TANESCO yatangaza mgao wa Umeme nchi nzima kwa siku nne

Hii nchi Watawala watafanya watakavyo kwa muda mrefu sana ujao, Watanzania asilimia kubwa wanacho taka kujua ni Usajili ndani ya Yanga na Simba unaendaje basi.

Mtaani vijiweni asilimia 100 ya stories zao ni Yanga na Simba yaani hawana hata na habari na kutaka kujua watoto wao walio maliza vyuo na hawana kazi
 
Na kwa hali hii bado wanamsema mwendazake?

Hii nchi imekuwa kama gali bovu,yaani full kwenda garage kila siku,bidhaa bei juu,umeme mgao....
Na kwa hii baridi ya hapa njombe,ngoja tu tuendelee kulala na majiko ya mkaa,ili tukufwee,wafurahii..
Usha maliza kuandama kwa Coment? Hii nchi ina Waswahili wengi sana,
 
Hiyo management mpya na waziri mpya hata sioni wanachofanya, wanajua publicity tu kama wasanii wa bongo fleva.
 
Shirika la Umeme nchini Tanzania ( Tanesco) wametangaza mgao wa umeme nchi nzima ulioanza jana Ijumaa ambapo utaenda mpaka Jumatatu ya tarehe 11.

Hayo yote yametokana na kupungua kwa uzalishaji katika mtambo wa Songas.

Source:
Azam news
Daaaaah.
 
Miaka 60 ya uhuru bado tuna umeme wa mgao. Kweli Nyerere alikurupuka kudai uhuru wakati hatukuwa tayari kujitawala.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…