TANESCO yatumia Tsh milioni 600 kufuga vyura wa Kihansi Marekani

TANESCO yatumia Tsh milioni 600 kufuga vyura wa Kihansi Marekani

Wanasiasa wanafanya vyovyote wanavyojisikia na hatuna cha kuwafanya, tunaishia kubweka bweka mtandaoni na vijiweni lakini hatuna cha kuwafanya.
Inasikitisha sana mkuu... Sanaa!!
 
Kwani hao vyura ata wakifa wanafaida gani wanazalisha Maji ya kihansi? Huu ni ufisadi
W ao wana haki ya kuishi kama wewe. Kila kiumbe kina faida yake katika dunia hii, kama wewe huijui haina maana kwamba ndiyo ukiue.
 
Hii nimecheka tu, lakini ipo kwa zaidi ya miaka 20, so tusilaumiane.

Pia ripoti ya CAG inahitaji context kuielewa na kupima ukweli wa mambo, nani anajua kwanini tulikubali kusaidiwa kuwahifadhi hao vyura??

Unajua sisi kama nchi tunapokea fedha kiasi gani kwenye mambo ya uhifadhi?? Unajua tukikataa kutunza hao vyura tutapoteza nini na nini?

Diplomasia ya uchumi ni pana sana, na wajinga wengi hawawezi kuielewa.
Yaani hapa wanamchukulia chura kama chura hata hawaelewi maudhui yake katika uhifadhi wa bioanuwai kwenye milima ya Udzungwa.

Elimu inahitajika.
 
Kwani hao vyura ata wakifa wanafaida gani wanazalisha Maji ya kihansi? Huu ni ufisadi
Hao vyura walienda marekani kitambo..Kuna kipindi nilisikia wamekufa wote,kumbe wapo...ni vyura wanaobeba mimba badala ya kutaga mayai
 
Umesoma report ya CAG au umeamua kumtetea anaonewa? Kwa kukusaidia anza kusoma paragraph ya pili kutoka chini, ilyoanza na kusema 'NIMEBAINI"
hiyo kuwa hakuna mpango wowote wa kurudisha vyura hao, nakushauri utembelee captive breeding facility iliyopo UDSM. Ilijengwa kwa ajili ya kuhifadhi na kuzalisha vyura hao ambao walikuwa wanapokelewa kwa awamu kutoka Marekani.
 
Report hii inamuhusu kalemani au makamba?
Ripoti inaihusu taasisi iliyo chini ya Wizara ya Nishati; wizara ambayo wakati mmoja ilikuwa chini ya Kalemani na wakati mwingine ikawa chini ya Makamba! Na kwa mujibu wa ripoti uliyoiweka wewe mwenyewe, ripoti hiyo inataja miaka ya kifedha ya 2020/2021 ambayo Waziri alikuwa Kalemani, na 2021/22 ambao Waziri alianza kuwa Kalemani na baadae Makamba. Hata hivyo, Ripoti ya 2021/2022 inahusisha takwimu za kabla ya April 2021 na hivyo kipindi husika waziri alikuwa Kalemani. Sio hivyo tu, ripoti inaendelea kusema mkataba ulishaisha lakini June 2020 ukaongezwa kwa miaka 2. Hapo Waziri pia alikuwa Kalemani. Unashangaza unapotaka kukwepa ukweli wa Kalemani kuhusika moja kwa moja kwa sababu ni yeye ndie alikuwa waziri, pia ni yeye ndie alikuwa waziri wakati hayo malipo ya 611 M yanafanyika.
 
Kwann yeye alipe MILIONI 600 ndan ya miaka 2 tu?.
Hiyo 612M imelipwa 2020/2021 na 2021/2022 baada ya mkataba kuongezwa chini ya Kalemani. Na hiyo 2020/2021 ambapo malipo ya kwanza yalifanyika baada ya kuongeza mkataba, Waziri alikuwa Kalemani. 2021/2022 alianza Kalemani akaja Makamba. Hata hivyo, ripoti ya 2021/2022 inahusisha takwimu za kabla ya April 2021 na kwahiyo hapo tena waziri alikuwa Kalemani kwa sababu Makamba aliingia nishati Oktoba 2021.
 
Back
Top Bottom