BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,591
- 8,826
Baada ya mvutano wa siku kadhaa kuhusu dhamana ya kada wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) mkoani Tanga, Kombo Mbwana, Mahakama ya Wilaya ya Tanga imeuhitimisha kwa kufunga dhamana yake.
Uamuzi wa kufunga dhamana umetolewa Alhamisi, Septemba 5, 2024 na Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Tanga, Moses Maroa kutokana na maombi ya Jeshi la Polisi.
Kombo ambaye ni Katibu wa Baraza la Vijana wa Chadema (Bavicha) Wilaya ya Handeni Vijijini, anakabiliwa na kesi ya jinai, akidaiwa kutumia vifaa vya mawasiliano ikiwemo kadi ya simu ya mkononi isiyosajiliwa bila kutoa taarifa.
Licha ya mashtaka yanayomkabili kuwa na dhamana, mahakama leo imeifunga dhamana hiyo baada ya Jeshi la Polisi kupitia kwa Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Mkoa (RCO) wa Tanga kuwasilisha pingamizi la dhamana kwa hoja ambazo mahakama imekubaliana nazo.
MWANANCHI
PIA SOMA: