Tanga: DC aagiza polisi kukomesha ukahaba

Tanga: DC aagiza polisi kukomesha ukahaba

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Mkuu wa wilaya ya Tanga Hashim Mgandilwa ameviagiza vyombo vya ulinzi na usalama kuhakikisha biashara ya madanguro maarufu kama madada poa inakoma mara moja Jijini humo.

DC Mganndilwa alitoa agizo hilo wakati wa kikao cha cha baraza la madiwani wa halamashauri ya jiji la Tanga ambapo aliyataja maeneo hayo kuwa ni Sabasaba na barabara ya Uhuru na kusema kuwa wanaofanya biashara kwenye maeneo hayo watafute miji mingine.

"Kuna maeneo kwetu sisi bado kuna, madanguro ambayo dada zetu wanajiuza naomba nitumie hadhara hii kwakuwa vyombo vya dola vipo hapa niwaombe tuanze kushughulika na hawa watu natamani tuone mji wetu unakuwa safi hatutaki kuona hizi biashara za kujiuza jeshi la polisi wakati nikifanya opereshen zenu basi mshughulike na watu hawa, "alisistiza DC Mgandilwa.

Katika hatua nyingine Mgandilwa amesema pamoja na hayo analipongeza jiji hilo kwa kuweza kutatua migogoro mbalimbali ya ardhi na kutaka kuwalipa fidia wananchi ambao bado wana migogoro ya fidia zao lengo ni kuondokana na migogoro isiyokuwa na lazima.

Kwa upande wake Mstahiki Meya wa jiji la Tanga Abdulrahman Shiloo amewataka wakuu wa idara kuheshimu maamuzi yanayofanywa na baraza la madiwani ili kuepukana na migongano isiyokuwa ya lazima inayoweza kukwamisha jitihada za maendeleo kwenye jiji hilo.

"Nitoe angalizo kwa wakuu wetu wa idara na watumishi wote wa halmashauri wapatao 3000 waelewe kwamba kikao cha mwisho chenye maamuzi katika jiji hili ni baraza la madiwani hivyo wasijaribu wala wasiwaze kujikweza kimadaraka hakikisheni sheria kanuni taratibu na miongozo zinafuatwa ili tusifikie kwenye migongano, "alisistiza Meya Shiloo.

Mkurugenzi wa jiji la Tanga Spora Liana amesema Halmashauri hiyo itatoa taarifa ya kila matumizi ya fedha yanayofanywa kwa wananchi lengo ni kuweka wazi kwa kila mwananchi kufahamu fedha za maendeleo zinazotolewa kwenye maeneo yao.
 
Huyo mkuu wa wilaya ajue kqamba ngono inafanyika kwa mashindano kwenye jiji la Tanga

Wapo viongozi hapo wamekua waasisi wakuvunja ndoa za watu, kuhamisha waume za watu au kuwafukuza kazi ili wawachukue wanawake zao. Hilo lipo wazi viongozi wa halmashauri wanajuana.

Wapo watumishi wamepata misukosuko kazini baada ya kuonekana wanakua vikwazo kwenye mahusiano ya baadhi ya wakuu wa idara

Mkuu wa wilaya apambane na watumishi hapo halmashauri ambao ni vinara wa ngono
 
Hii case ww sio wa kwanza kuisemea yupo jamaaa mmoja pia aliwahi kuisemea hii kitu, inabidi niamini kwa sasa hiki ni tatizo
 
Tunamsubiri katibu mwenezi aje awatetee wanyonge hao
 
Wawe serious.

Matatizo ya ubakaji yataongezeka.
 
Nahis madhara yake yanaweza kuwa makubwa kuliko anavyodhania
 
Akisha wahamisha hao Dada poa ,wale Domo zege wasiojua kutingoza atawapa Nini wakishikwa na hamu ya ku duu?
 
Ndoa yangu imeimarika baada ya kuweka dozi kwa madada poa. Huwa naenda kuosha rungu kila wiki mara mbili. Hata bajeti nilishaweka kabisa sh 40 elf kwa mwezi kiroho safi. Ukimwi ukija ntameza dawa na kinga ikiporomoka zaid nakufa. No tatz
 
Back
Top Bottom