TANESCO inaweza ikatengeneza faida kubwa sana endapo wataanza kukopesha units za LUKU. Hii ni ngumu kwa mteja kukwepa marejesho

TANESCO inaweza ikatengeneza faida kubwa sana endapo wataanza kukopesha units za LUKU. Hii ni ngumu kwa mteja kukwepa marejesho

Infantry Soldier

JF-Expert Member
Joined
Feb 18, 2012
Posts
15,892
Reaction score
16,476
Habari za wakati huu kaka na dada zangu wa humu JamiiForums.

Kwanini TANESCO haikopeshi units za umeme wa LUKU kwa wateja wake? Mimi ninaona kama mchakato huu utawawezesha kupata faida kubwa sana kama riba kwa maana ni ngumu sana kwa mteja kukwepa marejesho.

Tofauti ya mteja wa TANESCO na mteja wa mtandao wa simu za mikononi kama Vodacom na Tigo ni kwamba, mteja wa mitandao hii ana nafasi kubwa sana ya kutokulipa deni kwa maana anaweza kubadili simcard au anaweza kufa kisha deni likawa limepotea tofauti na mteja wa TANESCO ambaye deni linakuwa limebebwa na nyumba kiasi kwamba hata akifa, deni litakatwa wakati wa ku-transfer property ownership.

Mteja wa mitandao ya simu za mikononi anaweza akakopa Vodacom kisha akahama mtandao akaanza kutumia Tigo, lakini mteja wa TANESCO hawezi kubadili number yake ya mita ya LUKU. Kama alikopa umeme wa 5,000/= kwa kutumia M-PESA inakuwa ngumu sana kukopa tena kwa kutumia mtandao mwingine kama vile TIGO PESA kwa maana atatumia number ile ile ya mita hivyo computer system itakataa kufanya muamala wa kumpa units.

TANESCO wanaweza kufanya special arrangement na kampuni husika ya mtandao wa simu kama Vodacom au Tigo kutoka mkopo wa pesa mahususi kwa kununua units za umeme tu na sio muamala mwingine wowote. Ukitumia pesa hiyo kwa muamala mwingine inakataa.

Mathalana TANESCO wanaweza kukukopesha umeme wa 4,000. Halafu utakatwa labda 25% kila utakaponunua tena mpaka deni liishe. Au ukiamua unalipa 100%.

Wataalam wa masuala ya uchumi pamoja na ICT mnaweza kulifafanua hili zaidi kwa maana hiyo sio taaluma yangu lakini ninapendekeza number itakayoruhusiwa kukopa iwe moja tu (Mmiliki wa nyumba) hususan kwa nyumba zenye wakazi (wapangaji) wengi

NB: Ndugu zangu waislam, Mungu awatangulie na kuwasimamia katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhani. Siku zote 30 za mfungo zikawe za kheri na baraka kwenu. Wishing you courage and strength so that you win every challenge of this life.

USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
 
Wazo zuri sana. Tanesco wanasema wao n non profit organisation.

Sent from my SM-A260F using JamiiForums mobile app
Bila kupata faida wanawezaje kuwalipa wafanyakazi wake pamoja na gharama zingine za uendeshaji? Wanapata ruzuku ya serikali? Watapewa mpaka lini? TANESCO hawatoi gawio wa serikali kuu?
 
Bila kupata faida wanawezaje kuwalipa wafanyakazi wake pamoja na gharama zingine za uendeshaji? Wanapata ruzuku ya serikali? Watapewa mpaka lini? TANESCO hawatoi gawio wa serikali kuu?
Kuna meneja mmoja wa tanesco nilikua naongea nae akaniambia shirika linaenda kufa...coz cost of production n kubwa kuliko mapato.
 
Kwann mnapenda sana mkopo? Hii system ya TANESCO kutokopesha ni nzuri. Kuna nyumba za kupanga au fremu za biashara.
Mtu anakopa umeme wa laki moja ukiisha anahama. Mzigo unamwangukia mwingine
Naona waweke tu mfumo,ukinunua umeme kwa mfano wa 5000 unajijaza wenyewe. Hakuna kwenda kujaza kwenye mita
Unawezaje kukwepa deni la 20,000/= la LUKU?
 
Hii system ya TANESCO kutokopesha ni nzuri. Kuna nyumba za kupanga au fremu za biashara.
Mtu anakopa umeme wa laki moja ukiisha anahama.
Ni wapi nimezungumzia mkopo wa laki moja? Vodacom wanatoa mkopo wa laki moja kwa mara moja? Ndio maana nimesema anayeweze kuruhisiwa kukopa ni mtu mmoja tu.
 
Back
Top Bottom