Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 5,352
- 15,876
Kuhusu hoja ya Mdau aliyezungumzia Dar: Jengo la Stendi ya Mwenge linakosa umeme mara kwa mara, inasemekana lina deni ufafanuzi umetolewa kutoka upande wa TANESCO.
Asante kwa kutufahamisha kuhusu changamoto hii.
Tumepokea taarifa yako na tunaichukulia kwa uzito. Kesho (Julai 15, 2026) tutakutana na uongozi wa soko husika ili kubaini chanzo cha tatizo na kuchukua hatua stahiki.
Kwa sasa, hatujapokea taarifa za kukosekana kwa umeme katika maeneo ya Mwenge. Hata hivyo, kwa kuwa umetufikishia taarifa hii, tutaifuatilia na kuifanyia kazi kwa haraka.
Asante kwa ushirikiano wako.
Juma Msuya
Afisa Huduma kwa Wateja
TANESCO – Kinondoni Kaskazini
Pia soma ~ TANESCO: Tumefanya ukaguzi wa miundombinu katika Jengo la Mwenge Stendi na kubaini huduma ya umeme ni ya uhakika