Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
TAARIFA KWA UMMA
MABORESHO KATIKA KITUO CHA KUPOKEA KUPOZA NA KUSAFIRISHA
UMEME WA MSONGO WA KILOVOTI 220 CHA UBUNGO JIJINI DAR ES
SALAAM
Jumatano, 19 Februari 2025
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linawataarifu wateja wake kuwa kutakuwa na maboresho katika Kituo cha Kupokea, Kupoza na Kusambaza Umeme cha Msongo wa Kilovoti 220 cha Ubungo kilichopo jijini Dar es Salaam kuanzia siku ya Jumamosi, tarehe 22 hadi 28 Februari, 2025.
Hatua hii ni muhimu kwa Shirika katika kuboresha utoaji wa huduma kwa wateja wake kufuatia ongezeko la mahitaji ya matumizi ya umeme katika maeneo ya Zanzibar na Mikoa ya Dar es Salaam, na Pwani ambalo limepelekea Kituo hicho kuzidiwa na hivyo kulazimu kufungwa kwa Mashineumba (Transformer) mpya kubwa yenye uwezo wa MVA 300 ili kukidhi mahitaji ya umeme katika maeneo tajwa.
Wakati kazi hizo zitakapofanyika baadhi ya maeneo ya Zanzibar na Mikoa ya Dar es Salaam na Pwani yataathirika kwa kukosa umeme kwa nyakati tofauti.
Aidha, katika kipindi hicho ambacho huduma ya umeme itakosekana kwa nyakati tofauti Shirika pia litakuwa likifanya matengenezo mbalimbali ya miundombinu ya umeme kwenye maeneo tajwa ili kuiweka miundombinu yetu kwenye hali ya uimara hasa kwenye kipindi hiki tunachoelekea cha msimu wa mvua.
Shirika linaomba radhi kwa usumbufu katika kipindi chote ambacho huduma ya umeme itakosekana kwenye baadhi ya maeneo na litaendelea kutoa taarifa za maendeleo ya kazi hiyo mpaka kukamilika kwake.
Imetolewa na;
KURUGENZI YA MAWASILIANO NA UHUSIANO KWA UMMA TANESCO - MAKAO MAKUU DODOMA