo mwenye bold hapo juu ni mhandisi na amekuwa wizara ya nishati na madini tangu mwaka 1984, anajua details kibao kuhusu wizara na Tanesco, na kwa sasa ni kamishna msaidizi wa nishati jadidifu (Renewable energy) pale wizarani.
 

Kama kawaida kila anapoguswa Zitto lazima ujitokeze.Heheeeeeee
 

Sisimizi hapa umekonga penyewe haswa, fani ya uandishi wa habari siyo tuu imevamiwa na waandishi mamluki, bali pia wamiliki wenye agenda zao.
"He who pays the piper.... wana This Day, keep on playing the tune, according to the calling of of the payer".
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…