TANESCO yatangaza rasmi mgao wa umeme nchi nzima

TANESCO yatangaza rasmi mgao wa umeme nchi nzima

Sichukii..nakushangaa tu. Umeamua kuingia kwa kichwa changu na kutaka nifikiri kama wewe...impossible!!

Let the time decide...everybody will reap what he/she sows!! Na muda pia utaweka wazi kila jambo, hata ya sirini na hata yenye uongo uliogezwa ukweli.
Hatuishi miaka mingi sana duniani, kwahiyo inawezekana wengine baada ya sisi au baada ya miongo kadhaa, kuamua kuupa thamani ukweli.
Hatuwezi wote kuwa na mawazo sawa.....
 
Walimtoa Kalemani wizara ya nishati ili watimize malengo na hujuma zao kwa TANESCO na kwa waTanzania…….. yaani mgao unalazimishwa pasipo sababu za msingi!
Sababu mbona zimetajwa?...au hujasoma habari yote?
 
Ili mradi maiti haziokotwi kwenye viroba na watu kubambikiwa Kesi za uhujumu uchumi inatosha!!
Mbowe yuko mahakamani kwa Kesi ya ugaidi, pamoja na wenzake wanne,Shutuka wwe Mangi, inaonekana ulikuwa na chuki sana na Magufuri
 
Ukweli ni kwamba tuna serikali dhaifu na hovyo mno kwa sasa, kila kitu hakiendi, kila wanalogusa ni kaa la moto. Umeme tayari umeshatutoa jasho, hivi mama yenu alikuja na kasi ya chanjo imefikia wapi? mimi nilijua ilikuwa nguvu ya MBEGE tu, in facts mama na group lake ni inefficient kwa kila jambo.
 
Mlimsifia sana kiko wapi yani kweli karne ya 21 kuna kuwa na mgao kisa kurekebisha mitambo khee hii nchi dah Mungu atuone tu kwanini hatupati viongozi waa maana.
 
images (77).jpeg
 
Shirika la Umeme nchini (TANESCO), limetangaza rasmi kuanza mgao wa umeme wa siku 10 kwa nchi nzima ili kuruhusu matengenezo ya mitambo ya kufua umeme kote nchini. Mgao huo utaanza Februari Mosi hadi 10 mwaka huu.

========

TANESCO KUFANYA MABORESHO KWENYE VITUO VYAKE VYA UZALISHAJI UMEME VYA KINYEREZI I NA UBUNGO III

Katika jitihada za kuboresha upatikanaji wa umeme nchini, Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), linaendelea na maboresho kwenye vituo vyake vya uzalishaji umeme vya Kinyerezi I itakayozalisha megawati 185 na Ubungo III megawati 112.

Akizungumza na wanahabari leo Januari 28, 2022 Mkurugenzi mkuu wa Shirika hilo, Maharage Chande amesema mpaka sasa uzalishaji kutoka mitambo ya Ubungo III umefikia Megawati 60 ambazo tayari zimeunganishwa kwenye gridi ya Taifa.

Amesema kwa sasa kazi ya kupanua kituo cha Kinyerezi I inaendelea na megawati 70 za awali zitaingia kwenye mfumo wa gridi mwezi Aprili 2022 na ifikapo mwezi Agosti 2022 kazi hiyo itakuwa imekamilika na kupelekea Kituo cha Kinyerezi I ambacho sasa kinazalisha megawati 150 kuwa na uwezo wa kuzalisha megawati 335.

‘‘Mitambo hii inayoongezwa ili iweze kuzalisha umeme, inapelekea mahitaji ya gesi asilia kuongezeka ambapo inalazimu kufanya uboreshaji wa mfumo wa gesi kwenye mifumo ya TPDC (Tanzania Petroleum Development Company) na PAET (Pan African Energy Tanzania)’’ amesema Maharage.

Aliongeza kuwa zoezi la uboreshaji litafanyika kwenye visima vya gesi vilivyopo Songosongo kuanzia tarehe 01 hadi 10 Februari 2022, ambapo kukamilika kwake kutahakikisha gesi ya ziada inayohitajika inapatikana.

Hivyo utekelezaji wa maboresho hayo utapelekea mapungufu ya gesi kwenye mitambo ya kuzalishia umeme wa gesi asilia na kulazimika kuzimwa kwa baadhi ya mitambo ili kupisha zoezi hilo muhimu.

Sambamba na matengenezo hayo, hali hiyo itasababisha upungufu wa uzalishaji umeme na kuathiri baadhi ya maeneo, amesema wananchi watapata taarifa za makatizo ya umeme kama zitakavyotolewa na mikoa husika.

Maboresho hayo kwenye vituo vya vya uzalishaji umeme vya Kinyerezi I na Ubungo III yatasaidia kuimarisha hali ya upatikanaji umeme nchini na kupunguza malalamiko ya wateja ya kutokuwa na umeme wa uhakika na unaotabirika.

TANESCO
Naomba tukubariane wote kama nchi hata Kama Rais hataafiki Kuwa iwapo baada ya hizo siku 10 umeme bado utakatikakatika Waziri Makamba awajibishwe kwa Kufukuzwa kazi!!! Hizi sababu ya Kuwa na mgao Kwa sababu ya matengenezo ameanza kuzitoa toka aingie kwenye hiyo Wizara!!! He seems to focus only in areas where he can sign multimillion $$$ contracts and reap his commissions!!
 
Back
Top Bottom