Responded TANESCO: Ujenzi wa Kituo cha Kupoza Umeme Imalilo (Simiyu) umechelewa kwa sababu za Kiutendaji

Responded TANESCO: Ujenzi wa Kituo cha Kupoza Umeme Imalilo (Simiyu) umechelewa kwa sababu za Kiutendaji

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
5,352
Reaction score
15,876
WhatsApp Image 2025-06-14 at 11.23.46_8db1802b.jpg

Baada ya Mwanachama wa JamiiForums.com kulalamikia ucheleweshwaji wa Mradi wa Ujenzi wa Kituo cha Kupoza Umeme cha Imalilo kupitia andiko hili ~ Miaka mitano Serikali inajenga kituo cha kupozea Umeme Simiyu. Hakuna kinachoendelea, tumedanganywa? Shirika la Umeme Tanzania limetoa ufafanuzi:

TAARIFA KWA UMMA
MAFANIKIO YA MRADI WA GRIDI IMARA
​
Jumamosi, 14 Juni 2025
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linapenda kuutarifu umma kuhusu mafanikio makubwa ya utekelezaji wa Mradi wa Gridi Imara, ambao unaendelea kutekelezwa kwa awamu katika maeneo mbalimbali nchini.

Mradi huu ulianza mwaka 2022 na unalenga kuboresha miundombinu ya umeme kwa kujenga, kuboresha na kuimarisha vituo vya Kupokea, Kupoza na Kusambaza umeme, kubadilisha nguzo za miti na kuweka nguzo za zege, pamoja na kuongeza uwezo wa usambazaji na uunganishaji wa umeme kwa wananchi.

Mradi wa Gridi Imara unagharimu takribani Shilingi Trilioni 4.5, ambapo hadi sasa Serikali imewezesha kiasi cha Shilingi Bilioni 500 kwa ajili ya utekelezaji wa awamu ya kwanza ambapo kupitia fedha hizo, TANESCO imefanikiwa, kujenga vituo 5 vya Kupoza na Kusambaza umeme, kubadilisha idadi kubwa ya nguzo na kufanikisha maboresho mengine makubwa yanayoendelea nchini kote.

Utekelezaji wa mradi huu unaendelea kwa awamu na miradi yote iliyopangwa itatekelezwa kama ilivyokusudiwa ikiwemo Mradi wa Kituo cha Kupokea, Kupoza na Kusambaza Umeme cha Ilamilo katika Mkoa wa Simiyu, ambao ni sehemu ya vituo 18 vya kupoza umeme vinavyojengwa kupitia awamu ya kwanza ya Mradi wa Gridi Imara ambapo miradi 6 imekamilika kati ya miradi 27.

Ni kweli Kituo cha Kupoza umeme kilichopo eneo la llamilo Mkoani Simiyu kimechelewa utekelezaji wake kutokana na sababu za kiutendaji. Hata hivyo, Shirika linawahakikishia wakazi wa Simiyu kwamba mkandarasi wa ujenzi alishapatikana na utekelezaji wake utaendelea ili kuimarisha hali ya upatikanaji wa umeme.

Serikali kupitia Wizara ya Nishati na TANESCO tutahakikisha tunakamilisha kwa awamu ujenzi wa miradi yote ya Gridi Imara iliyopangwa kama ilivyokusudiwa katika maeneo yote nchini.

IMETOLEWA NA;
KURUGENZI YA MAWASILIANO NA HUDUMA KWA WATEJA,
TANESCO-MAKAO MAKUU,
DODOMA.


Pia soma ~
TANESCO: Tuliona tunasumbuana na Mkandarasi wa Mradi wa Imalilo tumeamua kuuendeleza na Wataalam wa ndani
 
Hii ndio serikali ya CHURA a.k.a Dalali full upigaji wasinge sema basi ingekula kwao wakazi w Simiyu. Na BADO kuna makandokando TU hapa.
Kazi ni kipimo cha utu
 
Back
Top Bottom