TANESCO: Mikoa 11 kukosa umeme kwa masaa 12 tarehe 15 Novemba 2021

TANESCO: Mikoa 11 kukosa umeme kwa masaa 12 tarehe 15 Novemba 2021

Cannabis

JF-Expert Member
Joined
Jan 20, 2014
Posts
11,557
Reaction score
33,535
kpl.jpg
Mikoa 11 ya Tanzania itakosa umeme kwa saa 12 Novemba 15 mwaka huu kutokana na matengenezo yanayofanywa na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) katika njia ya kusafirisha umeme wa kilovolti 220 kutoka Kidatu hadi Iringa.

Umeme utakatika kuanzia saa 12 alfajiri hadi saa 12 jioni ili kupisha matengenezo yanayolenga kuboresha hali ya upatikanaji wa umeme katika gridi ya Taifa.

Kutokana na matengenezo hayo kutakuwa na upungufu wa umeme kwa baadhi ya maeneo ya mikoa ya Mbeya, Njombe, Ruvuma, Singida, Shinyanga, Mwanza, Mara, Tabora, Arusha Kilimanjaro na Tanga.

TANESCO imewaomba radhi wateja wake kwa usumbufu utakaojitokeza.


===
MATENGENEZO NJIA YA USAFIRISHAJI UMEME KIDATU-IRINGA

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linawafahamisha wateja wake kuwa, Jumatatu Novemba 15, 2021 kutakuwa na matengenezo ya njia ya kusafirisha umeme wa kilovolti 220 kutoka Kidatu hadi Iringa kuanzia saa 12:00 asubuhi hadi saa 12:00 jioni.

SABABU: Kuboresha hali ya upatikanaji wa umeme katika gridi ya Taifa. Kutokana na matengenezo hayo kutakuwa na upungufu wa umeme kwa baadhi ya maeneo ya mikoa ya Mbeya, Njombe, Ruvuma, Singida, Shinyanga, Mwanza, Mara, Tabora, Arusha, Kilimanjaro na Tanga. Tunawaomba radhi watejawetu kwa usumbufu utakaojitokeza.

Tafadhali usishike wala kukanyaga waya uliokatika, toa taarifa dawati la dharura la wilaya kwa msaada zaidi au Kituo cha Miito ya Simu Makao Makuu:+255 222 194 400 na +255 768 985 100

Source:

 
Maji shida, hata umeme nao inakuwa shida wakati taarifa ya msemaji wa serikali kwa vyombo vya habari imekiri kuwa Tanzania inazalisha umeme na kuwa na ziada.
 
Ni vyema TANESCO mkatangaza au kuweka wazi kua kuna mgao wa umeme ili wale wanaotegemea umeme kufanya shughuli zao za kujiingizia kipato wapange ratiba za kufanya kazi hata kama ni usiku

Mmetangaza kua kesho ijumatatu kutakua na katizo la umeme kwa masaa 12, cha ajabu hilo katizo la umeme kwa masaa 12 limeanza Jana na leo pia mmesha kata toka saa 2 asubui na hatujui utarudi saa ngapi, Sisi tunaotegemea umeme kujiingizia kipato toka jana hatufanyi kazi na hatujaingiza chochote.

Kuna baadhi ya mambo atakumbukwa JPM Japo kuna Mambo aliharibu pia, Mama yetu yupo bize hasikilizi tena vilio vya wananchi, vilio vikizidi anapewa ka memo anajitokeza anakazia pale pale na kuungana na watendaji kazi wake bila kusikiliza malalamiko ya wananchi.

Screenshot_20211114-112155.jpg
 
Tuna huyu Waziri yeye ni show off tu za kuvaa mashati meupe ya mikono mirefu na kuyakunja hadi usawa wa viwiko kama Barack Obama, hakuna kitu.

Tunahitaji Mawaziri ambao wako down to earth na wanaleta mabadiliko hapo hapo ya upatikani wa nishati, kila kitu tunacho tatizo nini? Kuzurura zurura kwenye nchi za watu na kuomba omba haiwezi kutusaidia.
 
Hivi hawajafika wale wa "...ina maana huo ubovu umeanza baada ya JPM kufariki"?

Nchi ina viumbe wa ajabu sana hii.

Watu walijazwa ujinga hadi wakaamini matatizo nchi hii yameshamalizwa na JPM.

Cha ajabu zaidi, wakaamini matatizo yamemalizwa wakati huo huo yakiwa yanaishi ndani ya matatizo mazito zaidi kama vile ya kukosa ajira!!

Ukiuliza tatizo la umeme lilimalizwa kutokana na mradi upi mpya, hakuna anayekujibu wamejitahidi sana watakuambia zamani mafisadi walikuwa wanaziba maji ili wauze umeme!!

What a pity!
 
Back
Top Bottom