Hii nchi siku hizi raia wenye furaha ni mawaziri, wabunge, Rais, na wafanyabiashara wakubwa, raia wengine nje ya hapo tuhamie Burundi.
Nchi imejaa matatizo kila upande ajabu tunaaminishwa tuone tuna serikali, hata sielewi mambo yanavyoenda; pale tozo, huku uraiani panya rodi wanaua, ukienda polisi kuwekwa mahabusu, polisi nao wanakuua...
Ukigeuka upande mwingine kuna mgao ambao haueleweki chanzo chake, kama ni upungufu wa kina cha maji kwenye hayo mabwawa, au ni marekebisho ya kiufundi, wanajua wakisema tatizo ni marekebisho pekee wataulizwa mbona yalishafanyika juzi tu?
Basi ni vurugu tupu, wanatafuta sababu nyingine za kuunganishia, muhimu majenereta yaanze kuuzwa tena, kwangu hata yote yanasababishwa na udhaifu wa kiongozi wa serikali aliyepo madarakani, tunachezewa.