Hivi karibuni Watanzania kupitia mitandao mbalimbali walionesha ghadhabu juu ya ongezeko la kodi kwenye LUKU kutoka Tsh 1500 mpaka 2000 pasipo kutoa notice kwa umma. Baadae TANESCO walitoa maelezo kwamba ongezeko hilo ni deni la nyuma kwa baadhi ya wateja, cha kushangaza mambo yamekuwa tofauti ni kama tozo zimehararishwa kuendelea maana makato yamebaki kuwa 2000 kwa kila anayenunua umeme.
Kitendo hiki si chakiungwana maana inaonesha serikali inaibia raia wake pasipo woga wowote......kitendo hiki kinakera, kuumiza na kutia hasira kuona serikali ya CCM inavyopuuza wananchi wake kwa kufanya mambo pasipokufuata taratibu za kisheria. Kibaya zaidi hawatoi takwimu ya hizo pesa lakini pia zimesaidia kutatua changamoto zipi za umma.
Kitu kinachoumiza ni serikali kuendelea kuwa na matumizi makubwa na yasiyokuwa na tija kwa nchi. Mfano ziara ya Rais inakuwa na msafara wa magari zaidi ya 150 kwa wakati mmoja (Rais, Mawaziri na Naibu Mawaziri karibu wote)......Huu ni upumbavu uliopitiliza ambao matokeo pesa nyingi zinapotea kwenye mambo yasiosaidia jamii na hivyo nchi kuishia kukopa mara kwa mara huku deni la taifa likizidi kuongezeka na maisha ya Watanzania kuendelea kuwa duni..........Uchaguzi ujao inabidi tujipange sana kutokomeza huu uhuni na ufisadi tunaoushuhudia.