TANESCO: Umeme tunaozalisha ni mwingi mahitaji ni madogo nchi nzima, hakuna mgawo kwa sasa

TANESCO: Umeme tunaozalisha ni mwingi mahitaji ni madogo nchi nzima, hakuna mgawo kwa sasa

Umeme au wanaongelea UKIMWI?!
 
mje kutuzimia umeme siku nzma kwa kisingizio cha maboresho,, kumbe ndo mgao ivooo
 
TANESCO kama umeme unazalishwa mwingi ongezeni kipimo cha Unit za Luku tunaponunua basi ili kufidia machungu ya mlivyotukatia katia.
 
Sasa punguzeni Bei kama umeme ni mwingi ili kuvutia wananchi walio wengi kuunganisha umeme.
 
Ni punguani tu anayeweza kuamini hilo. Yaani uzime mitambo ya kuzalisha umeme wakati vijiji Nchi nzima having umeme halafu unajisifu umeme umetuzidi?viwanda vinatumia umeme wa bei ya juu,wananchi wanatumia umeme wa gharama kubwa kulikonchi yeyoye Africa mashariki.
 
Afisa Habari wa Tanesco amemweleza Waziri mkuu mh Majaliwa kwamba wamelazimika kuzima mitambo mitano kwa Sababu Umeme unaozalishwa ni mwingi MNO kuliko mahitaji

Source: Ayo TV

Raha ya Milele umpe e Bwana na Nuru ya Daima Umuangazie Shujaa Magufuli astarehe kwa Amani, amen!
 
Kundi la Samia, Makamba, Nape, JK na Kinana lazima wafure
 
Wafanye maamuzi magumu, ili kuokoa misitu yetu, kuharamisha shughuli za kiuchumia washushe Bei ya umeme kwa kiwango Cha chini kabisa ili kuachana na ma gesi ambayo ni ghali na hatari lakini ujasiriamali utaongezeka
 
Afisa Habari wa Tanesco amemweleza Waziri mkuu mh Majaliwa kwamba wamelazimika kuzima mitambo mitano kwa Sababu Umeme unaozalishwa ni mwingi MNO kuliko mahitaji

Source: Ayo TV

Raha ya Milele umpe e Bwana na Nuru ya Daima Umuangazie Shujaa Magufuli astarehe kwa Amani, amen!
Yaani uchawa!
 
hahahahahahahahahahahaha. Ngoja nicheke kwa kichaga. Tanzania hipi. tubusibili week 2 tu
 

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limesema limelazimika kuzima mitambo mitano kwakuwa majitaji ya umeme yapo chini huku uzalishaji wa umeme ukiwa ni mwingi...
Tanesco wamefanya uamuzi bila kufikiri, ninao uhakika kuwa licha ya majiko ya umeme yapo mengi na baadhi ya wateja wZnayo lakini hawayatumii, kisa bei ya umeme ni kubwa.
 

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limesema limelazimika kuzima mitambo mitano kwakuwa majitaji ya umeme yapo chini huku uzalishaji wa umeme ukiwa ni mwingi.

TANESCO imesema hayo wakati Afisa wa Shirika hilo akiongea mbele ya Waziri Mkuu kwenye Maonesho ya Wiki ya Nishati yaliyofanyika Viwanja Vya Bunge Jijini Dodoma.

“Mh. Waziri Mkuu kwa sasa hivi tunavyopngea tuna mitambo karibu mitano ipo nje, haifanyi kazi yoyote ni kwamba tu mahitaji yapo chini uzalishaji upo mwingi kwahiyo tumeiweka tu stand by kwa ajili ya kusubiria mahitaji yakiwa juu tunaiwasha, karibia megawats 175, umeme tunaozalisha ni mwingi mahitajii ni madogo Nchi nzima, narudia tuna mitambo mitano minne Kituo cha Kinyerezi I na mmoja Kituo cha Ubungo III, hii mitambo tumeizima kwasababu mahitaji yapo chini na uzalishaji wa umeme ni mwingi imebidi tuizime, kuhusu mgao hamna mgao kwa sasa”

Millard Ayo

View: https://twitter.com/Jambotv_/status/1783077345177289131?t=-Rb2gYKOBn8f5_7mUXI7WQ&s=19
 
Back
Top Bottom