TANESCO: Umeme tunaozalisha ni mwingi mahitaji ni madogo nchi nzima, hakuna mgawo kwa sasa

TANESCO: Umeme tunaozalisha ni mwingi mahitaji ni madogo nchi nzima, hakuna mgawo kwa sasa

Kuzalisha umeme kwa wingi hakunmaanishi kuwa kuna sehemu hazitozimwa umeme. Kwa jinsi tulivyo wajinga umeme utazimwa tu.
 

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limesema limelazimika kuzima mitambo mitano kwakuwa majitaji ya umeme yapo chini huku uzalishaji wa umeme ukiwa ni mwingi.

TANESCO imesema hayo wakati Afisa wa Shirika hilo akiongea mbele ya Waziri Mkuu kwenye Maonesho ya Wiki ya Nishati yaliyofanyika Viwanja Vya Bunge Jijini Dodoma.

“Mh. Waziri Mkuu kwa sasa hivi tunavyopngea tuna mitambo karibu mitano ipo nje, haifanyi kazi yoyote ni kwamba tu mahitaji yapo chini uzalishaji upo mwingi kwahiyo tumeiweka tu stand by kwa ajili ya kusubiria mahitaji yakiwa juu tunaiwasha, karibia megawats 175, umeme tunaozalisha ni mwingi mahitajii ni madogo Nchi nzima, narudia tuna mitambo mitano minne Kituo cha Kinyerezi I na mmoja Kituo cha Ubungo III, hii mitambo tumeizima kwasababu mahitaji yapo chini na uzalishaji wa umeme ni mwingi imebidi tuizime, kuhusu mgao hamna mgao kwa sasa”

PIA SOMA
- Waziri Mkuu Majaliwa: TANESCO imezalisha umeme zaidi ya mahitaji

- Biteko: TANESCO inanunua umeme wa Megawati 31 kutoka Uganda na Zambia

Millard Ayo
Ila bado Serikali haina ujasiri wa kuitangazia Dunia hili. Kwanza Serikali yenyewe haiiamini Tanesco Anaweza ukazindua Rasmi hapa na Dunia ikajua Tanzania mambo ni mapya Na baada ya siku Tatu Giza Hilo😂
 
Umeme ukiwa abundant nategemea nikiwasha electric light bulb zangu na jirani yangu akiwasha mashine yake inayotumia Three Phase motor wakati huo huo basi taa za nyumbani kwangu zisionyeshe ile Hali ya blink blink.
 
Dah wamekata toka jana jion hadi saiv bila bila[emoji81][emoji81][emoji81]hii nchi bhna
 
Kuna qatu hawaamini wakisomachi.

Cheza na mama wewe? Anafanya mambo yake bila kujimwambafai, kimya kimya, kama siyo yeye vile.
Qatu -watu
Wakisomachi- wakisomacho

Bibi rudi menkwa
 
huu ni mwaka 2024, kidogo tuu hapo baadaye tunaanza na nyimbo za mzee....
 
Maeneo yenye uhitaji wa umeme ni mengi tena mengi sana hivi ni busara kweli kutoa kauli kama hiyo?🤔 Gharama zenyew za kuunganishiwa umeme zipo juu vp kwa watanzania wenye uwezo wa chini wamelitizama hlo kweli🤔?
 
Back
Top Bottom