DuaZaMama
JF-Expert Member
- Jun 2, 2025
- 1,882
- 4,153
Baada ya Padri Charles Kitima kulituhumu Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kuwa lilihusika katika jaribio la kutaka kuua maisha yake kwa kuzima umeme, shirika hilo limetoa majibu yake kama ifuatavyo:
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linaufahamisha umma kuwa kuna taarifa zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii zikihusisha Shirika na matukio ya kihalifu.
TANESCO imesikitishwa na taarifa hizo ambazo si za kweli, na hazihusiani kwa namna yoyote na majukumu ya Shirika ya uzalishaji, usafirishaji na usambazaji wa huduma ya umeme nchini.
Umma unapaswa kufahamu kwamba kukatika kwa umeme kunaweza kusababishwa na sababu mbalimbali za kiufundi, ikiwemo hitilafu za dharura kwenye miundombinu au matengenezo yaliyopangwa ili kuboresha upatikanaji wa huduma.
Mambo haya yote ni ya kitaalamu, yanaratibiwa kwa mujibu wa taratibu, na hayana uhusiano wowote na vitendo vya kihalifu.
TANESCO inatoa wito kwa wananchi kuepuka kutoa au kusambaza taarifa zisizothibitishwa zinazoweza kupotosha umma na kuathiri taswira ya Shirika.
Shirika litaendelea kutekeleza majukumu yake ya kitaalamu kwa weledi na uadilifu, na kuhakikisha huduma ya umeme inapatikana kwa uhakika kwa wateja wake kote nchini.
Pia Soma: Padri Kitima: Tanesco walishirikiana na watekaji kuzima umeme ili waniue