Responded HOJA TANESCO mtuelimishe hapa namna JNHP inavyoweza kutatua changamoto ya kukatika umeme

Responded HOJA TANESCO mtuelimishe hapa namna JNHP inavyoweza kutatua changamoto ya kukatika umeme

Hoja ya Mdau inayopendekeza maboresho au mabadiliko ndani ya jamii, inayotakiwa kuangakiwa kwa mapana na Mamlaka husika

Msanii

Platinum Member
Joined
Jul 4, 2007
Posts
26,483
Reaction score
40,130
Hongereni sana TANESCO, tumeshuhudia kukamilika kwa mradi huu mkubwa na hakika mtambo umewashwa leo, mmetuambia tayari mmeunganisha na gridi ya Taifa. Nina dukuduku hapa
  1. Gridi ya Taifa ni moja, kwa nini kusiwe na gridi za Taifa ambazo zinapokea umeme huo na kutumika kama backup iwapo moja imepata mkwamo?
  2. Mnawezaje kutuhakikishia kuwa yale mambo ya kuachia tope kujaa bwawani yamekoma? Alitusanua Hayati JPM ambaye kwenye uzinduzi wa leo hamjamtaja as essential ya huu mradi mkubwa?
  3. Najua hamtashusha bei ya umeme kama mlivyotuahidi. Je faida ya JNHP kwa mlipakodi wa Tanzania ni ipi?

Naomba mnijibu maswali yangu na wengine humu kwenye hili.

====================================

UFAFANUZI WA TANESCO 👇🏼
 
Rais Magufuli alipotangaza ujenzi wa bwawa la umeme kuanza mara moja bila kujali sura ya mtu alipata upinzani mkali sana kutoka ndani ya nchi na nje ya nchi.
Nje ya nchi gazeti la economics lilikuwa linakuja na makala ndefu kuonyesha kuwa huo mradi ni white elephant na utasababisha madhara makubwa kwenye mazingira.
Ndani ya nchi mradi ulipata upinzani mkali kutoka kwa Prof Muhongo, January Makamba na Nape Nauye wakidai utasababisha mbuga ya Selous ambayo ni urithi wa dunia kufutika na kuchimba bwawa ndani ya hifadhi hiyo ni kuiharibu Selous kitu kitakachopelekea kusinyaa kwa uchumi wa mikoa ya kusini!.
Nape Nauye alisimama bungeni na kupinga mradi huo hadharani huku akipigiwa makofi mengi na wabunge wa wakati huo!!
Je leo mradi umekamilika hayo madhara waliyokuwa wanayasema yameonekana
 
Nakumbuka jinsi walivyompinga Magufuli kwa 'script' yao waliyokuwa nayo? Sasa tunawaalika TANESCO ndio wanapaswa kuja kutusanua nini tutarajie baada mradi kukamiika
 
Hongereni sana TANESCO, tumeshuhudia kukamilika kwa mradi huu mkubwa na hakika mtambo umewashwa leo, mmetuambia tayari mmeunganisha na gridi ya Taifa. Nina dukuduku hapa
  1. Gridi ya Taifa ni moja, kwa nini kusiwe na gridi za Taifa ambazo zinapokea umeme huo na kutumika kama backup iwapo moja imepata mkwamo?
  2. Mnawezaje kutuhakikishia kuwa yale mambo ya kuachia tope kujaa bwawani yamekoma? Alitusanua Hayati JPM ambaye kwenye uzinduzi wa leo hamjamtaja as essential ya huu mradi mkubwa?
  3. Najua hamtashusha bei ya umeme kama mlivyotuahidi. Je faida ya JNHP kwa mlipakodi wa Tanzania ni ipi?

Naomba mnijibu maswali yangu na wengine humu kwenye hili
Habari, ndugu mteja na asante kwa kuwasiliana nasi.

Kwenye majibu ya hoja yako jambo la kwanza ni kuelewa maana ya gridi.

Gridi ya umeme ni mtandao uliounganishwa wa vifaa na nyaya zinazofikisha umeme kutoka kwa vyanzo vyake vya uzalishaji hadi kwa walaji.

Kwenye gridi ya Umeme hapa tuna;

1. Uzalishaji; Umeme hutengenezwa kwenye vituo maalum kama mabwawa ya maji, mitambo ya gesi, au nishati ya jua.

2. Usafirishaji; Nishati husafirishwa kupitia nyaya kubwa na nguzo za umeme kama ilivyo Gridi ya Taifa nchini Tanzania.

3. Usambazaji; Umeme hupunguzwa nguvu kupitia vituo vidogo na kufikishwa kwenye nyumba, shule, na viwanda.

Hivyo tunapozunguzia gridi ni muunganiko wa vitu vyote hivyo.

Hata hivyo, nchi nyingi katika kuimarisha upatikanaji wa umeme huwa zinajenga ring circuit ambayo inawezesha kupata umeme kutokea upande wote baada ya kuondoa sehemu yenye hitilafu.

TANESCO pia imeendelea kutekeleza miradi hiyo kuunganisha nchi. Hadi sasa chalinze Dodoma imekamilika. Dodoma-Singida -Babati-Arusha iko tayari. Pia kuelekea kanda ya ziwa na magharibi mwa nchi.

Mabwawa ya umeme yanasimamiwa kikamilifu na kwa TANESCO imekuwa ikifanya kazi hiyo vizuri na tukuhakikishe kuendelea kuifanya vizuri.

Kuhusu bei ni suala la sera ambapo lazima uangalie gharama za uendeshaji. Matokeo yanayopatikana ndiyo yanaweza kutoa taswira ya kupandisha au kushusha gharama.

Hata hivyo jukumu la kupandisha au kushusha gharama lipo kwa mdhibiti wa huduma za umeme na maji (EWURA).

Hatua kubwa imipigwa kwenye kuimarisha hali ya upatikanaji wa umeme nchini.

Asante. ^CM
 
Back
Top Bottom