Tanga: Afisa wa TRA ajirusha ghorofani na kufariki

Tanga: Afisa wa TRA ajirusha ghorofani na kufariki

Mfanyakazi wa Mamlaka ya Mapato (TRA) Mkoa wa Arusha, Richard Walalaze (35) amekutwa amefariki baada ya kujirusha kutoka ghorofani jijini Tanga.

Akithibitisha tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Henry Mwaibambe amesema kuwa mfanyakazi huyo amejirusha kutoka ghorofa ya pili ya Hoteli ya Ocean Breez jijini Tanga alikokuwa amepanga chumba tangu Julai 16 mwaka huu.

Mwananchi imefahamishwa kuwa Richard alikuwa miongoni mwa watumishi wa TRA waliokuwa jijini Tanga kwa kazi maalumu ya kuandaa taarifa ya Mamlaka hiyo ya mwaka.

Chanzo: Mwananchi
Uchunguzi ufanyike. Alikuwa kwenye Kuandaa Taarifa maalum sasa iweje ahirushe
 
Kwenye hizi kazi za TRA, Immigration & TPA kujiua ni jambo dogo tu. Huko kunakuwaga na mambo mengi sana.
Na ukipata kazi huko inabidi utafute chemba wakupike haswa!vinginevyo unaweza kuondoka kichwa tu kuuma,kujirusha ghorofani,ajali ya kijinga sana n.kiufupi vifo vya kutengenezwa ni vingi.Umepona sana kufukuzwa kazi.
 
Sio Drc yote kuna vita . Burundi maisha yapo chini na pesa ulizoiba uta enjoy sana
DRC hata kama hakuna vita watu wake sio wastaarabu. Pia machafuko ya hapa na pale huwa yanatokea... kwa mfano Lubumbashi hakuna vita ila siku moja moja mjini kinanuka..
 
Hii habari ina ukakasi sana, ukute karushwa na watu ambao aidha walimuwinda kwasababu ya masuala ya kodi au kuna watu wamepiga hela nyingi kwa jina lake wakaamua kumu- eliminate
Mwezi uloisha alifiwa na baba yake mzazi... akiwa training Tanga hakua na mahudhurio mazuri mpka umauti ulipomkuta.. msikimbilie katika conclusion.. huyo alikua na depression
 
Ana umri gani hadi useme depression? Umesema mwezi uliopita maana yake ni June, ndio aje kufanya maamuzi late july?
Acha kuspeculate vitu ambavyo havipo.. what if hakuwa na mahusiano mazuri na mzazi wake? Depression inampata yoyote na wakati wowote.
 
K
Acha kuspeculate vitu ambavyo havipo.. what if hakuwa na mahusiano mazuri na mzazi wake? Depression inampata yoyote na wakati wowote.
KaWaio conclusion ni alijiua kwa msongo wa mawazo polisi waachane na uchunguzi?
 
DRC hata kama hakuna vita watu wake sio wastaarabu. Pia machafuko ya hapa na pale huwa yanatokea... kwa mfano Lubumbashi hakuna vita ila siku moja moja mjini kinanuka..
Sio wastaarabu kivipi embu niambie hapo maana nimepanga nizamie huko
 
Back
Top Bottom