TANESCO inaweza ikatengeneza faida kubwa sana endapo wataanza kukopesha units za LUKU. Hii ni ngumu kwa mteja kukwepa marejesho

Sasa mkuu ukikopa huo umeme kisha unaondoka kwani utaondoka nao kwenda kuutumia huko ulikohamia au inakuwaje?

Hebu tuelimishane please.
 
Sasa mkuu ukikopa huo umeme kisha unaondoka kwani utaondoka nao kwenda kuutumia huko ulikohamia au inakuwaje?

Hebu tuelimishane please.
Hahahahahaaa alafu umeme wenyewe ni wa 3,000/= tu ndio unataka kumfanya mpaka ahame kila nyumba mtaa mzima leo kapanga hapa kesho pale kisa 3,000/= tu
 
Ni hivi nimepanga nyumba. Nimelipa kodi ya miezi 4. imebaki wiki 1 kodi iishe na mm sina mpango wa kuendelea kukaa. Nakopa umeme wa 20,000 au 50,000 natumia. Muda unaisha naondoka.
Au kwa kukomoa tu kwasbb hatukua na maelewano mazuri. Siku naondoka nakopa umeme wa 20, 000 au 40,000 naondoka. Hilo deni unafikiri nani atalipa?
Muwe mnasoma kwanza post na mnaelewa kabla ya ku-comment
Sasa mkuu ukikopa huo umeme kisha unaondoka kwani utaondoka nao kwenda kuutumia huko ulikohamia au inakuwaje?

Hebu tuelimishane please.
 
Kama Tanesco inataka kufa basi waanze kukopesha umeme. Hiyo shilingi 3,000 unayoidharau chukulia watu 10,000 wamekopa umeme na hawajalipa. Unafikiri wamepoteza kiasi gani cha fedha? Fedha ambayo utaipata kwa siku moja, uipate kwa siku 10 si utopolo tena kwa faida ndogo.
Siyo kila ushauri unafaa. Km mm mtanzania ambaye naipenda TANESCO wasijekujaribu kukopesha umeme sababu madeni hufilisi. Kama wanataka kufa kifo cha mende basi wajaribu kukopesha umeme.
Km wanataka kupata pesa waboreshe huduma zao na kisha wapandishe bei ya umeme.
Wakaulize TALA, BRANCH na mitandao ya simu wamepoteza kiasi gani kwenye kukopesha.
Hahahahahaaa alafu umeme wenyewe ni wa 3,000/= tu ndio unataka kumfanya mpaka ahame kila nyumba mtaa mzima leo kapanga hapa kesho pale kisa 3,000/= tu
 
Chukulia watu 10,000 wanunue umeme 3, 000 ni sawa na shilingi 30,000,000. Hii pesa utaipata kwa siku 1.
Chukulia watu hao hao wakope umeme wa kiasi hicho hicho kwa riba halafu wakae wiki au wiki 2 ndiyo walipe umeme. Unajua mpaka hapo umepoteza kiasi gani cha fedha na muda? Madeni hufilisi, ingekuwa hivyo watu au mashirika yanayokopesha wangepata faida kubwa na yangetajirika.
Kama TANESCO inataka kufa, basi wakopeshe umeme.
Hahahahahaaa alafu umeme wenyewe ni wa 3,000/= tu ndio unataka kumfanya mpaka ahame kila nyumba mtaa mzima leo kapanga hapa kesho pale kisa 3,000/= tu
 
Madeni hufilisi, ingekuwa hivyo watu au mashirika yanayokopesha wangepata faida kubwa na yangetajirika.
Hivi unajua kuwa 90% ya faida inayotengenezwa na banks ni kupitia mikopo? Mbona hazifilisiki? Kinachoifanya TANESCO kukosa ubunifu ni hiyo monopolistic mindset waliyonayo kwa maana wanajuana hawana mpinzani tofauti na mitandao ya simu inayofanya biashara za ushindani hivyo huumiza kichwa kila wakati ili kuona watapata vp faida...
 
Kwanini unaangalia upande wa shirika peke yake? Umeangalia upande wa faida kwa mteja? Hivi unajua kama mkopo ni sehemu ya CUSTOMER CARING? Mteja anapokopa wakati wa dharura husaidia kujenga uhusiano mwema na imani yake kwa shirika. Think twice.
 
Bahati mbaya hukumsoma vizuri mtoa mada mkuu!.

Ameoanisha ununuzi wa umeme usiozidi shs 4000 sasa hiyo yako ya 20kl imetoka wapi?.

 
Kama Tanesco inataka kufa basi waanze kukopesha umeme. Hiyo shilingi 3,000 unayoidharau chukulia watu 10,000 wamekopa umeme na hawajalipa.
Kwanini unawaza negativity? Kwanini unawaza wasipolipa? Mbona haujasema vp endapo watalipa?...
 
Wakaulize TALA, BRANCH na mitandao ya simu wamepoteza kiasi gani kwenye kukopesha.
Acha kufananisha TANESCO na mitandao ya simu pamoja na hao TALA. Mkuu, itoshe tu kusema hauna hoja yoyote yenye mashiko na inawezekana wewe ni boss huko TANESCO.
 
Ni hivi nimepanga nyumba. Nimelipa kodi ya miezi 4. imebaki wiki 1 kodi iishe na mm sina mpango wa kuendelea kukaa. Nakopa umeme wa 20,000 au 50,000 natumia.
Kuna kampuni gani ya mitandao ya simu inakupa mkopo wa 50,000? Kumbuka units za kukopa ni wakati wa dharura tu hivyo units za 3,000/= zinatosha saaaana.
 
Nakuona tu unavyojitungia figures mara 20,000 mara tena 50,000. Mkuu, ukipenda andika hata 900,000/= ili hoja yako iwe na mashiko zaidi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…