TANESCO imechukua hela zetu lakini haitaki kutufungia Umeme

REF:FA12051069729487 JACKILIN I NJOU umefanikiwa kulipia Bill Number 378 BILL:991032726258 TZS27000 RECEIPT:921205059122202 2021-07-24 09:09:33.

Hii nmelipia toka mwezi wa saba mwaka jana Mabwepande lakini kila nikifwatilia pale Tanesco Tegeta mara waseme nguzo hakuna siku nyingine naambiwa Mita za mabwepande hazipo alafu ukiangalia nguzo imepita upenuni kwangu kama wanataka Rushwa waseme alafu nilio watangulia naona wanafungiwa umeme
bila kujiongeza utasubiria miezi saba mingine
 
Ndio wanataka Rushwa Mkuu we jiongeze lasivyo utasubiri sana na utaishia kuona majirani ndio wana angaziwa maisha yao, maana hawa jamaa siku zote waga wanadai wana upungufu wa nguzo, sa ili upate hizo hizo nguzo chache inabidi uchangamke

Usiridhike na vimaneno vya huyu admin wa Tanesco humu jf ni mnafki tu, ye anachofanya ni kutekeleza majukumu yake nyuma ya keyboard ya kutufariji ila kiuhalisia anajua kabisa kuwa mkono mtupu haulambwi
Tafadhali onesha namba ya simu uliyoandika kwenye fomu yako kwa hatua zaidi
 
Mie nishaletewa umeme Mkuu baada ya kujiongeza, endelea kuwafariji wateja ambao wanasubiri haki itendeke, haiingii akilini mtu alielipia tangu July bado anasubiri ila alielipia November ameletewa na wanakaa mtaa mmoja alafu suluhisho liwe ni kukuandikia namba ya simu hapa jamii forum eti ndio mtu apate Msaada ilhali anaenda ofisini na hapati Msaada wowote Zaidi ya kuambiwa nguzo hakuna sa sijui hao wanaoleletewa walienda na nguzo zao Tanesco
 
Tafadhali pokea taarifa rasmi kutoka kwa Shirika lako la Umeme Nchini (TANESCO) wateja wote waliofanya malipo kabla ya mabidiliko ya bei yaliyotangazwa tarehe 5/01/2022 tutawaunganishia umeme kabla ya tarehe 30/03/2022 bila ongezeko la gharama zozote

TANESCO tunayaangaza Maisha Yako
Wacha tusubiri tuone....... Tarehe 30 sio mbali
 
Mie nishaletewa umeme Mkuu baada ya kujiongeza, endelea kuwafariji wateja ambao wanasubiri haki itendeke, haiingii akilini mtu alielipia tangu July bado anasubiri ila alielipia November ameletewa na wanakaa mtaa mmoja alafu suluhisho liwe ni kukuandikia namba ya simu hapa jamii forum eti ndio mtu apate Msaada ilhali anaenda ofisini na hapati Msaada wowote Zaidi ya kuambiwa nguzo hakuna sa sijui hao wanaoleletewa walienda na nguzo zao Tanesco
Yule Kalemani nlikua simpendi Kwa vile yupo CCM Ila alikua mtekelezaji haswa kuliko uyu wa sasa Twitter darling yaan, kwa kifupi tumepigwa. Wanataka Nguzo zao kutoka sauzi ambazo wamenunua pale iringa zije watupige
 
REF:FA12051069729487 JACKILIN I NJOU umefanikiwa kulipia Bill Number 378 BILL:991032726258 TZS27000 RECEIPT:921205059122202 2021-07-24 09:09:33.

Hii nmelipia toka mwezi wa saba mwaka jana Mabwepande lakini kila nikifwatilia pale Tanesco Tegeta mara waseme nguzo hakuna siku nyingine naambiwa Mita za mabwepande hazipo alafu ukiangalia nguzo imepita upenuni kwangu kama wanataka Rushwa waseme alafu nilio watangulia naona wanafungiwa umeme
Pole Sana aseee nakuambia apo mpk watoke hawa wapigaji ndo tutapata umeme nakuambia ulio imara, najiuliza Ile treni ya SGR kama inategemea umeme huu c ipo siku utajikuta katikati ya msitu mmekatikiwa umeme
 
Tafadhali onesha namba ya simu uliyoandika kwenye fomu yako kwa hatua zaidi
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] nyie jamaa muda mwingine mnaniachaga hoi sana[emoji12][emoji12]duh kama kweli hivi mpo serious na kazi[emoji154][emoji154]kumbe[emoji24][emoji24][emoji24]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tunashukuru kwa taarifa

Tafadhali tuoneshe taarifa kamili kwa ufatiliaji na hatua zaidi

Aliandika namba ya simu ipi kwenye maombi yake

TANESCO Huduma kwa Wateja

Makao Makuu
Kama wako seeious vile kumbe hamna lolote
 
Tanesco na TRA ni janga la taifa, dhuluma haimuachi mtu salama
 
Tupo kukuhudumia onesha taarifa kamili tafadhali
Malalamiko ni mengi nchi nzima hata mkipewa hapa taarifa hakutakua na msaada. Mtu nyumba yake imeisha ila anashindwa kuhamia kisa umeme. Umeme unaombwa utafikiri unatolewa nchi jirani
 
Mpaka sasa haujasema unalalamikia nini ili tukuhudumie
 
Bei ya kuvutiwa umeme kwa mijini bei ikoje kwa single phase?

Je, 3phase pia kwa sh ngapi?
Ndugu Mteja!

Zifuatazo ni gharama halisi za kuunganishiwa umeme kuanzia tarehe 5/02/2022

[emoji3578]Gharama za kuunganisha umeme mjini ndani ya mita 30 kwa mteja wa njia moja kutoka kwenye miundombinu ya umeme shilingi 320,960/=,

[emoji3578] Mteja wa njia moja ndani ya mita 70 kutoka kwenye miundombinu ya umeme shilingi 515,618/=,

[emoji3578]Umbali wa njia moja ndani ya mita 120 kutoka kwenye miundombinu ya umeme shilingi 696,670/=

[emoji3578]Aidha, gharama za kuunganisha umeme mjini ndani ya mita 30 kwa mteja wa njia tatu kutoka kwenye miundombinu ya umeme shilingi 912,014/=,

[emoji3578] Mteja wa njia tatu ndani ya mita 70 kutoka kwenye miundombinu ya umeme shilingi 1,249,385/=,

[emoji3578]umbali wa njia tatu ndani ya mita 120 kutoka kwenye miundombinu ya umeme shilingi 1,639,156/=.

Zingatia

Gharama ya kuunganisha umeme vijijini kwa wateja wa njia moja ni shilingi 27,000/= kama ilivyoelekezwa na EWURA.

NB: Gharama zote zimejumuisha Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT).
 
Bado bei zenu zile zile, kwakweli mnatunyanyasa sana na gharama za unit ziko juu mno....ndio maana vijijini na hata mijini kuna watu wanatumia taa za sola. Kwakweli mchina tunamshukuru sana.

Atleast mngetufanyia bei zifuatazo ingeturahisishia, na hata wale wa chini wangemudu bei elekezi

Single phase 150000
3 Phase 320000
 
Tanesco semeni tu kwamba mnawafungia fasta waliotoa 320,000/= siyo kuleta longolongo......
 
Back
Top Bottom