pole sana kwa maumivu dada yangu ila nimekupa taarifa mapema, usije kupotea onlineAhsante kwa kuniambia mdogo wangu, najua huwa unanijali ila basii tu kichwa yako ngumu sometimes..!!
Ila serious nimeumia na hii habari..!
Hatuwezi wote kuwa na mawazo sawa.....Sichukii..nakushangaa tu. Umeamua kuingia kwa kichwa changu na kutaka nifikiri kama wewe...impossible!!
Let the time decide...everybody will reap what he/she sows!! Na muda pia utaweka wazi kila jambo, hata ya sirini na hata yenye uongo uliogezwa ukweli.
Hatuishi miaka mingi sana duniani, kwahiyo inawezekana wengine baada ya sisi au baada ya miongo kadhaa, kuamua kuupa thamani ukweli.
Safi sana!...January na Kikwete nia yao ni kuleta makampuni yao yatuuzie umeme wa dharura. Je ni bwawa gani la kufua umeme lina uhaba wa maji?
Hizo kumi ni bosheni tu! Hapo ni kutangazwa kwa hali ya hatari tu mgao hautakaa uisheNa hazitakua 10, zingekua 10 Wala wasingetangaza maana hata sasa mgao upo
Sababu mbona zimetajwa?...au hujasoma habari yote?Walimtoa Kalemani wizara ya nishati ili watimize malengo na hujuma zao kwa TANESCO na kwa waTanzania…….. yaani mgao unalazimishwa pasipo sababu za msingi!
Ww mgeni na bongo nn hiyo ndo nitoleee tutakula mgao mpaka akili zitukae sawa ww angalia vitu vilivo panda bei yaaan viko juu hatari.Tuwe wavumilivu si wameleza sababu na kwa muda wa siku 10 tu
Mbowe yuko mahakamani kwa Kesi ya ugaidi, pamoja na wenzake wanne,Shutuka wwe Mangi, inaonekana ulikuwa na chuki sana na MagufuriIli mradi maiti haziokotwi kwenye viroba na watu kubambikiwa Kesi za uhujumu uchumi inatosha!!
Huyu mwamba kiukweli nikimuona fikra zangu hazitafsiri kama hatunaye kimwili bali tunaishi nae.
Kwa tume ipi?Hakuna kitu kibaya kama kuwa na kiongozi ambaye hajapigiwa kura, hana cha kupoteza
Trillions zilizokopwa zikawekwa kwenye bomba la gesi ina maana hazijaleta nafuu yoyote ? Imekuwa ni hasara tupu?!Siwatetei. Ila mvua zilizonyesha ni ndogo sana aisee
Akisifiwa na watu wote milioni 60 hatutanyooka?Nyinyi si mnamponda Magu kwa ushabiki wenu wa kisiasa safari hii tutanyooka
Kawadanganye wanafunzi unaowafundisha shuleni humu hakuna mtoto wa kumdanganya.mwendazake aliamuru TANESCO wasithubutu kuzima umeme nchi nzima no matter what - sasa haya ndiyo madhara yake - tutulie.
Mtu anaitwa Maharage unategemea cha maana kutokana kwake! Wajumbe wa bodi wote wapiga dili mojawapo ni Gachuma wa Coca mwanza! Yaani Makamba anatuletea upuuzi kwa kweli!View attachment 2098631
tuanze kuimba wimbo wa AY "habari ndio hiyo"
Naomba tukubariane wote kama nchi hata Kama Rais hataafiki Kuwa iwapo baada ya hizo siku 10 umeme bado utakatikakatika Waziri Makamba awajibishwe kwa Kufukuzwa kazi!!! Hizi sababu ya Kuwa na mgao Kwa sababu ya matengenezo ameanza kuzitoa toka aingie kwenye hiyo Wizara!!! He seems to focus only in areas where he can sign multimillion $$$ contracts and reap his commissions!!Shirika la Umeme nchini (TANESCO), limetangaza rasmi kuanza mgao wa umeme wa siku 10 kwa nchi nzima ili kuruhusu matengenezo ya mitambo ya kufua umeme kote nchini. Mgao huo utaanza Februari Mosi hadi 10 mwaka huu.
========
TANESCO KUFANYA MABORESHO KWENYE VITUO VYAKE VYA UZALISHAJI UMEME VYA KINYEREZI I NA UBUNGO III
Katika jitihada za kuboresha upatikanaji wa umeme nchini, Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), linaendelea na maboresho kwenye vituo vyake vya uzalishaji umeme vya Kinyerezi I itakayozalisha megawati 185 na Ubungo III megawati 112.
Akizungumza na wanahabari leo Januari 28, 2022 Mkurugenzi mkuu wa Shirika hilo, Maharage Chande amesema mpaka sasa uzalishaji kutoka mitambo ya Ubungo III umefikia Megawati 60 ambazo tayari zimeunganishwa kwenye gridi ya Taifa.
Amesema kwa sasa kazi ya kupanua kituo cha Kinyerezi I inaendelea na megawati 70 za awali zitaingia kwenye mfumo wa gridi mwezi Aprili 2022 na ifikapo mwezi Agosti 2022 kazi hiyo itakuwa imekamilika na kupelekea Kituo cha Kinyerezi I ambacho sasa kinazalisha megawati 150 kuwa na uwezo wa kuzalisha megawati 335.
‘‘Mitambo hii inayoongezwa ili iweze kuzalisha umeme, inapelekea mahitaji ya gesi asilia kuongezeka ambapo inalazimu kufanya uboreshaji wa mfumo wa gesi kwenye mifumo ya TPDC (Tanzania Petroleum Development Company) na PAET (Pan African Energy Tanzania)’’ amesema Maharage.
Aliongeza kuwa zoezi la uboreshaji litafanyika kwenye visima vya gesi vilivyopo Songosongo kuanzia tarehe 01 hadi 10 Februari 2022, ambapo kukamilika kwake kutahakikisha gesi ya ziada inayohitajika inapatikana.
Hivyo utekelezaji wa maboresho hayo utapelekea mapungufu ya gesi kwenye mitambo ya kuzalishia umeme wa gesi asilia na kulazimika kuzimwa kwa baadhi ya mitambo ili kupisha zoezi hilo muhimu.
Sambamba na matengenezo hayo, hali hiyo itasababisha upungufu wa uzalishaji umeme na kuathiri baadhi ya maeneo, amesema wananchi watapata taarifa za makatizo ya umeme kama zitakavyotolewa na mikoa husika.
Maboresho hayo kwenye vituo vya vya uzalishaji umeme vya Kinyerezi I na Ubungo III yatasaidia kuimarisha hali ya upatikanaji umeme nchini na kupunguza malalamiko ya wateja ya kutokuwa na umeme wa uhakika na unaotabirika.
TANESCO