Tanesco mnatuhujumu wakazi wa Mwanza na Kanda ya ziwa Kwa ujumla

Tanesco mnatuhujumu wakazi wa Mwanza na Kanda ya ziwa Kwa ujumla

TANESCO.
MTAFUTIWE MBADALA KAMA BANDALI TU MAANA MMEZIDI KILIO NI KIKUBWA ALMOST NCHI NZIMA HUDUMA ZA KUSUA SUA HUU MFUMO KIPINDI CHA MAGUFULI HSUKUWEPO KABISA UMEME UKIKATIKA UNAPEWA SABABU NA UNALIDHIKA SIKU HIZI SIJUI MMEKUWAJE JIREKEBISHENI MNAKELA AISEE
 
Mwanza kuna kitu huwa kinaenda sawa kweli?

Umeme, maji, barabara za mitaa kasheshe kote .
 
Matengenezo yafanywe usiku!
Ni kutojali maisha ya watu kunapelekea maboresho kama kubadili nguzo, transfoma, n.k kupelekea ukosefu wa umeme siku kadhaa.
MATENGENEZO YOTE YASIYO YA DHARURA YAFANYWE USIKU!
 
TANESCO.
MTAFUTIWE MBADALA KAMA BANDALI TU MAANA MMEZIDI KILIO NI KIKUBWA ALMOST NCHI NZIMA HUDUMA ZA KUSUA SUA HUU MFUMO KIPINDI CHA MAGUFULI HSUKUWEPO KABISA UMEME UKIKATIKA UNAPEWA SABABU NA UNALIDHIKA SIKU HIZI SIJUI MMEKUWAJE JIREKEBISHENI MNAKELA AISEE
Habari Leonce jr, asante kwa kuwasiliana nasi kupitia ukurasa huu, tumepokea maoni yako na kuwasilisha idara husika kwa hatua zaidi.^MY
 
Matengenezo yafanywe usiku!
Ni kutojali maisha ya watu kunapelekea maboresho kama kubadili nguzo, transfoma, n.k kupelekea ukosefu wa umeme siku kadhaa.
MATENGENEZO YOTE YASIYO YA DHARURA YAFANYWE USIKU!
Habari Kimbori, asante kwa kuwasiliana nasi kupitia ukurasa huu,

TANESCO inatambua umuhimu wa huduma ya umeme katika shughuli za kila siku za wananchi na inaendelea kuchukua hatua kuhakikisha athari za katizo la huduma zinapungua. Tunapenda kufafanua kuwa ratiba ya matengenezo huandaliwa kwa kuzingatia aina ya kazi inayofanyika, mahitaji ya kiufundi, usalama wa wafanyakazi na wananchi, pamoja na hali ya mfumo wa umeme. Baadhi ya kazi za matengenezo zinahitaji kufanyika katika muda maalum ili kuhakikisha zinakamilika kwa usalama na ufanisi.^MY
 
Uongo
 
Hawa tanesco wamezidi kila wiki lazima waiguse mwanza na viongozi wako kimya matengenezo gani yasio isha? Washaichukulia mwanza poa sana hawa
 
Hawa tanesco wamezidi kila wiki lazima waiguse mwanza na viongozi wako kimya matengenezo gani yasio isha? Washaichukulia mwanza poa sana hawa
Habari seneni, pole sana kwa changamoto hii.

Tafadhali fahamu kuwa hayo ni matengenezo yanayotekelezwa kwa awamu kwa lengo la kuhakikisha huduma ya umeme inaendelea kupatikana wakati maboresho yakiendelea kufanyika.

Taarifa kuhusu matengenezo yaliyopangwa hutolewa kupitia njia zetu mbalimbali za mawasiliano. Ikiwa hujawa ukipokea taarifa hizo, tunakushauri ututumie kupitia Inbox namba yako ya WhatsApp pamoja na Wilaya unayoishi, ili tukusaidie kuunganishwa na kundi husika.

Kuunganishwa katika kundi hili kutakuwezesha kupata taarifa za matengenezo kwa wakati, pamoja na kutoa taarifa kuhusu katizo lisilopangwa au hitilafu ambayo haikuwemo kwenye ratiba ya matengenezo. Taarifa hizo husaidia timu zetu za dharura kufuatilia na kuchukua hatua kwa wakati.

