A
Habari ndugu mteja.TANESCO wametuunga na wengine tumejoin wenyewe katika magroup yao ya TANESCO huku Masasi Mkoani Mtwara, tukilalamika humo hakuna kusaidika, hapa tu wametoka kukata umeme, wanakata sana, hivi kweli kuna uzalishaji hapa wa kueleweka?
Vitu vinaungua mara kwa mara kutokana na mtundo wao wa kukata umeme mara kwa mara.
Hii sio mara ya kwanza kulalamika hapa JF, yaani haiwezi isha siku moja bila kukatiwa umeme hapa Wilaya ya Masasi, kila siku wana matengenezo, hawajali kama ni siku za kazi au siku za kiuzalishaji zinaendelea.
Habari ndugu mteja, asante kwa kuwasilisha ujumbe wako kwetu.Umeme ni tatizo sugu,miradi ya watu iliyoeekwa mfukoni!
Usipotafuta mbadala wa nishati hii utateseka sana!
Binafsi nilikua nawapigia sana hai tanesco nilikuja gundua nitakosana na watu na kuonekana mwanaharakati,hata nguzo zao zipo hapa naziangalia TU hata hamu nazo sina!
Tanesco ni sikio la kufa coz umeme umefanywa biashara badala ya huduma ya kudumu!
LABDA MIMI MWENYEWE NIKIPENYA NAWEZA BADILI HALI,NI SERIOUSNESS TU HAMNA!
Habari ndugu mteja,kuna Tanseco mkuranga,umeme unakatika kuliko viuno vya yondo-syster.Wangeweka betting umeme kuwaka bila kukatika /hautakatika.Ningekuwa tajiri mkeka lazima upige tick
Habari ndugu mteja,Nimekuja juzi kijjn wilayani Masasi .kabla sijafika Mama yangu alinipa tahadhari ninunue tochi na power bank huku umeme unazingua sana,na kweli tangu nimefika nimejionea hiyo katakata umeme