TANESCO yaingia mkataba wa kukodi software kutoka India kwa USD 30M

Nimecheka sana.
 
Software kama hizi serikali inatakiwa iwawezeshe wataalam wa ndani kupitia Mamlaka ya Serikali Mtandao kutengeneza, kama vile mfumo wa malipo serikalini ulivyotengenezwa na wataalam wetu wa ndani kwa kuwezeshwa na serikali.

Kuna maprofesa wa IT pale jalalani (udsm), ukienda DIT kuna maprofesa wa komoyuta wa kutosha ukirudi SUA, UDOM wataalamu wamejazana!

Hata kama hawataki kutumia wasomi je hata hapo wizarani hawa watu hawapo mpaka tuwatumie wahindi kweli?
 
TAtizo la mtoa Uzi ni mshamba, mill 30 kwa software ni ya kawaida kwa kampuni kubwa kama TANESCO

Mmezoea kutumia software za uwizi unafikiri kampuni kubwa kama TANESCO nao watatumia hapana
Unaelewa maana ya dola milioni 30 au umekurupuka? Je hatuna watuna wataalam wa kufanya hiyo kazi mpaka tutumie wahindi?
 
Mnaolalamika tengenezeni software zenu halafu mkawauzie Tanesco kwa bei nafuu kama mnaona ni kazi nyepesi. Kwa nini mnataka kuandikia mate wakati wino upo? Changamkeni fanyeni kazi andikeni hizo software halafu mkauzie hayo mashirika ya umma.
Unaijua eGA mkuu? Kwanini utumie wahindi wakati eGA ipo?
 
Je kwenye hizo gharama kuna ukweli hapo?
Tatizo ni kuwa Tanesco huenda wamechukua mfumo kwa ukamilifu wake badala ya kuwaambia wawatengenezee mfumo ambao ni 'taylor made' kwa matumizi ya Tanesco ambao ungekuwa nafuu na Chande analijuwa hilo. lakini nahisi alikuta faili mezani ikabidi amalizie mchakato..
 
ndio hawa ambao wame project hasara ya trillion 13 hadi 2025,! job truetrue
 
R.I.P JPM, kama ni kweli Mama Nchi imemshinda JWTZ wachukue Nchi 😭😭😭😭
Unaelewa Unachojaribu Kukimaanisha?
Muombe Sana Mungu Afungue Ufahamu Wako Na Kamwe Usirudie Kuandika Kitu Kama Hiki.
 
Makamba yeye kila kitu huwa anawaza nje tu , mifumo kama gepg, plann rep , GotTHoMis imetengenezwa na wataalam wetu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…