TANESCO yaingia mkataba wa kukodi software kutoka India kwa USD 30M

TAtizo la mtoa Uzi ni mshamba, mill 30 kwa software ni ya kawaida kwa kampuni kubwa kama TANESCO

Mmezoea kutumia software za uwizi unafikiri kampuni kubwa kama TANESCO nao watatumia hapana
Mkuu hizi ni USD 30,000,000 ambazo ni sawa na TZS 69,000,000,000. Hizi ukipewa wewe utakula wewe na familia yako hadi michepuko yako maisha yako yote bila kufanya kazi yeyote.
 
Watanzania naona tulisahau kabisa ajenda ya ufisadi wakati wa Magufuli, mpaka sasa kuna ufisadi umefanyika fasta fasta bila ya watu hata kushtuka.

Mkataba uliosainiwa baina ya Serikali ya Tanzania (kupitia TANESCO) na kampuni ya Tech Mahindra ya India wenye thamani ya dola milioni 30 ni wa kukodisha software ya Enterprise Resources Planning (ERP) - ambayo wahindi hawa wenyewe wanaiita Corporate Management System (CMS), kama inavyosomeka kwenye bango pichani chini.

Software ya aina hii huwa inaunganisha vitengo vyote vya taasisi katika software moja kwa ajili ya urahisi wa kuendesha taasisi. Hivyo basi kwa lugha nyingine ni kwamba Wahindi hawa watafunguliwa milango ya kuingia kila mahali ndani ya TANESCO, na hivyo kuwa na siri zote za mfumo wetu wa umeme.

Jambo kama hili ni hatari sana kwa usalama wa taifa. Hakuna njia rahisi ya kuiangusha nchi bila ya kufyatua hata kombora moja kama kuangusha mfumo wa nchi wa umeme.

Software kama hizi serikali inatakiwa iwawezeshe wataalam wa ndani kupitia Mamlaka ya Serikali Mtandao kutengeneza, kama vile mfumo wa malipo serikalini ulivyotengenezwa na wataalam wetu wa ndani kwa kuwezeshwa na serikali.

Zabuni ya kukodisha software hii ilianzaga kwenye dakika za lala salama za utawala wa Kikwete. Hivyo basi kitendo cha zabuni hii kukaa benchi kwa miaka mitano ya Magufuli kinaonesha kuwa hakuwa amekubaliana nayo. Baada ya Magufuli kufa naona wadau wa zabuni hii wameiendeleza na kuimwagia wino fasta, kama wanavyotaka kufanya kuhusu bandari ya Bagamoyo.

img-618a884f193e3.jpg
Wizi mtupu! Corporate Management System haileti Umeme.
 
Kwa hicho kiasi cha fedha kweli hiyp software isingepatika yenye kufanana na hiyo duniani? HUYU MAMA TUMEPIGWA
 
Karne hii ya sayansi na Teknolojia kweli tunanunua software ya drive taasisi dah sijui akili zetu tunaztumia kwa matumbo ,

Tuna believe contract iko secured. [emoji135][emoji135]
 
Nchi hii ukipata nafasi unachukua tu chako mapema, leo kuna hukumu nimeiona, mtu kapokea rushwa mil 75,Kahukumiwa miaka 3 jela au kulipa 2millioni........so ukipata chance chukua tu
 
Watanzania naona tulisahau kabisa ajenda ya ufisadi wakati wa Magufuli, mpaka sasa kuna ufisadi umefanyika fasta fasta bila ya watu hata kushtuka.

Mkataba uliosainiwa baina ya Serikali ya Tanzania (kupitia TANESCO) na kampuni ya Tech Mahindra ya India wenye thamani ya dola milioni 30 ni wa kukodisha software ya Enterprise Resources Planning (ERP) - ambayo wahindi hawa wenyewe wanaiita Corporate Management System (CMS), kama inavyosomeka kwenye bango pichani chini.

Software ya aina hii huwa inaunganisha vitengo vyote vya taasisi katika software moja kwa ajili ya urahisi wa kuendesha taasisi. Hivyo basi kwa lugha nyingine ni kwamba Wahindi hawa watafunguliwa milango ya kuingia kila mahali ndani ya TANESCO, na hivyo kuwa na siri zote za mfumo wetu wa umeme.

Jambo kama hili ni hatari sana kwa usalama wa taifa. Hakuna njia rahisi ya kuiangusha nchi bila ya kufyatua hata kombora moja kama kuangusha mfumo wa nchi wa umeme.

Software kama hizi serikali inatakiwa iwawezeshe wataalam wa ndani kupitia Mamlaka ya Serikali Mtandao kutengeneza, kama vile mfumo wa malipo serikalini ulivyotengenezwa na wataalam wetu wa ndani kwa kuwezeshwa na serikali.

Zabuni ya kukodisha software hii ilianzaga kwenye dakika za lala salama za utawala wa Kikwete. Hivyo basi kitendo cha zabuni hii kukaa benchi kwa miaka mitano ya Magufuli kinaonesha kuwa hakuwa amekubaliana nayo. Baada ya Magufuli kufa naona wadau wa zabuni hii wameiendeleza na kuimwagia wino fasta, kama wanavyotaka kufanya kuhusu bandari ya Bagamoyo.

img-618a884f193e3.jpg

Kukodisha software si ndiyo kununua hewa?
 
Kuweka 'ERP system' katika TANESCO siyo kitu kibaya lakini nachelea matumizi ya huu mfumo hayatazidi 33% ya uwezo wake.
Hivyo watakuwa wanalipia 'full' lakini matumizi 'only a third..'.
Zaidi ya hayo kuna ERP nyingine zenye kujulikana zaidi na 'support' unapata ulimwenguni pote hata hapa TZ kama SAP, SAP Hanna n.k.
Pia kuna 'firms' lukuki na 'madogo' kibao wa ki-TZ wanatengeneza na ku-'support' mifumo kama hiyo.
Na pia TANESCO na Wa-TZ hawahitaji 'heavy softwares' kama hizo..
Lakini siyo mbaya kumpa MD Chande 'benefit of doubt' kwani naye ana utaalam katika Mifumo ya Komputa..
 
TAtizo la mtoa Uzi ni mshamba, mill 30 kwa software ni ya kawaida kwa kampuni kubwa kama TANESCO

Mmezoea kutumia software za uwizi unafikiri kampuni kubwa kama TANESCO nao watatumia hapana
Samahani mkuu, kuna wakati ukiwa muelewa sana unaweza kupoteza ufanisi wa kufikiri vizuri.

Umesema mtoa mada ni mshamba?

Kwa miaka yote hiyo ambayo Tanesco hawakuwa na hiyo Software, wamepoteza mapato au kitu gani hasa?

Utaratibu gani umetumiwa kuingia mkataba huo, Makamba hana hata miezi 3 ofisini, hii tender imetangazwa lini?

Nchi imeingia kwenye mgao wa umeme kwa kutosa 345MW, unajua bilioni 65 inaweza kuteletea kituo cha kuzalisha umeme wa 105MW? Hiyo Software inaweza kuziba pengo la 105MW kiuchumi?
 
Back
Top Bottom