Asante! ^FL
 
Na leo kuna maeneo mengi ya Mwanza hakuna umeme, hizi sababu mnazotoa za kukata umeme zimekuwa too much na hazina tija kwa uchumi wa watu wengi wanaotegemea umeme, mmeifanya hii huduma kama hisani, hamko tofauti na mamlaka ya maji Mwanza,
Mmeshauriwa kufanya hayo matengenezo usiku fata huo ushauri, very hopeless public entity
 
Sekta zote wanaziua makusudi i.e,ajira, ujenzi,mahoteli, biashara ndogo ndogo hatari mno. Meneja wa kanda abadilishwe
 
Na leo kuna maeneo mengi ya Mwanza hakuna umeme, hizi sababu mnazotoa za kukata umeme zimekuwa too much na hazina tija kwa uchumi wa watu wengi wanaotegemea umeme, mmeifanya hii huduma kama hisani, hamko tofauti na mamlaka ya maji Mwanza,
Mmeshauriwa kufanya hayo matengenezo usiku fata huo ushauri, very hopeless public entity
Habari, ndugu mteja. Pole sana kwa changamoto hii, na tunaomba radhi kwa usumbufu uliojitokeza.

Tunapokea ushauri na maoni, na tutayafanyia kazi. Tafadhali fahamu kuwa wakati wa utekelezaji wa matengenezo, kuna mambo mbalimbali ya kiufundi yanayozingatiwa, ambayo wakati mwingine yanaweza kusababisha ratiba kutekelezwa kama ilivyotangazwa.

Hata hivyo, baada ya kukamilika kwa maboresho haya, tunatarajia huduma ya umeme kurejea na kuendelea kutolewa kwa ubora zaidi.

Asante. ^FL
 
Nilis
Na leo kuna maeneo mengi ya Mwanza hakuna umeme, hizi sababu mnazotoa za kukata umeme zimekuwa too much na hazina tija kwa uchumi wa watu wengi wanaotegemea umeme, mmeifanya hii huduma kama hisani, hamko tofauti na mamlaka ya maji Mwanza,
Mmeshauriwa kufanya hayo matengenezo usiku fata huo ushauri, very hopeless public entity
nilishawambia wafanye usiku wanasingizia wanajali afya zao TANESCO hawana shift za usiku kwani hamuwezi kulindea na polisi wakati wa maintenance usiku
 
Nilis

nilishawambia wafanye usiku wanasingizia wanajali afya zao TANESCO hawana shift za usiku kwani hamuwezi kulindea na polisi wakati wa maintenance usiku
Habari, ndugu mteja, na sante kwa ujumbe wako.

Hua tunapokea na kufanyia kazi ushauri na maoni kutoka kwa wateja wetu. Tafadhali fahamu kuwa wakati wa utekelezaji wa matengenezo, kuna masuala mbalimbali ya kiufundi yanayozingatiwa, ambayo yanaweza kusababisha ratiba kutekelezwa kama ilivyo kwa sasa.

Tunaomba uvumilivu wako, na tuamini kuwa wataalamu wetu wanafanya kazi kwa nia njema, kwa lengo la kuhakikisha huduma ya umeme inaimarika na kuwa bora zaidi baada ya kukamilika kwa maboresho haya.

Asante. ^HN
 
Habari, ndugu wateja

Kwanza, tunaomba radhi kwa dhati kwa wateja wetu wa Mwanza kutokana na kukatika kwa huduma ya umeme kama ulivyoeleza, hususan siku za Jumapili. Hali hiyo ilitokana na matengenezo ya muhimu yaliyotakiwa kufanyika kuimarisha hali ya upatikanaji umeme kwa wateja wetu na mahitaji ya mifumo. TANESCO Mkoa wa Mwanza inaendelea kuboresha na kuimarisha miundombinu ya umeme ili kuongeza uwezo wa ubora wa upatikanaji umeme kupunguza changamoto ya kukatika umeme kwa siku zijazo.

Hivyo ukiona TANESCO imetoa taarifa ya katizo ni kwa lengo la kuboresha, kama haupati taarifa tunaomba mawasiliano yako tuweze kukuunganisha na nyezo zetu za mawasiliano ili ikitokea ratiba au matengenezo uweze kufahamishwa.

Pia, tumepokea maoni na mapendekezo yenu kuhusu changamoto ya kukatika kwa umeme siku za Jumapili. Kama kuna taarifa kuhusu matengenezo yaliyopangwa zitatolewa mapema kupitia njia zetu rasmi za mawasiliano.

Tunawashukuru sana kwa uvumilivu,

Asanteni sana! ^MY
 
Back
Top Bottom