Tanga jiji la kishamba sana, nashindwa kuelewa kwanini mkoa huu ulipewa heshima ya kuitwa Jiji

Kiukweli Tanga bado sana. Kuna siku tulikuwa na shughuli ya mdogo wangu alikuwa anaoa. Sasa saloni tu ya kunyoa ni za kawaida sana. Ilibidi bwana harusi anyoe halafu arudi home kuoga na kuvaa. Nikamuuliza kwa nini usingefanya huduma zote huko tukukutane kanisani? Akasema salon haina huduma ya kuoga.
 
Yaleyale......akil za ucku
 
Toa vgezo vya kuitwa jiji zen kumbe kufata sheria n ushamba
 
Nimelazimika kuwakumbuka wabunge woote wa kigoma nikaona wasivyowatendea haki wapiga kura wao.

Hata hiyo manispas sijui hela wanapeleka wapi.
 
Haha naona ukaamua kunipiga picha,aki usiku huu hutolala,damn at u!
 
Hivi ushamba maana yake ni hasa.Na ni nani mwenye dhamana au mamlaka ya ku-decide kwamba huyu/kitu hiki ni cha kishamba na huyu/hiki sio and using what criteria.Na hizo criteria ni nani kaziweka?Je kama hizo criteria sio sahihi,they are only meant to mislead,which is infact the case?

Ni makosa kudhani kwamba gorofa/mavazi/barabara za lami/magari etc. ni maendeleo na kwamba eti mji mkubwa specifically for our case in question ni maendeleo.Laiti ungejua hidden agenda iliyoyoko kwenye urbanization na majumba marefu usingeona ni maendeleo.

Nimalizie kwa kusema wewe unayeona majumba marefu na miji mikubwa ndio maendeleo, ndio mshamba,you have been misled au kwa kiswahili cha mtaani umeingizwa mkenge.Laiti ungejua anayeishi kwenye nyumba ya matope na majani is healthier, kuliko wewe unayebugia masumu yaliyoko kwenye matiles,magypsum,mabati ya kisasa,marangi nk.kwenye hiyo nyumba yako, unayoiita eti ya kisasa, kumbe ndio mauti yako! Pole sana.Kweli usilolijua ni usiku wa giza.
 
Povu la nini kaka? Kwa kifupi mji wa Tanga umejaa umasikini wa kutisha
 
Nasikia huo mji una wakazi wanaoonekana kwa macho na wasioonekana ama wenye uwezo wa kujigeuzi kitu chochote kama kifuu cha nazi , paka n.k
 
Iko hivi Hakuna mji tanzania hii uliopangiliwa vizuri kabisa Town center kama Tanga,Kuanzia Ofisi Za DC na RC njoo barabara za number mpaka Raskazone uko planned poa kweli, Cha Pili Tanga ilipewa hadhi ya jiji kwa vile ilikuwa ya pili ikitoka dar basi ilifata Tanga, Palikuwa na Viwanda kem kem hapo Tanga Ndugu bila kusahau Bandari ya kwanz kwa ukubwa ilikuwa hapo, Kabla ya Dar haijaongezewa kina, Tanga ina neema na kila Tunda linapatikana Pale, Upepo mwanana wa bahari bila kusahau Watoto wazuri, Kuna shida ya kiuongozi ndio imeirudisha nyuma tanga bila kusahau uvivu wa wenyeji na Udini sana but Kiukweli Tanga iko well geographically
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…