Tanga: Auawa kwa kuchomwa kisu, inadaiwa chanzo kumuomba maji ya kunywa aliyefunga

Tanga: Auawa kwa kuchomwa kisu, inadaiwa chanzo kumuomba maji ya kunywa aliyefunga

Wewe ufahamu wako mdogo kama sio mdogo basi unajidanganya, talifa ya kamanda imesema bado awajabaini sababu haswa ya kifo hicho wewe unajifanya kujua chanzo kama sio ujinga nini??
Kajifunze kuandika kwanza ndio uje kujilinganisha na mimi
 
Labda kuna sababu nyingine nje ya hapa binafsi sitaki kuamini kwamba ishu ni maji ya kunywa tu
 
Dar kuna mama alifika dukani kariakoo kununua vitu akiwa na chupa ya maji mkononi, hakuhudumiwa, alipigwa kibao!
Sasa si ndio upuuzi mwenyewe huu. Yani kisa wewe unafunga basi unalazimisha na wengine wote wafunge . Ingekua mimi hapo ndio pangeanza vita ya tatu ya Dunia
 
Hao walikua na yao nyuma ya pazia
HII HAPA HABARI YA GAZETI LA MWANANCHI INAELEZEA VINGINE KABISA
Mkinga
. Mkazi mmoja wa Kijiji cha Vuo, Wilaya ya Mkinga, Amiri Mohamed (24) ameuawa kwa kuchomwa na kisu baada ya kutokea ugomvi wa kugombea maji ya kupikia.
Kwa mujibu wa habari zilizopatikana na kuthibitishwa na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tanga, Henry Mwaibambe ni kuwa mauaji hayo yalifanyika jana saa 4 asubuhi katika Kitongoji cha Vuo, Kata ya Vuo wilayani hapa.

Mashuhuda wa tukio hilo walisema vijana hao licha ya kwamba ni waumini wa dini ya Kiislamu hawana kawaida ya kufunga. Hivyo unapofikia mchana huenda katika kibanda kilichojificha na kujipikia vyakula kisha kula mchana kwa tahadhari ya kuonekana na waliofunga Ramadhani.
"Hakane Nyundo alimfuata mwenzake Amiri na kumtaka ampe maji yaliyokuwa kwenye ndoo ili apikie, lakini Amiri alipokataa, wakashikana. Alipoona anazidiwa nguvu akaenda kuchukua kisu na kumchoma," amesema Husna Hamad.

Mwenyekiti wa Serikali ya Kitongoji, Mohamed Kunema alisema baada ya kuchomwa kisu kwenye ubavu wa kushoto, uongozi ulimuwahisha Kituo cha Afya cha Kiwengu ambako waliamua kumpa rufaa ya kwenda Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga ya Bombo lakini alifariki njiani.

"Hawa vijana hawana kawaida ya kufunga mwezi Mtukufu wa Ramadhani huamua kwenda kwenye mageto kujipikia na kula mchana kwa kificho...Sijui ilikuwaje Nyundo alipoona amezidiwa akaamua kumchoma kisu mwezie," amesema Mwenyekiti.

Akithibitisha habari hizi, Kamanda Mwaibambe amesema Hassan Nyundo anashikiliwa na polisi, baada ya uchunguzi kukamilika atafikishwa kwenye vyombo vya sheria.

Sheikh wa Mkoa wa Tanga, Juma Luwuchu alisema kwa mujibu wa maelekezo. Hassan na Amiri walikuwa wamefikisha umri wa kisheria wa kufunga Ramadhani kwa sababu anayefika miaka 18 anahukumiwa kutenda dhambi asipotekeleza agizo la kufunga.
 

Attachments

  • Screenshot_20230407-170156.png
    Screenshot_20230407-170156.png
    114.3 KB · Views: 3
Ni ulize kwanza?hao wote ni Wanaume?japo majina ni Jinsia ya Kiume!!!
Nina wasiwasi na Maji yaliyoombwa wakati wa Mfungo..
 
Kaua kipindi cha mfungo, na ni kipindi cha toba.
 
Back
Top Bottom