Hongereni sana
TANESCO, tumeshuhudia kukamilika kwa mradi huu mkubwa na hakika mtambo umewashwa leo, mmetuambia tayari mmeunganisha na gridi ya Taifa. Nina dukuduku hapa
- Gridi ya Taifa ni moja, kwa nini kusiwe na gridi za Taifa ambazo zinapokea umeme huo na kutumika kama backup iwapo moja imepata mkwamo?
- Mnawezaje kutuhakikishia kuwa yale mambo ya kuachia tope kujaa bwawani yamekoma? Alitusanua Hayati JPM ambaye kwenye uzinduzi wa leo hamjamtaja as essential ya huu mradi mkubwa?
- Najua hamtashusha bei ya umeme kama mlivyotuahidi. Je faida ya JNHP kwa mlipakodi wa Tanzania ni ipi?
Naomba mnijibu maswali yangu na wengine humu kwenye hili
Habari, ndugu mteja na asante kwa kuwasiliana nasi.
Kwenye majibu ya hoja yako jambo la kwanza ni kuelewa maana ya gridi.
Gridi ya umeme ni mtandao uliounganishwa wa vifaa na nyaya zinazofikisha umeme kutoka kwa vyanzo vyake vya uzalishaji hadi kwa walaji.
Kwenye gridi ya Umeme hapa tuna;
1. Uzalishaji; Umeme hutengenezwa kwenye vituo maalum kama mabwawa ya maji, mitambo ya gesi, au nishati ya jua.
2. Usafirishaji; Nishati husafirishwa kupitia nyaya kubwa na nguzo za umeme kama ilivyo Gridi ya Taifa nchini Tanzania.
3. Usambazaji; Umeme hupunguzwa nguvu kupitia vituo vidogo na kufikishwa kwenye nyumba, shule, na viwanda.
Hivyo tunapozunguzia gridi ni muunganiko wa vitu vyote hivyo.
Hata hivyo, nchi nyingi katika kuimarisha upatikanaji wa umeme huwa zinajenga ring circuit ambayo inawezesha kupata umeme kutokea upande wote baada ya kuondoa sehemu yenye hitilafu.
TANESCO pia imeendelea kutekeleza miradi hiyo kuunganisha nchi. Hadi sasa chalinze Dodoma imekamilika. Dodoma-Singida -Babati-Arusha iko tayari. Pia kuelekea kanda ya ziwa na magharibi mwa nchi.
Mabwawa ya umeme yanasimamiwa kikamilifu na kwa TANESCO imekuwa ikifanya kazi hiyo vizuri na tukuhakikishe kuendelea kuifanya vizuri.
Kuhusu bei ni suala la sera ambapo lazima uangalie gharama za uendeshaji. Matokeo yanayopatikana ndiyo yanaweza kutoa taswira ya kupandisha au kushusha gharama.
Hata hivyo jukumu la kupandisha au kushusha gharama lipo kwa mdhibiti wa huduma za umeme na maji (EWURA).
Hatua kubwa imipigwa kwenye kuimarisha hali ya upatikanaji wa umeme nchini.
Asante. ^CM