TANESCO yaingia mkataba wa kukodi software kutoka India kwa USD 30M

Sheria ya kunyonga ipoo, sasa ikiwa hata hujui sheria za nchi utamuongoza nani wewe?
Kwa wahujumu na mafisadi au wewe ulifikiri kwa wabakaji na Nani alinyongwa lete maeleze acha kuropoka Kama upo usingizini
 
TAtizo la mtoa Uzi ni mshamba, mill 30 kwa software ni ya kawaida kwa kampuni kubwa kama TANESCO

Mmezoea kutumia software za uwizi unafikiri kampuni kubwa kama TANESCO nao watatumia hapana
Hukuelewa kwamba unakodishiwa,sio unauziwa.Unajua cha kukodishiwa kinaishiaga wapi.Labda mtoa post hajaelewa vizuri.Usd milioni 30.halafu watakuja na training programme kwa Watanesco kwa kulipwa.Sipati picha jamani nosaidieni.

Halafu tutakuwa tunawalipa mpaka lini.Sijaelewa,muda wa kukodisha ukiisha wanachukua software yao au inakuwaje.Wakati wa matumizi iki co rrupt lazima waje au tunawaajiri.Nisaidieni sielewi. Watu wa IT Kina shahidi wa Kingai wa Tigo toa tena upupu hapa.
 
Mbona mifumo kama hii saivi serikalini watu wanafanya Tena sema tu hapa Kuna interest za watu. Na hata kama serikalini wakishindwa Kuna kampuni kibao tu za humu humu ndani pia zinafanya
 
Kama ni hivyo kwanin software nyingi za watanzania ni flop sio rahisi kama unavyotaka kuaminisha watu unafikiri hawana sample za software zilizotengenezwa Tanzania
 
Tuna vijana wa kitanzania wamesomeshwa vizuri mambo ya IT, walanguzi wamerudi kazini...
Hao maekspati wetu wa IT wametengeneza software ngapi ambazo zimeuzwa kwenye mashirika au nchi nyingine?
 
Naweza nikawa nimekosea, lakin pia mtoa Uzi ameelezea jujuu sana
 
Kama ni hivyo kwanin software nyingi za watanzania ni flop sio rahisi kama unavyotaka kuaminisha watu unafikiri hawana sample za software zilizotengenezwa Tanzania
Sioengelei hizi software zinazotengenezwa na makajanja anayekuambia anatoa app kwa 30,000 au kila siku yeye ana punguzo kuna watu wakongwe wapo wamefanya mambo makubwa na hakuna longolongo na wapo wanaoamini zimetengenezwa na wazungu ila ukiambiwa historia yake ndio utaelewa. Tatizo ni watu wamevamia fani na kumekosekana regulation ya maana ya nani ni nani ndio maana wengi mnakuwa na hiyo perception. Unafikiri hakuna software zilozochukuliwa kutoka nje ambazo zimeflop pia ? ukiambiwa ndio utashangaa zaidi gharama zilizoingiwa
 
Kwanini wakodi ?? Hawawezi inunua kabisa? Bcs watakodi mpk lini?
Siku hizi software nyingi zinakodishwa badala ya kuuzwa moja kwa moja. Faida ya kukodi ni kwamba kila wakati unapate updates na latest version ya hiyo software. Ukinunua, inakubidi kila mara ununue mpya. Hii ni gharama kubwa sana. Shida ya kukodi ni kuwa inategemea na vifaa vingapi unataka kufunga/kuunganisha hiyo software. Nyingine ni kuwa ukiacha kulipa kodi basi access yako nayo inakwenda na maji. Kwa mantik hii ni kuwa hii pesa iliyotajwa ni ya kila mwaka au kila baada ya kipindi walichokubaliana.

Amandla...
 
Nenda baba nenda Magufuli lala salama!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…