Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Siku chache baada ya baadhi ya Wanachama wa JamiiForums.com kuandika maandiko ya kulalamikia Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kutokana na changamoto ya kukatika kwa umeme mara kwa mara katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Tabora ikiwemo Kata ya Tura Wilayani Uyui na maeneo mengine ya Manispaa ya Tabora, ufafanuzi umetolewa.
Maeneo mengine yaliyotajwa kuwa na changamoto hiyo ni Mjini Kati, Ipuli na Isevya hali inayosababisha changamoto katika uendeshaji wa shughuli zinazotegemea umeme.
Kusoma hoja ya Mdau, bofya hapa ~ TANESCO wamezidisha kukata umeme Kata ya Tura, Wilaya ya Uyui, Tabora
JamiiForums imezungumza na Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja wa TANESCO - Tabora, Mwanahamis Hussein ambaye anaelezea kwa ufafanuzi zaidi:
Kulikuwa na hitilafu iliyotokea katika transfoma moja kwenye Kituo cha Kupooza Umeme cha Kiloleni, hii ilisababisha transfoma iliyosalia kubeba mzigo wa umeme kwa Manispaa ya Tabora pekee, wakati Wilaya zingine zikiendelea kupata huduma kawaida.
Hali hiyo imesababisha mgao wa umeme kwa nyakati tofauti kwa Wateja wa Mjini Kati.
Taarifa ilitolewa kwenye Vyombo vya Habari, tulienda kwenye redio inayofika maeneo mengi ambayo ni CG FM. Mwanzoni kabisa wa tatizo tulizungumzia tatizo hilo, tuna magroup ya WhatsApp, taarifa hiyo ilitumwa pamoja na viambatanishi vya picha na jinsi hali inavyoendelea siku hadi siku mpaka pale tatizo lilipoisha, sasa hivi hatuna tena hilo tatizo.
Transfoma nyingine ililetwa kutoka Arusha, ilishafungwa na huduma zinaendelea kama kawaida. Hiyo changamoto hakuna tena hapa Manispaa ilikuwa ni hitilafu tu ya muda.
Kuhusiana na hii ya Uyui, kuna siku ambazo kunakuwa na planned shutdown kwa ajili ya matengenezo ya kawaida, tumekuwa tukitangaza katika Vyombo vya Habari vya huku.
Kama sio kesho (Jumanne) ama kesho kutwa (Jumatano) pia umeme utakatika, lakini tushapeleka taarifa kwenye redio tangu jana, kwenye hayo magroup tumeshaweka tangazo kwamba umeme utakatika kwa ajili ya matengenezo.
Jumanne (Novemba 5, 2024) kutakuwa na line ya Urambo na line ya Sikonge kwa matengenezo kinga, na kituo chetu cha kupokea, kupooza na kusambaza umeme cha Kiloleni na Jumatano kutakuwa na line ya Uyui na line ya Ulyankulu.
Matatizo mengineyo ni yale ya mmoja mmoja, mfano Kata ya Tura, hizo ni changamoto za maeneo ambapo inatakiwa mteja mwenyewe kutoa taarifa TANESCO na mafundi kufika na kutatua hiyo changamoto.
Ikitokea amekaa kimya siku tatu kama alivyoandika, sisi tunakuwa hatuna taarifa kwamba mteja hana huduma.
Akiandika kama hivyo tunaenda kutatua, hivyo kama mkoa, tumekuwa tukifanya vikao na wadau na kualika viongozi ambako Wateja / Wananchi wanapatikana na kuweka taratibu za kufuata endapo kuna changamoto."
Namba zetu kwa Wateja ni 0748 550000 ambayo inatumika Tanzania nzima, pia kuna ya kwetu ya hapa Tabora ambayo ni 0733735548.
Pia soma ~ Tabora Manispaa, hasa Ipuli umeme unakatwa kila siku bila mpangilio, TANESCO tuambueni kama kuna mgao tujue