Tanga: Mjamzito adaiwa kufa baada ya kuwekewa damu kimakosa, Watano wasimamishwa kupisha uchunguzi

Informer

JF-Expert Member
Joined
Jul 29, 2006
Posts
1,606
Reaction score
6,672
Watumishi watano wa Kituo cha Afya cha Mikanjuni kilichopo Jijini Tanga wamesimamishwa kazi kupisha uchunguzi baada ya kufanya uzembe uliosababisha kifo cha Mama mjamzito Fatuma Mussa Suleiman (36) Mkazi wa Magaoni, aliyefariki baada ya kuwekewa damu ambayo hakustahili kupewa na hakuwa na uhitaji nayo kwa wakati huo.

Mkuu wa Wilaya ya Tanga, James Kaji amesema kuwa Mama huyo alilazwa katika Kituo cha Afya Mikanjuni March 27, 2204 saa kumi alfajiri kwa tatizo la uchungu ambapo damu aliyowekewa Marehemu ilikuwa ni ya Mgonjwa mwingine ambaye alikuwa amelazwa kwenye kituo hicho akipatiwa matibatu ambapo baada ya kupatiwa damu hiyo Fatuma alianza kuonesha dalili za Mtu mwenye mzio mkali (Allergic reaction) kisha akafariki.

Watumishi hao waliosimamishwa kazi kupisha uchunguzi ni pamoja na Wauguzi watatu Fadhila Ally Hozza aliyekuwa zamu ya mchana, Restitua Kasendo Deusdedit na Muya Ally Mohamed walioingia zamu ya usiku na pia Madaktari waliomfanyia upasuaji Andrew Eliasikia Kidee na Hamis Mohamed Msami.

“Mgonjwa alifanyiwa upasuaji ambapo alifanikiwa kupata Mtoto wa kike wa kilo 3.4 na hakuwa na changamoto yeyote na baada ya upasuaji na aliendelea kupatiwa matibabu chini ya uangalizi wa Wauguzi na Madaktari wa zamu, katika wodi aliyokuwa amelazwa marehemu kulikuwa na mgonjwa ambaye alikuwa anahitaji kuwekewa damu na damu yake ilikuwa tayari imeandaliwa, Muuguzii aliyekuwa zamu alimuwekea Marehemu damu ambayo hakustahili kupewa na hakuwa na uhitaji huo, baada ya kuwekewa damu marehemu alipatwa na mzio mkali (Allergic reaction) iliyopelekea kifo chake”
 
Tukiambiwa tunaishi in a shithole country tunachukia wakati ndio ukweli wenyewe,ndio maana royal families zinakimbilia na kufia Millpark,huu ni unyama wa hali ya juu,inatakiwa kila mgonjwa anafunguliwa faili na ndani ya faili kuna vikaratasi vingi ambavyo vina taarifa yote ya mgonjwa,nurse anapompa maji ya kunywa mgonjwa LAZIMA ajaze kikaratasi hicho na kukibandika kwenye faili la mgonjwa including muda aliompa maji hayo (huu ni mfano),hivyo kwa dawa,sindano na damu (hii ilitakiwa iwe imeshaandaliwa na nani anatakiwa kumpa mgonjwa na sio vurugu hizi ndani ya mahospitali yetu)
 
Watumishi watano wa Kituo cha Afya cha Mikanjuni kilichopo Jijini Tanga wamesimamishwa kazi kupisha uchunguzi baada ya kufanya uzembe uliosababisha kifo cha Mama mjamzito Fatuma Mussa Suleiman (36) Mkazi wa Magaoni, aliyefariki baada ya kuwekewa damu ambayo hakustahili kupewa na hakuwa na uhitaji nayo kwa wakati huo.

Mkuu wa Wilaya ya Tanga, James Kaji amesema kuwa Mama huyo alilazwa katika Kituo cha Afya Mikanjuni March 27, 2204 saa kumi alfajiri kwa tatizo la uchungu ambapo damu aliyowekewa Marehemu ilikuwa ni ya Mgonjwa mwingine ambaye alikuwa amelazwa kwenye kituo hicho akipatiwa matibatu ambapo baada ya kupatiwa damu hiyo Fatuma alianza kuonesha dalili za Mtu mwenye mzio mkali (Allergic reaction) kisha akafariki.

Watumishi hao waliosimamishwa kazi kupisha uchunguzi ni pamoja na Wauguzi watatu Fadhila Ally Hozza aliyekuwa zamu ya mchana, Restitua Kasendo Deusdedit na Muya Ally Mohamed walioingia zamu ya usiku na pia Madaktari waliomfanyia upasuaji Andrew Eliasikia Kidee na Hamis Mohamed Msami.

“Mgonjwa alifanyiwa upasuaji ambapo alifanikiwa kupata Mtoto wa kike wa kilo 3.4 na hakuwa na changamoto yeyote na baada ya upasuaji na aliendelea kupatiwa matibabu chini ya uangalizi wa Wauguzi na Madaktari wa zamu, katika wodi aliyokuwa amelazwa marehemu kulikuwa na mgonjwa ambaye alikuwa anahitaji kuwekewa damu na damu yake ilikuwa tayari imeandaliwa, Muuguzii aliyekuwa zamu alimuwekea Marehemu damu ambayo hakustahili kupewa na hakuwa na uhitaji huo, baada ya kuwekewa damu marehemu alipatwa na mzio mkali (Allergic reaction) iliyopelekea kifo chake”
Nashauri familia ya marehemu ifungue kesi na iweke wakili wahakikishe wanalipwa fisia angalau kuwapooza machungu ya ndugu yao..
 
Huu ni uzembe wa hali ya juu.

1.Hapo huenda hawakukabiziana report vizuri.
Yale yale ya " wagonjwa ni wale wale ameongezeka mama mmoja kafanyiwa Sizaa na kuna damu ya mgonjwa mmoja.

2.Unaenda kutoa Damu ukiwa pekee yako wakati utaratibu unataka angalau muwe wawili.
Ili muweze kuhakikisha.

3. Kuwa karibu na mgonjwa wakati wa zoezi zima la utoaji damu.
Pamoja na kupima vitals.
 
Back
Top Bottom