TANESCO nini shida, umeme sasa ni highly unpredictable, yaani kwa siku unakatika hata mara nne, tano, tutafiki kwel?

Upo maeneo gani mkuu?
 
Kama huwezi sema eneo lenye matatizo na bado unajiita wewe ni Great Thinker then twafaaa!!
Wewe ni wakala wa Tanesco au kishoka? Hii Forum ya kutoa maoni na kujadiliwa tu, kwa nini akutajie eneo wakati wewe huhusiki na Tanesco? ... Hata kama akikitajia utafanya nini?... Hapo juu nimekutajia eneo linalokatwa umeme kila siku na umeme umepungua nguvu kabisa, kwa hiyo tupe sababu ya kukatika umeme leo kuanzia saa 9 alasiri hadi saa 2 usiku ni nini?.
 
Upo maeneo gani mkuu?
Mkuu nadhani nirudie,sitasema kwa kuwa mnalindana sana na mnatoa siri za wateja.Itoshe kusema kwamba kufuatana na comments za wachangiaji wengi,tatizo ni kubwa kwa hiyo litafutieni ufumbuzi.Si vigumu kujua tatizo liko wapi kama kuna team work.
 
Utopolo tupu! Unataja Ilala nzima!! Are you serious? Kama hata eneo unalokaa unaogopa kulitaja mambo makubwa unaweza kweli kujadili??
 
Baki na tatizo lako!
 
Utopolo tupu! Unataja Ilala nzima!! Are you serious? Kama hata eneo unalokaa unaogopa kulitaja mambo makubwa unaweza kweli kujadili??
Narudia tena na naomba unipe majibu ya kuridhisha, Umeme umekatwa chanika leo kuanzia saa 9 alasiri hadi saa mbili usiku huu, naomba unipe sababu za kukatika leo tu!.
 
Narudia tena na naomba unipe majibu ya kuridhisha, Umeme umekatwa chanika leo kuanzia saa 9 alasiri hadi saa mbili usiku huu, naomba unipe sababu za kukatika leo tu!.
Matengenezo ya line kubwa na taarifa ilitolewa! Kuna matengezo yanafanyika maeneo ya Buyuni kwenye viwanja vipya!
 
Utopolo tupu! Unataja Ilala nzima!! Are you serious? Kama hata eneo unalokaa unaogopa kulitaja mambo makubwa unaweza kweli kujadili??
Mkuu kumbuka kwamba unaowasiliana nao ni wateja wenu,kwa hiyo tumia lugha rafiki.Lakini kwa nini mnakazania kujua eneo?Kufuatana na comments za watu kwenye hii mada,tatizo ni kubwa shuhulikieni.Nimesema kama kuna team work si vigumu kujua matatizo yalipo.Halafu inaelekea mmekaririshwa kuuliza swali la location.Kama mteja hajisikii salama kutoa location yake,use other alternatives.Mkuu nimesema mnalindana sana na mnapeana taarifa kwa hiyo si salama mteja kutoa taarifa zake.
 
Matengenezo ya line kubwa na taarifa ilitolewa!
Matengenezo ya line ipi kubwa, taarifa ilitolewa wapi? kupitia media gani? na kama mlitangaza mlielekeza umeme utakatwa na kurudishwa saa ngapi?
 
Mitano tena!
 
Kwa maana hiyo Tanesco watajuaje sasa shida ilipo yaani waanze kutafuta Tanzania nzima mkuu? Hebu wakati mwingine tuwe realist katika complaint zetu mkuu! Kwani kusema kwa mfano Magomeni mtaa wa Makongoro itakuwa na shida kweli??
 
Matengenezo ya line ipi kubwa, taarifa ilitolewa wapi? kupitia media gani? na kama mlitangaza mlielekeza umeme utakatwa na kurudishwa saa ngapi?
Piga simu Tanesco Kisarawe utapata majibu yote eneo lako ni Kanda ya Kisarawe mkuu!
 
Kwa hiyo majibu yako hayo yana maana gani hapa, iwapo huna majibu sahihi pita kimya tu ujifunze, unanielekeza niwapigie Tanesco Kisarawe ambako kumejaa wasanii tu kama unavyofanya wewe?
 
Kwa hiyo majibu yako hayo yana maana gani hapa, iwapo huna majibu sahihi pita kimya tu ujifunze, unanielekeza niwapigie Tanesco Kisarawe ambako kumejaa wasanii tu kama unavyofanya wewe?
Kama hutaki kuripoti basi baki hivyo hivyo mkuu! Pole!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…