Tanga, Korogwe: Ajali yaua 17 na kujeruhi 12

Coaster iliyokuwa imebeba mwili wa marehemu na abiria 26 Ikitokea Dar es Salaam Kuelekea Moshi Kilimanjaro kwa ajili ya mazishi.[emoji848][emoji2827]
Marehemu hakuwa tayari kusafirishwa? Ama kuna mtu hakupenda awepo kwenye msafara?

Kuna watakaokuja kubeza unachowaza....

Ila mara kadhaa tumeshashuhudia waafrika wanagombea maiti kwenda kuzika, ugomvi msibani na kutoelewana kati ya ndugu wa marehemu.

Moja ya maswali yako inaweza kuwa kweli, akipatikana mwana familia wa karibu na marehemu wa kwanza aliyekuwa anasindikizwa kama alikuwa na macho ya rohoni kuna siri mahala.

Kma ni ajali ya kawaida basi kuna liana mahala, ama wazee wa mji/ ardhi anakoenda kuzikwa marehemu hawamtaki....

Mungu awapatie ufumbuzi wapone majeraha ya mwilini na rohoni.
 
Mungu awqsemehe dhambi zao, kifo cha mateso makubwa imetosha.
 
Coaster iliyokuwa imebeba mwili wa marehemu na abiria 26 Ikitokea Dar es Salaam Kuelekea Moshi Kilimanjaro kwa ajili ya mazishi.[emoji848][emoji2827]
Marehemu hakuwa tayari kusafirishwa? Ama kuna mtu hakupenda awepo kwenye msafara?
Inashangaza na huzuni pia, kwa mila yawezekana kabisa, inaogopesha sana, simulizi zijazo tutapata majibu
 
Coaster iliyokuwa imebeba mwili wa marehemu na abiria 26 Ikitokea Dar es Salaam Kuelekea Moshi Kilimanjaro kwa ajili ya mazishi.[emoji848][emoji2827]
Marehemu hakuwa tayari kusafirishwa? Ama kuna mtu hakupenda awepo kwenye msafara?
Kuna namna ngoja tungoje updates zaidi. Hii huwa inatokea sana, hakika kuna vitu huwa havifi unakufa mwili tu
 
Muhubiri 3
1 Kwa kuwa kila jambo na wakati wake, na majira kwa kila kusudi chini ya mbingu.

2 Kuna wakati wa kuzaliwa na wakati wa kufa, wakati wa kupanda na wakati wa kung'oa yaliyopandwa,

3 wakati wa kuua na wakati wa kuponya, wakati wa kubomo na wakati wa kujenga.

4 Kuna wakati wa kulia na wakati wa kucheka, wakati wa kuomboleza na wakati kucheza.

Ufu 14:13
Nikasikia sauti kutoka mbinguni ikisema, Andika, "Heri wafu wafao katika Bwana tangu sasa. Naam, asema Roho, wapate kupumzika baada ya taabu zao; kwa kuwa matendo yao yafuatana nao."

Ayubu 14:1

Mwanadamu aliyezaliwa na mwanamke Siku zake za kuishi si nyingi, naye hujaa taabu."
 
Narudia tena Tanzania ni miongoni mwa nchi hatarishi uwapo barabarani.
Ajali za namna hii zinaakisi akili za watu wetu kwamba sisi ni taifa la wajinga wengi.

Siku moja, nimepewa lift na ndugu yangu mtu mwenye elimu yake na kazi nzuri, lakini namna alivyokua anaendesha ovyo barabarani nikasema huyu lazima apate ajali. Wamenishusha zangu Moro, wao wakielekea Dodoma, baadaye napata taarifa wamekula mzinga gari haifai, yeye na mkewe wameumia vibaya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…