TANESCO yatumia Tsh milioni 600 kufuga vyura wa Kihansi Marekani

TANESCO yatumia Tsh milioni 600 kufuga vyura wa Kihansi Marekani

Kuna uhusiano gani kati ya vyura na TANESCO?
au Vyura na Umeme?
Kwa nini wasihamishiwe mikoa mingine mpaka waende Marekani?
Nadhani hawa vyura ni special ambao wana uwezo wa kuzalisha umeme. Sasa wakiwa wengi hapo baadae hatutategemea maji, gesi wala nini kuzalisha umeme bali watatumika hawa hawa vyura.
 
Vyura washindwe kuishi kwenye makazi yao waliyokulia, waende kuishi Marekani? Litanzania lote hili, walikosa sehemu ya kuwaweka?

Hili jambo lilishajadiliwa mjengoni, ni nani anapaswa kusimamia au kuhakikisha maazimio ya bunge yanatekelezwa? Na yasipotekelezwa nini kinafanyika?

Ni UPUUZI zaidi kusema, "....hii sio sawa, hapa hapaendi sawa..." kisha mwisho unamalizia "....NAUNGA MKONO HOJA mh spika...."

No wonder, qualification ni kujua kusoma na kuandika; Professors, wanazuoni na wasomi walioko humo nao wamekuwa DIMINISHED to that level.
  • ATC hawajui wanayemdai
  • Bei ya ndege inaongezwa mara 2.15
  • Bi 88 zapigwa halmashauri
  • Tanesco na miradi isiyo na Tija, usd 30m
  • Wabadhirifu kubebembelezwa watupishe
  • Nnauye kuwa msemaji wa mitandao ya simu
  • Waziri wa fedha kuwa mmiliki wa klabu za mpira kila anapopewa uwaziri
  • Bil 400 kulipwa kama faini kwa kandarasi kisa ucheleweshaji wa malipo, hapa watu wanatumia hii loophole kulamba asali
  • Tanesco kuanza kununua umeme toka kwa IPP tena, akina Ruge wamerudi

Ukiorodhesha, server itajaa, itoshe kusema PUNDA BILA VIBOKO, HAENDI.
Hii nchi wapigaji wengi sana
 
Tulia wewe unaongoza maiti mimi ungenipa bandari tu ningekuonyesha kazi
–paul kagame akimwambia kikwete –
 
Hii nimecheka tu, lakini ipo kwa zaidi ya miaka 20, so tusilaumiane.

Pia ripoti ya CAG inahitaji context kuielewa na kupima ukweli wa mambo, nani anajua kwanini tulikubali kusaidiwa kuwahifadhi hao vyura??

Unajua sisi kama nchi tunapokea fedha kiasi gani kwenye mambo ya uhifadhi?? Unajua tukikataa kutunza hao vyura tutapoteza nini na nini?

Diplomasia ya uchumi ni pana sana, na wajinga wengi hawawezi kuielewa.
Being intelligent isn't enough but how your attitude and thoughts guide your intelligence matters the most kiufupi umeandika upupu.
 
Pamoja na maungufu yake ila haya kayakuta. Vyura walipelekwa Toka enzi za mkapa huko. Waliwahi kupigia kelele halafu likafunikwa
Umesoma report ya CAG au umeamua kumtetea anaonewa? Kwa kukusaidia anza kusoma paragraph ya pili kutoka chini, ilyoanza na kusema 'NIMEBAINI"
IMG_20230407_001027.jpg
 
Umesoma report ya CAG au umeamua kumtetea anaonewa? Kwa kukusaidia anza kusoma paragraph ya pili kutoka chini, ilyoanza na kusema 'NIMEBAINI" View attachment 2579672
Juni 2020 wakati mkataba unaongezwa waziri ni nani? Mpango. Na je nani aliongeza mkataba?? Acheni kuangalia chini. Hakuanza yeye bana. Kaingia kwenye Baraza October 2021. Acheni kumchukia mtu Mpaka mmfungie na yasiyomhusu.
 
Anaitwa January Makamba.

Kijana mwizi ,fisadi, asiye na uchungu wa Nchi.
Na hiyo 2020/2021 alikuwa January Makamba?! Na huo mkataba ambao uliongezwa June 2020 ilikuwa January Makamba?! Au umekurupuka tu kusoma heading bila kusoma content?!
 
Umesoma report ya CAG au umeamua kumtetea anaonewa? Kwa kukusaidia anza kusoma paragraph ya pili kutoka chini, ilyoanza na kusema 'NIMEBAINI" View attachment 2579672
Inaonekana na wewe mwenyewe hujasoma kilichoandikwa pamoja na kuki-post.. January kaingia wizarani mwishoni mwa 2021 wakati hicho kiwango ni cha 2020/2021 ambapo hakuwepo kabisa na 2021/2022 ambapo alihudumu msimu huo kwa miezi 6 na miezi 6 mingne ni ya Kalemani. In addition, taarifa inasema Mkataba uliongezwa June 2020, muda ambao pia hakuwepo! Sasa huoni wewe ndo unajaribu kumnasua mtu ambae alihudumu kwa miezi 18 wakati hayo yanatokea?
 
Huu mradi WA vyura umesainiwa mwaka 2020...wahusika wahojiwe...
Aliekuwa waziri mwaka 2020 Nani?
 
Hao vyura walipelekwa huko miaka mingi hata wakati wa shujaa uchwara walikuwepo huko,acheni chuki kwa Makamba.
 
Inaonekana na wewe mwenyewe hujasoma kilichoandikwa pamoja na kuki-post.. January kaingia wizarani mwishoni mwa 2021 wakati hicho kiwango ni cha 2020/2021 ambapo hakuwepo kabisa na 2021/2022 ambapo alihudumu msimu huo kwa miezi 6 na miezi 6 mingne ni ya Kalemani. In addition, taarifa inasema Mkataba uliongezwa June 2020, muda ambao pia hakuwepo! Sasa huoni wewe ndo unajaribu kumnasua mtu ambae alihudumu kwa miezi 18 wakati hayo yanatokea?
Report hii inamuhusu kalemani au makamba?
 
Back
Top Bottom