Prof Griff
JF-Expert Member
- Aug 29, 2008
- 6,772
- 5,258
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
200% deal wuuu,
Wewe weka ukweli inanunuliwa sh ngapi?Huyo mto mada ndo mpotoshaji
Hiyo ERP ina features gani special kushinda nyingine, wanatakiwa watueleze
Waongo, ukisoma specifications za ERMS ya eGA inasema wazi kuwa ni interoperable na mifumo mingine.wanasema ule wa eGA siyo integratable na mifumo mingine😀
Cha ajabu hutasikia hata bunge likihoji huu ujinga.Watanzania naona tulisahau kabisa ajenda ya ufisadi wakati wa Magufuli, mpaka sasa kuna ufisadi umefanyika fasta fasta bila ya watu hata kushtuka.
Mkataba uliosainiwa baina ya Serikali ya Tanzania (kupitia TANESCO) na kampuni ya Tech Mahindra ya India wenye thamani ya dola milioni 30 ni wa kukodisha software ya Enterprise Resources Planning (ERP) - ambayo wahindi hawa wenyewe wanaiita Corporate Management System (CMS), kama inavyosomeka kwenye bango pichani chini.
Software ya aina hii huwa inaunganisha vitengo vyote vya taasisi katika software moja kwa ajili ya urahisi wa kuendesha taasisi. Hivyo basi kwa lugha nyingine ni kwamba Wahindi hawa watafunguliwa milango ya kuingia kila mahali ndani ya TANESCO, na hivyo kuwa na siri zote za mfumo wetu wa umeme.
Jambo kama hili ni hatari sana kwa usalama wa taifa. Hakuna njia rahisi ya kuiangusha nchi bila ya kufyatua hata kombora moja kama kuangusha mfumo wa nchi wa umeme.
Software kama hizi serikali inatakiwa iwawezeshe wataalam wa ndani kupitia Mamlaka ya Serikali Mtandao kutengeneza, kama vile mfumo wa malipo serikalini ulivyotengenezwa na wataalam wetu wa ndani kwa kuwezeshwa na serikali.
Zabuni ya kukodisha software hii ilianzaga kwenye dakika za lala salama za utawala wa Kikwete. Hivyo basi kitendo cha zabuni hii kukaa benchi kwa miaka mitano ya Magufuli kinaonesha kuwa hakuwa amekubaliana nayo. Baada ya Magufuli kufa naona wadau wa zabuni hii wameiendeleza na kuimwagia wino fasta, kama wanavyotaka kufanya kuhusu bandari ya Bagamoyo.
![]()
Tena hata huko IFM, UDSM , DIT umeenda mbali, hapa hapa JF mbona tupo watu tunapiga hizo kazi...mimi kwenye hiyo 69.5 billion wanipe 0.5 tu naunda timu yangu ya ushindi tena kuna wakongwe humu humu wapo wakikubali tunaungana tunatoa hiyo ERP kama wanavyotaka na kama hawaamini waseme hata kifungu cha mkataba nikishindwa wanifunge na tukimaliza kazi tunawafanyia knowledge transfer wanakuwa na control nzima ya mfumo🐒Tuliza puru usome uelewe!
USD 30 million ni equivalent na billion 69.5 za kitanzania! Hizo pesa ni nyingi mno kuna vichwa viko UDSM,DIT,IFM ambavyo with a fraction of that amount of money wangeweza ku develop system nzuri tu kwa msaada kidogo tu wa hao wahindi!
Haiingii akilini mtu alipe zaidi ya 70 billions kwa kukodi system mara mia angekuwa amaeinunua mazima! Hapo kuna upigaji wa kutisha sana! Hio system nauhakika haina thamani zaidi ya billion 10 kwa kuikodisha tu.
Hata jamii foram ilifungwa? Magufuri alikuwa na maadui wengi kungelikuwa na ufisadi akina kigogo wasingelishindwa kuandika,acha unafiki.Sio kwamba ufisadi ulikufa wakati wa Dikteta Magufuli, tatizo hapakuwa na vyanzo vya habari kuelezea mambo ya serikali.
