Cute Wife
JF-Expert Member
- Nov 17, 2023
- 1,906
- 5,000
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limesema limelazimika kuzima mitambo mitano kwakuwa majitaji ya umeme yapo chini huku uzalishaji wa umeme ukiwa ni mwingi.
TANESCO imesema hayo wakati Afisa wa Shirika hilo akiongea mbele ya Waziri Mkuu kwenye Maonesho ya Wiki ya Nishati yaliyofanyika Viwanja Vya Bunge Jijini Dodoma.
“Mh. Waziri Mkuu kwa sasa hivi tunavyopngea tuna mitambo karibu mitano ipo nje, haifanyi kazi yoyote ni kwamba tu mahitaji yapo chini uzalishaji upo mwingi kwahiyo tumeiweka tu stand by kwa ajili ya kusubiria mahitaji yakiwa juu tunaiwasha, karibia megawats 175, umeme tunaozalisha ni mwingi mahitajii ni madogo Nchi nzima, narudia tuna mitambo mitano minne Kituo cha Kinyerezi I na mmoja Kituo cha Ubungo III, hii mitambo tumeizima kwasababu mahitaji yapo chini na uzalishaji wa umeme ni mwingi imebidi tuizime, kuhusu mgao hamna mgao kwa sasa”
PIA SOMA
- Waziri Mkuu Majaliwa: TANESCO imezalisha umeme zaidi ya mahitaji
- Biteko: TANESCO inanunua umeme wa Megawati 31 kutoka Uganda na Zambia
Millard Ayo