Kangosha
Member
- Sep 18, 2023
- 52
- 135
Kwa kipindi cha mwezi wote wa Kwanza hadi leo kuanza mwezi wa pili kumekuwa na kukatika umeme mara kwa mara katika maeneo ya mji mwema na maeneo mengine ya Mtwara.
TANESCO mnaturudisha sana nyuma sisi ambao ni wajasiriamali tunaotegemea Umeme kujipatia riziki. Kwa siku umeme unaweza kukatika hadi mara 6.
Kuna fundi mmoja wa TANESCO nilimuuliza kwa nini umeme unakatika sana,akasema ni sababu ya mvua na upepo. Kweli jibu lake lilinishangaza maana kwa dunia ya leo sikutegemea kuwa mvua ikinyesha iwe sababu ya umeme kukatika. Hii ni kumaanisha kuwa kipindi cha mvua shughuli za kiuchumi zinazohitaji umeme zisimamishwe!!!.
Niiombe Serikali yangu pendwa inayoongozwa na Dk.Samia itusaidie kupata suluhisho la kukatika umeme mara kwa mara maeneo ya Mtwara.
Tunashukuru kwamba umeme umesambazwa maeneo mengi.Ila tatizo limekuwa kwamba umeme sio wa uhakika.