2025Hili tatizo linaanzia kule juu kabisa, unapokuwa na kiongozi asietaka kushughulisha akili yake kwa chochote zaidi ya kusubiri kuletewa taarifa na wasaidizi wake huyo ndie chanzo.
Wasaidizi wake wanaweza kumpelekea mawazo ya hovyo yenye malengo ya "kutupiga", na kwasababu kiongozi mwenyewe hawezi kuhoji chochote anayakubali tu mawazo hayo kutokana na namna pumba anazolishwa zitakavyokuwa zimepangiliwa.
Matokeo yake ndio haya, unaona habari ya kukodi software ya $ 30 milion, baada ya kutoka kule kwenye mradi wa LNG ambao nao naamini alipigwa sound akaukubali bila kujua chochote, wala asijue hao anaowatuma ndio wajanja wenyewe, anachofanya Rais ni sawa na kumkabidhi fisi bucha sasa tunavuna tulichopanda.
Halafu interoperability ni kitu ambacho kinaweza kuongezwa hata kama haikuwepo as long as hao ega ndio walioitengeneza... labda waseme mfumo wa ega haukuwa interoperable na matumbo yaoWaongo, ukisoma specifications za ERMS ya eGA inasema wazi kuwa ni interoperable na mifumo mingine.
Huu mkataba una harufu nzito ya Ufisadi
Hii serikali ya Samia mbona inageuka ya Kipigaji mapema namna hii kulikoni?
Sijawahi kusikia hapa nchini software imetengenezwa na kuuzwa hata kwa majirani zetu, au wewe umewahi sikia?Huo mkataba unanuka ufisadi.
Hiyo software ingeweza kuwa developed humuhumu nchini na kuleta ajira kwa watu wetu.
Kitu walichokifanya TANESCO ni kucreate ajira kwa wahindi badala ya watu wetu
Na unaweza kukuta hapo wanaogopa hiyo software mpya itawaumbua na kuziba mianya yao ya kuiba mapesa.Kuna Halmashauri niliwahi kufanya kazi Idara ya Ardhi waliibia Halmashauri huku madiwani wakimwaga sifa nyingi kwa ubunifu wa ile Idara. Walidownload Google Map wakadai wamenunua software kwa gharama ya Sh 20 milioni ili kusaidia mipango mji.
Lile dude tulilibeba mpaka Maonesho ya Nane Nane kuwaonesha wananchi jinsi Halmashauri yetu ilivyopiga hatua katika Idara ya Mipango Miji. Sidhani mpaka leo kama ile Halmashauri ilishagundua iliibiwa. Tuligundua vijana wawili tu kitoka Idara nyingine ambao tulikuwa ndo tumepata ajira.
Just imagine kama Halmashauri inaibiwa kienyeji namna hiyo hali ikoje katika mambo makubwa ambayo Watanzania wengi hawana utaalam nayo?
Tupe basi mifano ya software mbalimbali kwenye mashirika makubwa na bei zao ili tulinganishe..Yaani ndiyo walipe BILIONI 65 kwa ajili ERP software? we jinga kabisa
Sheria ya kunyonga ipoo, sasa ikiwa hata hujui sheria za nchi utamuongoza nani wewe?Natamani hii nchi niingoze Mimi nilete sheria ya kunyonga .....
Je kwenye hizo gharama kuna ukweli hapo?Kuweka 'ERP system' katika TANESCO siyo kitu kibaya lakini nachelea matumizi ya huu mfumo hayatazidi 33% ya uwezo wake.
Hivyo watakuwa wanalipia 'full' lakini matumizi 'only a third..'.
Zaidi ya hayo kuna ERP nyingine zenye kujulikana zaidi na 'support' unapata ulimwenguni pote hata hapa TZ kama SAP, SAP Hanna n.k.
Pia kuna 'firms' lukuki na 'madogo' kibao wa ki-TZ wanatengeneza na ku-'support' mifumo kama hiyo.
Na pia TANESCO na Wa-TZ hawahitaji 'heavy softwares' kama hizo..
Lakini siyo mbaya kumpa MD Chande 'benefit of doubt' kwani naye ana utaalam katika Mifumo ya Komputa..