William J. Malecela
R I P
- Apr 27, 2006
- 26,584
- 10,400
Zitto huna haja ya kutoka JF, ulichangia mjadala kwa kuonekana ukitumia vyeo vyako vyote vya ubunge na kama Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ndio maana baadhi ya takwimu ulizitoa katika kumtetea Dk Idris zilitokana na hesabu zilizowasilishwa katika Kamati yako.
Hili pia ni fundisho kwako na nakumbuka uliwahi kushauriwa na mwanaJF mmoja kuhusu misimamo unayojiamini kuwa nayo kuwa wakati fulani inahitaji kupitiwa kwa makini.Labda ungekuwa na wataalamu wa mawasiluiano ya umma kwa karibu wangekusaidia nini cha kusema wapi na wakati gani.Lakini ukiacha hilo gazeti msimamo wako wa jana uliwashangaza wanaJF wengi.
Mara kadhaa ulitetea wazi humu kuwa Dk. Idris ni makini na mtawala mweledi, sasa unaogopa vipi kivuli chako jamaa walipoandika ulichokisema hasa kwa kuzingatia ulikotoka na misimamo yako ya nyuma ukiwa mpinga mafisadi,
- Mkuu Tina kwenye hili niko na wewe 100%, Mheshimiwa Zitto chonde chonde mkuu, wewe ni kiongozi wa taifa meaning kwamba 24/7 unakuwa kazini ndio maana tunatumia hela nyingi sana za sisi walalahoi kuwalipa wabunge kama wewe, sasa eti ulikuwa hujui kwamba anytime unapoongea siasa unakuwa unaweka msimamo wako wazi ni halali kwa yoyote yule kuku-quote as maneno yako kama kiongozi na pia ni msimamo wako on the ishu?
- Eti unasema ulikua hujui hilo? wakati unaigia hapa kwa jina lako mwenyewe na hukulazimishwa na mtu? Hivi hukuona wenzako kutoka huko Chadema walianza hapa na majina yao ya kweli walipoona joto ya jiwe wakakimbia na kuja na majina fake, wakiogopa kama sisi walalahoi huku wakidai hawaogopi wanataka kutukomboa!
- Sasa kweli maneno umesema mwenyewe, halafu una-chicken out na visingizio uchwara hapa for what ili tukupe sympathy, Zitto kwa hili hukuonewa na wala hakuna cha kuandikwa kwa nia mbaya, umesema imeandikwa kama ulivyosema, unaruhusiwa ku-recant lakini sio kukimbia kivuli chako mkuu, hivi hili taifa tumelogwa na nani I mean uoga uoga unaogopa nini mkuu? Kama ulichosema ndio unachokiamini inakuwaje saa ya kuhesabiwa inafika unakimbia na kuruka kama kunguru!
- Halafu humu kuna watu wanajaribu hata kukutetea for what? Eti Tanzania tuna sheria inayosema maneno ya mbunge yanatakiwa kuwa quoted akiongea bungeni, lakini sio kwenye mitandao? Nonsense! Vita vidogo tu hivi vya maneno na propaganda vinawatoa kamasi halafu mnatuambia eti mnaweza kushindana na mafisadi, pleasee!
- Zitto rudi hapa na usimame kama mwanaume, maneno umeyasema mwenyewe sasa beba tu msalaba wako hapa, JF juu zaidi na Mungu aibarikie JF kumkoma nyani idumu milele!
Respect.
FMEs!