Tanga: Afisa wa TRA ajirusha ghorofani na kufariki

Tanga: Afisa wa TRA ajirusha ghorofani na kufariki

Hakuwa makini. Ghoropha ya pili ni karibu sana,unaweza usife na huwezi kunyanyuka kwenda kuruka tena ili ujimalizie(kama alipanga kujiua mwenyewe)

Inategemea ameangukia sehemu gan ya mwili, kama ni kichwa hapo ni hatari sana.
 
Wamejuaje kama amejirusha na hajarushwa (Au upelelezi umekwisha na wame-conclude beyond reasonable doubt)
Kuna bahasha ikiwekwa mezani....wewe kama RPC UNAJUA Moja kwa moja kwamba kajiua tu...hata iweje...kama bandari tu usjifanye spika imetoboka unakoroma!
 
Bongo forensic investigation hatupo vizuri...
Hatuna vifaa vya uchunguzi wa kisayansi... Kisha pia angalia taasisi yenyewe ni TRA... Hapo polisi wakija ni mwendo wa pesa mbele na kuandaa ripoti kipesa pesa...

Kuna billionea wa kirusi alianguka kwenye hoteli ghorofa ya 14 miaka kama miwili iliyopita..
Wakaja wachunguzi na vifaa vyao.. Wakascan sakafu/ tiles katika floor ya hoteli baada ya kuchukua viatu alivyokuwa amevaa billionea huyo mara ya mwisho..
Majibu yakaonyesha alipokuwa amesimama kulikuwa na viatu vingine pembeni.. Ikimaanisha wakati anaruka kulikuwa na watu pembeni yake..
Ikafahakima alirushwa kwa nguvu na watu wasiofahakima... Na wakachukua baadhi ya sample kama nguo.. Kujaribu kuestablish dna ya watu waliokuwamo ndani na mtu huyo..
 
Mfanyakazi wa Mamlaka ya Mapato (TRA) Mkoa wa Arusha, Richard Walalaze (35) amekutwa amefariki baada ya kujirusha kutoka ghorofani jijini Tanga.

Akithibitisha tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Henry Mwaibambe amesema kuwa mfanyakazi huyo amejirusha kutoka ghorofa ya pili ya Hoteli ya Ocean Breez jijini Tanga alikokuwa amepanga chumba tangu Julai 16 mwaka huu.

Mwananchi imefahamishwa kuwa Richard alikuwa miongoni mwa watumishi wa TRA waliokuwa jijini Tanga kwa kazi maalumu ya kuandaa taarifa ya Mamlaka hiyo ya mwaka.

Chanzo: Mwananchi
Halafu ni ndugu yetu huyu.. Nitafuatilia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom