KERO TANESCO Masasi mnakata sana umeme, tutafanya uzalishaji wa maendeleo kweli?

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
TANESCO wametuunga na wengine tumejoin wenyewe katika magroup yao ya TANESCO huku Masasi Mkoani Mtwara, tukilalamika humo hakuna kusaidika, hapa tu wametoka kukata umeme, wanakata sana, hivi kweli kuna uzalishaji hapa wa kueleweka?

Vitu vinaungua mara kwa mara kutokana na mtundo wao wa kukata umeme mara kwa mara.

Hii sio mara ya kwanza kulalamika hapa JF, yaani haiwezi isha siku moja bila kukatiwa umeme hapa Wilaya ya Masasi, kila siku wana matengenezo, hawajali kama ni siku za kazi au siku za kiuzalishaji zinaendelea.
 
Nimekuja juzi kijjn wilayani Masasi .kabla sijafika Mama yangu alinipa tahadhari ninunue tochi na power bank huku umeme unazingua sana,na kweli tangu nimefika nimejionea hiyo katakata umeme
 
Umeme ni tatizo sugu,miradi ya watu iliyoeekwa mfukoni!

Usipotafuta mbadala wa nishati hii utateseka sana!

Binafsi nilikua nawapigia sana hai tanesco nilikuja gundua nitakosana na watu na kuonekana mwanaharakati,hata nguzo zao zipo hapa naziangalia TU hata hamu nazo sina!

Tanesco ni sikio la kufa coz umeme umefanywa biashara badala ya huduma ya kudumu!

LABDA MIMI MWENYEWE NIKIPENYA NAWEZA BADILI HALI,NI SERIOUSNESS TU HAMNA!
 
Sio NTWARA tu.Dar kwenyewe ni changamoto.
 
Habari ndugu mteja.

Asante kwa kuwasiliana nasi, na pole kwa changamoto hiyo. Tafadhali tupatie namba yako ya simu pamoja na taarifa kamili za eneo unalopatikana, ikiwemo Kata, Mtaa/Kijiji ili tuweze kukupatia msaada zaidi.^RS
 
Umeme ni tatizo sugu,miradi ya watu iliyoeekwa mfukoni!

Usipotafuta mbadala wa nishati hii utateseka sana!

Binafsi nilikua nawapigia sana hai tanesco nilikuja gundua nitakosana na watu na kuonekana mwanaharakati,hata nguzo zao zipo hapa naziangalia TU hata hamu nazo sina!

Tanesco ni sikio la kufa coz umeme umefanywa biashara badala ya huduma ya kudumu!
LABDA MIMI MWENYEWE NIKIPENYA NAWEZA BADILI HALI,NI SERIOUSNESS TU HAMNA!
Habari ndugu mteja, asante kwa kuwasilisha ujumbe wako kwetu.

Tafadhali tutumie mawasiliano yako ili tuweze kupata ufafanuzi zaidi kuhusu changamoto ya huduma unayokutana nayo na kukufanyia ufuatiliaji. Aidha, unaweza kutupatia maelezo ya ziada yatakayotusaidia kulielewa suala hilo na kutafuta suluhisho.

Asante kwa kuwasiliana nasi.^RS
 
Habari wateja wetu,

Licha ya kuwa tumewaomba mtupatie mawasiliano yenu, tafadhali tambueni kuwa tunaendelea kufuatilia suala hili kwa karibu. Tutawasiliana nanyi na kuwapatia majibu stahiki mara tu tutakapopata taarifa zaidi.

Mawasiliano yenu ni muhimu, kwani wataalamu wetu wanaweza kuhitaji taarifa za ziada kuhusu changamoto hiyo katika maeneo yenu ili kurahisisha ufuatiliaji na utatuzi wake.

Tunaomba uvumilivu wenu wakati tunaendelea na ufuatiliaji.

Asante.^RS
 
kuna Tanseco mkuranga,umeme unakatika kuliko viuno vya yondo-syster.Wangeweka betting umeme kuwaka bila kukatika /hautakatika.Ningekuwa tajiri mkeka lazima upige tick
 
Habari ndugu mteja,

Asante kwa kuwasiliana nasi na pole kwa changamoto hiyo. Tafadhali tufahamishe Kata, Mtaa/Kijiji, eneo maarufu karibu na wewe pamoja na namba ya simu ili tuweze kukupatia msaada zaidi.^FL
 
Nimekuja juzi kijjn wilayani Masasi .kabla sijafika Mama yangu alinipa tahadhari ninunue tochi na power bank huku umeme unazingua sana,na kweli tangu nimefika nimejionea hiyo katakata umeme
Habari ndugu mteja,
asante kwa kuwasiliana na TANESCO huduma kwa wateja na pole kwa changamoto hiyo, tafadhali tufahamishe Kata, Mtaa, karibu na kitu gani maarufu na namba ya simu kwa msaada zaidi.^HN
 
Back
Top Bottom