Kuna uharaka gani wa kutengeneza huo mfumo bila kushirikisha watalaamu wa ndani ya nchi, au japo kutangaza hiyo tender?
Je, mfumo ungeleta maji au kujaza mto Ruvu au kufanya mvua inyeshe ikiwa umetengenezwa na wahindi?
Tatizo kubwa la TANESCO kwa sasa ni kutokuwepo kwa huo mfumo?
1. Nina uhakika 100% huo mfumo unatengenezwa hapa nchini Tanzania bila shida yoyote
2. Hiyo hela inayolipwa kwa wahindi ni "overwhelming"
3. Tungetumia wataalamu wetu, mfumo ungekuwa ni wetu, watalaamu au vijana wetu wangepata ajira, hela ambayo ingetumika ingekuwa ni kiasi kidogo sana ukilinganisha na hiyo waliyolipwa wahindi
4. Usimamizi, usalama/ulinzi, maboresho, na matengenezo ya mfumo, vingeendelea kuwa chini ya wataalamu wetu kwa gharama ndogo
5. Tungeendelea kukua na kujitegemea katika sekta ya software
Matumizi na functionalities za huo mfumo hazitakuwa tofauti sana logically na za huu mfumo
Need Human Resource Information/Management System (HRIS/HRMS) (
***** - HR SERVICE na mifumo mingine iliyoelezewa hapa
https://www.ega.go.tz/uploads/pressreleases/sw-1574867949-ERMS ENG.pd? Kinachotakiwa ni kuadapt tu mifumo iliyopo, kucustomize/kumodify, kuongeza modules na functionalities pale inapotakiwa. Pia Wataalamu wetu wana uwezo wa kutengeneza huo mfumo from scratch.
Huo mfumo unafanana na ipi kati ya hii
The 11 Best ERP Solutions for Government and Public Sector Workers?