TANESCO imechukua hela zetu lakini haitaki kutufungia Umeme

Ivi nikilipa kesho iyo laki 320 i achukua muda gani mpaka kufungiwa umeme
 
mimi niliomba mita 3 kwa ajili ya fremu 3 nilipigiwa simu na bosi wa survey ilala makao makuu samora kuwa utafungiwa moja tu kwanza nyingi baadae tangu mwezi wa 10/2021 nilifungiwa moja zingine 2 yeye survey mpaka apende hata kama miaka. sijui huwa ni sheria ya tanesco au uamuzi wake yeye. na meneja mkuu alinikubalia kupata mita 3
 
Tunashukuru kwa taarifa

Tafadhali tuoneshe taarifa kamili kwa ufatiliaji na hatua zaidi

Aliandika namba ya simu ipi kwenye maombi yake

TANESCO Huduma kwa Wateja

Makao Makuu
Wewe bwana au bibi TANESCO bora unyamaze tu hapa watu tuna vitu vizito rohoni tukitapika utanuka kweli kweli.

Tupo wengi kwenye orodha ya wanaosubiri huduma.
 
Wewe bwana au bibi TANESCO bora unyamaze tu hapa watu tuna vitu vizito rohoni tukitapika utanuka kweli kweli.

Tupo wengi kwenye orodha ya wanaosubiri huduma.
Mkuu Tanesco ni shirika la Ajabu sana, huyu Admin anatufariji tuu, mimi nimelipia toka mwenz 8 hadi leo sijafungia umeme..ila jirani zangu waliolipia mwenz wa kumi na kuendelea wanaunganishwa umeme bila shida.. nilienda ofisin majibu yao kuna uhaba wa vifaa, wanao waunganisha umeme kwa sasa ni wale ambao siyo wa kuhitaji nguzo, , kwahiyo nimeambiwa nisubir hadi pale watapo leta vifaa, aise nimekata tamaa kbsa.
 

Tutawakumbusha kuhusu ili maana ulivyojibu as if hiyo siku haitafika au ni mbali sana!!
 
Mimi pia nilipeleka fomu mwezi wa 9 mwaka Jana ,surveyor hakutokea mpaka mwezi wa 12 nilipoamua kwenda kukomaa kuchukua surveyor nikalipia mwanzoni mwa mwezi December ila mpaka leo wananipiga tarehe tu,upuuzi upuuzi tu.
 
Wakati wafanyabiashara wengine tunahangaika kutafuta wateja, Tanesco wengine anawapangia kiasi gani cha bidhaa wachukue 😳
 
Mimi kupewa tu Control number nilipie hiyo 27 elfu ilinichukua Mwaka na kidogo, Sijui kuja kufungiwa itanichukua muda gani, Nashawishika Kutoa Rushwa ili nipate tu hii huduma, Wakuu kukaa kwenye Nyumba enye bila umeme yataka Moyo. Serikali yetu kwenye hili swala la kutoa huduma kwa wanainchi wake bado sana.
 
Tunashukuru kwa taarifa

Tafadhali tuoneshe taarifa kamili kwa ufatiliaji na hatua zaidi

Aliandika namba ya simu ipi kwenye maombi yake

TANESCO Huduma kwa Wateja

Makao Makuu

We Mpumbavu , hivi wewe hukutumbuliwa apo Juzi juzi, tutolee ukenge wako huku.
 
Tunashukuru kwa taarifa

Tafadhali tuoneshe taarifa kamili kwa ufatiliaji na hatua zaidi

Aliandika namba ya simu ipi kwenye maombi yake

TANESCO Huduma kwa Wateja

Makao Makuu
Asante kwa kuja hapa kutoa ufafanuzi. Huu ni uungwana.

Toka mwezi Desemba mwanzoni mwaka jana nilifanyiwa survey kwa ajili ya kuunganishiwa nishati ya umeme na tayari nguzi na nyaya zimeshaunganishwa mita kumi kutoka katika kibanda changu.

Nimejaza form na kuiwasilia ofis zenu hap Morogoro. Toka muda huo mpaka sasa nahangaika kupata control number nilipie lakini katika dawati la huduma ofisini hapo hawatoi majibu ya kuridhisha ni kwa nini sipati huduma hiyo mpaka Mh. Rais alipo tangaza mabadiliko ya bei ya kuunganishiwa umeme na bado sijapata control number.

Nini ni shida hapa TANESCO Morogoro?
Je nitalipa gharama ipi?...hii mpya au ile ya zamani ambayo nilishaanza mchakato wa kulipia na form zangu zikapokelewa kabla ya tangazo la mabadiliko hayo?

TANESCO
 
Lile kundi la wapigaji wa Nguzo kutoka sauzi Africa ndo limeingia kwenye system, kumbe Nguzo zimetoka iringa Tu hapo zinapigwa mihuri ya imported na naskia Wana kiwanda Chao cha Nguzo za siment kule bagamoyo wanatengeneza taharuki makusudi ya kukosa kufungiwa ili ule mradi wao pia WA Nguzo za siment upite
 
Mkuu tusaidiane kupata namba ya waziri Makamba umu tumtumie hizi changamoto hata kama sio mtekelezaji labda atasikia. Au hata ya mama samiah mwenye nayo plz iweke jukwaani apa tumwambie
 
Tafadhali onesha namba ya simu uliyoandika kwenye maombi yako kwa hatua zaidi
 
Vitambulisho vya NIDA tu kuvipata nitatizo,miaka nenda rudi,Tanesco shida.Uchumi wa kati tupo
 
Hii kitu hata mimi inanishangaza sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…